Unabii wa Mama Bikira Maria wa Fatima, umeanza kutimia:
"Siku zile, shetani atafanya kazi zaidi kupitia wanaojiita viongozi wa dini kuliko waumini wa kawaida, na watu wengi watapotea kupitia viongozi hao. Wanadamu wataamini wanamtumikia Baba wa mbinguni, kumbe wanamtumikia shetani"
Malasusa amejiweka wazi sana kuwa ni wakala wa shetani, na kupitia yeye, wengi watapotea.
Mungu wetu, ni Mungu wa haki, ndiyo maana siku zote, tangu enzi, manabii walisimama na wanaoonewa, na siyo na wanaonea. Malasusa ameamua kusimama na wanaowaua watanganyika, Malasusa ameamua kusimama na wanaowateka na kuwapoteza Watanganyika. Malasusa ameamua kulitumia jina la Mungu kufanikisha malengo ya shetani. Lakini, kama ndani ya KKKT, kuna wanaoomba kwa imani, kwa Mungu wa kweli, kwa kuwa Mungu wetu huwasikiliza waombao, kuna wakati utakuja, Malasusa atawekwa pembeni ili asizidi kuwa lango la waumini wa KKKT kumwelekea shetani, na hayo yatatokea wakati ule ambao kila mmoja mwenye macho na masikio atakuwa amefahamu pasipo shaka, kuwa kumbe Malasusa alikuwa ni wakala wa shetani aliyeamua kutumia jina la Mungu wa kweli, kuwapeleka wengi kwenye ufalme wa shetani.