Kizazi cha watoto wa 2000s kinasikitisha sana katika kufuatilia mambo ya msingi

Mto Songwe

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2023
Posts
6,683
Reaction score
14,060
Hiki kizazi cha watoto wa 2000s kama kinavyoitwa licha ya kwamba sio watoto ila imezoeleka kuitwa hivyo nami wacha nitumie hivyo ili kueleweka zaidi.

Hiki kizazi kwa kweli kinasikitisha sana katika kujikita kufuatilia mambo ya msingi. Ni ngumu sana kutofautisha msomi wa chuo kikuu wa hiki kizazi na yule ambae hata darasa la nne wala saba hakumaliza.

Kwa kweli hawa vijana wanasikitisha sana mambo mengi ya msingi hawayafahamu hasa yanayogusa taifa lao sijui tatizo ni nini? Malezi mabovu ya wazazi au ndio utandawazi?

Moja ya kizazi kitakachokuwa rahisi sana kupigwa propaganda na kutawaliwa na CCM basi ni hiki kizazi cha watoto wa 2000s

Hawa watoto sijui ni nini hasa wanavyowaza vichwani mwao.
 
Generation Z

Bado wanamuda wa kujifunza na kubadilika nafkir ndio wanaingia 23

Wakifika 30s watabadilika
 
Tusikilaumu sana kwa sababu wamezaliwa pamoja na Smart phone ambapo social media zinazungumzia FASHION,NEW TRACK ,AMAPIANO MANGE KIMAMBI APP na CHEKA TU STAND UP COMEDY yaani ni vile ambavyo vinaburudisha ubongo kifupi hawataki habari ngumu ndo maana hata humu Jf hawamo
 
Uwezo na upeo wa kufikiri wa hiki kizazi kupambanua mambo hasa yanayohusu maisha na ubunifu mwingine wa kumfanya asonge mbele bila kushikwa au kupewa support hakuna kabisa!

Kuna msemo unasema SHIDA NI MWALIMU, na hakuna mzazi anayependa mtoto wake apate shida, ila mi nafiriki kukua ukakuta kila kitu kilishapatikana au kuandaliwa nayo wakati mwingine sio nzuri kwa watoto wa kiafrika hasa kizazi hiki cha kuanzia 2000

Kizazi hiki sehem kubwa kinahitaji kukumbushwa kama sio kusukumwa bila hivyo mambo yatakwenda mrama.
Otherwise hakikisha wewe kama mzazi unaweka misingi imara ambayo ukimuachia mwanao kuendeleza ulichokianzisha hakiishi leo wala kesho angalau na wajukuu wakikute.

Mbunge wa Kahama J. Kishimba aliwahi sema mtoto anamaliza chuo anarudi home kugombania remote na wadogo zake lakini pia hata kumtuma mjini huwezi unahisi atagongwa na gari yupo yupo kama kuku wa kisasa! (Ndivyo kilivyo kizazi cha sasa hivi)

Japo mimi nafikiri na elimu na utandawazi nao ni chanzo cha hiki kizazi kuwa kizito kwenye kufikiri.
Profesor Issa Shivji juzi alikuwa analia na swala la midahalo huko vyuoni ni kweli kizazi cha sasa sio hayo mambo ya midahalo yenye hoja za kujenga taifa wala kuhoji.
Kijana aliyemaliza chuo hana tofauti na ambae hakuendelea na masomo wakati zamani utofauti ulikuwepo mkubwa.
 
Nazani SHIDA NI MWALIMU, yaani MWALIMU ndio mwenye shida.

Mbaya zaidi MWALIMU mwenyewe hayupo na akiwepo ima akose kipindi ama akose wanafunzi.

#VIJANA HAWATAKI SHIDA
 
Hiki kizazi cha watoto wa 2000s kama kinavyoitwa licha ya kwamba sio watoto ila imezoeleka kuitwa hivyo nami wacha nitumie hivyo ili kueleweka zaidi.

Hiki kizazi kwa kweli kinasikitisha sana katika kujikita kufuatilia mambo ya msingi. Ni ngumu sana kutofautisha msomi wa chuo kikuu wa hiki kizazi na yule ambae hata darasa la nne wala saba hakumaliza.

Kwa kweli hawa vijana wanasikitisha sana mambo mengi ya msingi hawayafahamu hasa yanayogusa taifa lao sijui tatizo ni nini? Malezi mabovu ya wazazi au ndio utandawazi?

