Angalao ninamuunga mkono Stephen Hawking. Mtu akifa, haendi popote.
Gari (mashine) linapofanya kazi vizuri, huo ndio uhai wake. Linaposhindwa kufanya kazi milele, linakuwa limekosa uhai. Halifanyi tena kazi iliyokusudiwa. Linatumika kama skrepa hadi linaisha kabisa. Hali ya gari kufanya kazi (roho) itakuwa imeenda wapi?
Roho za wanyama wengine na viumbe hai wengine ukiondoa binadamu zinaenda wapi? Viumbe hawa wana "destination" gani baada ya kufa? Angalao maandiko yanasemaje kuhusu viumbe hawa wasio wanadamu? Mwenye majibu, tafadhali anisaidie.
Je, tunaweza kufanisha kifo cha "gari" na mwisho wake na kifo cha binadamu na mwisho wake?.
Kwa maoni yangu, kifo ni hali ya kiumbe hai kushindwa kuendelea kujimudu milele. Kujimudu kwa maana ya kwamba mifumo ya mwili inafanya kazi kwa ushirikiano na kwa utimamu. Huu ndio uhai.
Kwa hiyo, kuna hali mbili. Kuwepo na kutokuwepo.
Kuwepo ni mchakato. Kuanzia kutungwa kwa mimba hadi kuzaliwa na kuendelea kuishi.
Kutokuwepo nao ni mchakato ambao unaanza na kiumbe kushindwa kujimudu milele. Hii unaweza kusema ni hali ya kiumbe kupoteza uhai. Kinachofuata ni kumalizika kwa kuwepo ambapo mwili unaoza na kuisha kabisa.
Kwa hiyo, kwa maelezo hapo juu, mwili na roho havitenganishwi. Kwanza hakuna kitu roho. Kuna hali ya kiumbe hai kujimudu. Gani kujiendesha kiutimamu kwa kadiri ya mifumo ya kiumbe hai inavyofanya kazi. Kufanya kasi kiutimamu "in a coordinated fashion" ndiko huko kunakotafsiriwa kama roho. Ila, kimsingi, hakuna kitu roho.
Utimamu wa utendaji wa mifumo ya kiumbe (hai-mfumo wa damu, chakula, n.k pamoja na ogani zoye, viumbe visivyo hai-gari-injini kufanya kazi vizuri, jiwe kuendelea kuwa jiwe, mbao kuendelea kuwa mbao n.k) ndiko kunakosabisha kuwepo kwa hiki tunachokiitaa mwili.
Kukosekana milele kwa utendaji timamu wa mifumo, ndicho kifo. Madhara ya ukosefu wa utimamu wa utendaji hupelekea mwili kuharibika na kisha kupotea kabisa.
Hii inamaanisha kuwa so rahisi kutenganisha hicho kinachoitwa roho na mwili. Hakuna kitu roho wala mwili, bali kuna kuishi au kutokuishi. Kuwepo au kutokuwepo.
Tunachokiona kama mwili ni mchakato wa kutokuwepo tu. Haimaanishi kuwepo kwa kitu mwili bado kuna uwepo.
Kwa hiyo, hakuna kinachoenda popote. Upon au haupo. Basi kama jinsi ambavyo ambaye hayupo, hajawahi kuwepo na hatokaa awepo had I atakapokuwepo.
Unakumbuka uzi wa "Usipokuwepo, hakuna Kilichopo"?. Yani, wewe ndio mwanzo na mwisho wa kila kitu. Hats Mungu hawezi kuwepo bila ya kuwepo wako.
Hata kifo, hakipo bila wewe kuwepo. Usipokuwepo (ukifa au hujazaliwa), hakuna ambacho kipo, na hakuna ambacho kitakaa kuwepo.
Lazima kuwepo kwanza ili kila kitu kingine kuwepo.
Kwenda mbinguni, Motoni, peponi n.k ni hadithi zinazofifisha uwezo wa binadamu. Ni utumwa mkubwa sana.