Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
nimekupata mkuu.
unatuzungumziaje tunaoamini yasiyoonekana kwamba, pamoja na yote tunawajibika kwa maisha yetu Siku ya Hukumu.
Unazungumziaje ufufuo kwa nguvu ya wasioonekana (Mungu), kwa mtu ambaye amekwishakuwa medically confirmed dead.
Uchaguzi bora kabisa katkati ya dunia ya mashaka na kizungumkuti wakifa bila kuwa na tumaini ambalo Mungu ametuletea sisi viumbe wake anaotupenda kupitia Yesu Kristo.Mimi nimechagua kuwa mkristo... Mwamini katika Mungu mmoja kwakuwa nimeuona ukweli
Hiyo ndiyo imani yangu,kama hukuwepo sehemu kabla ya kuzaliwa,hutokuwepo sehemu kabla ya kufa.....wanyama wengine watajua wenyewe.mkuu kama ndiyo hivyo. ilitokeajetokeaje bila kupanga watu bila kujali imani au sayansi zao za kijamii kukuta wanaamini mkanganyiko wa mambo haya na afterdeath scenario.
hukumu ya haki nayo vipi, ipo au haipo. ukifa unakufa tu kama afanyo unintellegent being yoyote kama vile mbu au nyumbu serengeti mto mara.
Mkuu, ni vyema ukimalizia swali lako kwa kisema binadamu wa kwanza kabisa. Ukiuliza aliyemfanya binadamu, jibu ni binadamu. Kila mtu amezaliwa. Ila, swali kuu ni mwanzo wa kila kitu.Sasa nikuulize swali, gari si limetengenezwa na binadamu na lina asli yake (yaani mavyuma) sasa nani aliyemfanya mwanadamu?
Sayansi sio nyenzo madhubuti ya kuhakiki mambo,aghalabu hufeli,sayansi ni ujuzi wa kibinaadamu tuKama ulivyosema ni Imani. Haina basis ya scientific proof
Ndo mana Imani ziko nyingi,kila mtu ana uhuru wa kuamini anachotaka.Ila hawezi kuki parade kama fact kwasababu akijathibitishwa kisayansi
Sayansi ni kifaa duni sana kuhitimishia jambo hili, nakupata mkuuSayansi sio nyenzo madhubuti ya kuhakiki mambo,aghalabu hufeli,sayansi ni ujuzi wa kibinaadamu tu
Kuna wanasayansi makundi mawili, wanasayansi wakubwa kabis lakini wanaamin haya tunayojadili na kundi lingine haliamini.Kama ulivyosema ni Imani. Haina basis ya scientific proof
Ndo mana Imani ziko nyingi,kila mtu ana uhuru wa kuamini anachotaka.Ila hawezi kuki parade kama fact kwasababu akijathibitishwa kisayansi
ubarikiwe mkuu.Naamini katika Kifo na Ufufuko!
Utazika mtu akiwa haiMimi naamini kuwa, kufa ni hali ya moyo kushindwa kusukuma damu. Hivyo hufanya viungo vyote kushindwa kufanya kazi yake na kupelekea milango ya fahamu kushindwa kutoa taarifa.
Ndio maana ili ujue mtu kafa, lazima uangalie mapigo ya moyo
Na mtu akisha kufa, haendi popote, huo ndo unakua mwisho wake
Kifo fumbo ambalo ni kutokuwa na majibu ya haraka sahihi na kwa sababu hawa jamaa hawarudi na hata kama wakirudi hatuwaamini.
1:Wahindu (hinduism)
Hakuna cha mbingu wala jehanam, Mtu akifa anarudi kwenye maisha haya kama kitu au kiumbe kingine.
2:Uislam
Quran 45:26. Sema: Mwenyezi Mungu anakuhuisheni, kisha anakufisheni, kisha anakukusanyeni Siku ya Kiyama isiyo na shaka. Lakini watu wengi hawajui.
hapa inaonekena Hata ufeje, mwili utakusanywa na kutakiwa kusimama mbele ya hukumu. wataalam wanaweza kutupa maarifa zaidi.
3:Wabudha
Hawa wanaamini Ukifa mwili utaoza lkn akili/mind itaendelea kuwepo. Na pia kuna kuzaliwa upya baada ya kifo.
4:Wayahudi/Judaism
Nafsi inaishi milele, mwili ni kama kasha ambalo limeazimwa roho likifa linaoza roho inaendelea kula maisha.pamoja na hili wanamaelezo ya ziada.
5:Wakristo
Hapa wamegawanyika makundi mawili.
wale wanaoamini Mtu akifa roho yake haifi, inaenda kula raha mbinguni, au kama ni ovu inateswa motoni. Pia wapo wanaoamini na mimi nikiwemo mtu akifa ni kaubirini analala usingizi mzuri wa mauti kusubiri hukumu ya haki siku ya kiyama. haendi popote.
6:Mababu zetu na Wababe wakiafrika wanasemaje.
Kifo sio mwisho wa maisha, bali ni mwendelezo wa maisha kwa mfumo tofauti ambao hauna mwili. Kwa baadhi ya mila Kifo ni sherehe maana jamaa anakuwa amehamishiwa katika maisha mengine ambayo ni bora zaidi.
8:Wanasayansi na wasiamini Mungu na Miungu
Hapa nao wanamaoni mengi, ila athiest na mwanasayansi nguli aliyefariki majuzi Stephen Hawking anasema Ubongo ni kama Kompyuta kuna wakati Unachoka unaacha kufanya kazi na kufa. Hakuna chochote mtu akifa, zaidi hakuna cha mbingu wala kiyama wala moto. Hizo ni hadithi za watu Wanaoogopa giza.
vipi wewe unaamini lipi.
Na kuota pindi ulalapo.kifo ni kama kulala usingizi mzito, wafu hawajui neno lolote , umenikumbusha wimbo wa Remy Ongala unasema kifo hakina huruma
mkuu unanikumbusha ya chief songea eti mpokeeni kwanza bwana yesu kabla hamjanyongwa.akawaona wangese akanyongwa akajiendea zake mizimuni huko yupo mpaka leo.Uchaguzi bora kabisa katkati ya dunia ya mashaka na kizungumkuti wakifa bila kuwa na tumaini ambalo Mungu ametuletea sisi viumbe wake anaotupenda kupitia Yesu Kristo.
mkuuMkuu mitale na midimu ubarikiwe kwa mada murua pia napenda utoaji majibu wako kuna watu wamekosoa kwa jazba ila umewajibu kwa busara sana kwa hilo nikupongeze sana
Kwanza nieleze msimamo wangu kuwa naamini mtu akifa anaenda kusubiri sehemu whether paradiso yaani sehem ya mustarehe akisubiri hukumu ya Mungu ama aende kuzimu yaani kwenye mateso ya shetani akisubiri hukumu ya mwisho
Ila nimesoma hapo unasema unaamini mtu akifa analala tu kaburini anasubiri hukumu je una maana mtenda dhambi na mtenda wema wote watasubiri tu kaburini mpaka hukumu??
Je wale wafu aliowafufua Yesu wakapaa naye kwenda JUU kutoka kuzimu walikwenda kusubiria wapi hukumu tofauti na WAOVU waliobaki kuzimu kama Biblia inavyosema kuwa kuzimu itatema wote waliokufa ili wakahukumiwe
Natanguliz shukrani kwa majibu yako