Moja ya kizazi kitakachokuwa rahisi sana kupigwa propaganda na kutawaliwa na CCM basi ni hiki kizazi cha watoto wa 2000s

Hawa watoto sijui ni nini hasa wanavyowaza vichwani mwao.
Kizazi cha mazezeta
 
Kwanza Mleta mada wewe ni wa mwaka Gani?Unatumia Kigezo gani kusema kwamba kizazi cha Y2K kinasikitisha.Kama unawapiwa kwa kutumia uwepo wao JF au wanachofanya mitandaoni basi Fahamu kwamba Jamii forum imeanza mwaka 2005.Internet imeanza 90s kwenda 2000.Wao ndio kizazi ambacho kimelelewa kiteknolojia na watu ambao walikuwa wanajifunza Teknolojia.Yaani Wametukuta tunafuatilia hayo mambo yasiyokuwa ya msingi na kufanya yasiyokuwa ya msingi na wakajifunza hayo kutoka kwetu.Sasa watakapofika wakati wa kuweka mambo yao watakuwa bora kuliko sisi.

Kwa ufupi ni kwamba Hiki kizazi ni Dream Generation.Ni swala la Muda tu.
 
01.Y2K ni kizazi kinachowaza mafanikio bila kujua njia za kuelekea mafanikio.
02.Ni kizazi chavkufuatilia habari za watu kuliko useful infors za uvumbuzi na kujitegemea ndiyo maana uchawa nao ni official job.
03.Kizazi kinachotaka kupata mafanikio,hela umaarufu huku kikiwa kimelala ndiyo maana KUBET,KUTAFUTA FOLLOWERS na D9 ni vitu vilivyopekelewa kirahisi vichwani mwao.
04.Kizazi kisichoamini kutokwa jasho ndiyo maana hata wanaume wanatamani kupata mtu wa kuwalea ndiyo maana ushoga upo ila unaongezeka kwa kasi
05.Kizazi ambacho kimeishiwa nguvu za kiume kwa sababu hakitaki manual works
06.Kizazi ambacho kinakula na ya kutolea kama unabisha mpe mtaji mdogo ako huyo aliemaliza degree ya BCOM in Small Business and Entrepreneurship uone kama hajarudi na ngeu badala ya faida.
 
Hiki kizazi cha watoto wa 2000s kama kinavyoitwa licha ya kwamba sio watoto ila imezoeleka kuitwa hivyo nami wacha nitumie hivyo ili kueleweka zaidi.

Hiki kizazi kwa kweli kinasikitisha sana katika kujikita kufuatilia mambo ya msingi. Ni ngumu sana kutofautisha msomi wa chuo kikuu wa hiki kizazi na yule ambae hata darasa la nne wala saba hakumaliza.

Kwa kweli hawa vijana wanasikitisha sana mambo mengi ya msingi hawayafahamu hasa yanayogusa taifa lao sijui tatizo ni nini? Malezi mabovu ya wazazi au ndio utandawazi?

Moja ya kizazi kitakachokuwa rahisi sana kupigwa propaganda na kutawaliwa na CCM basi ni hiki kizazi cha watoto wa 2000s

Hawa watoto sijui ni nini hasa wanavyowaza vichwani mwao.
Umewaleaje?Walikuwa wanakuelewa katika malezi?Ulikuwa unawafanyia majaribio?Ufaulu wao ulikuaje?
 
Hiki kizazi cha watoto wa 2000s kama kinavyoitwa licha ya kwamba sio watoto ila imezoeleka kuitwa hivyo nami wacha nitumie hivyo ili kueleweka zaidi.

Hiki kizazi kwa kweli kinasikitisha sana katika kujikita kufuatilia mambo ya msingi. Ni ngumu sana kutofautisha msomi wa chuo kikuu wa hiki kizazi na yule ambae hata darasa la nne wala saba hakumaliza.

Kwa kweli hawa vijana wanasikitisha sana mambo mengi ya msingi hawayafahamu hasa yanayogusa taifa lao sijui tatizo ni nini? Malezi mabovu ya wazazi au ndio utandawazi?

Moja ya kizazi kitakachokuwa rahisi sana kupigwa propaganda na kutawaliwa na CCM basi ni hiki kizazi cha watoto wa 2000s

Hawa watoto sijui ni nini hasa wanavyowaza vichwani mwao.
Mkuu zingatia maneno haya, ndio muda wake umetimia.

Nanukuu:

"Hard times create strong men. Strong men create good times. Good times create weak men. And, weak men create hard times"

Mwisho wa kunukuu.
 
Back
Top Bottom