KKKT ni kubwa kuliko Mch. Kimaro, msihuzunike kuna jambo hamlijui, viongozi wake hawajakurupuka

KKKT ni kubwa kuliko Mch. Kimaro, msihuzunike kuna jambo hamlijui, viongozi wake hawajakurupuka

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Naomba nianze kwa kuwapa pole waumini ambao walibarikiwa na mchungaji kimaro!

Kazi ya kitume ni kama mvua, inanyesha kwa wakati wake na kupisha kwa muda ili shughuli zingine zifanyike, mpate muda wa kupanda, kuvuna, na hata kuezeka panapovuja.

Yamkini mvua ya mahubiri ya mchungaji kimaro ilipendwa na wengi, ili stawisha imani za watu wengi, ili punguza joto kali la mizigo.

LAKINI Tusisahau mvua za namna hii kwa upande mwingine zina majanga yasiyoonekana bayana!

Yamkini kupitia mvua hii watu walizibua mitaro yao, yamkini mvua hii ilileta limonia,yamkini kuna mahali palivuja sana.

Hivyo mambo kama hayo huwezi kuyaelewea kama ukiitazama mvua kwa lengo la masika!

Mchungaji ELIONA KIMARO ANAWEZA KUWA NA SHIDA GANI?
Mimi siyo kiongozi wala muumini wa KKKT! Mimi bado natafta kanisa zuri hata humu jf niliwahi kuuliza kanisa gani zuri ili nikajiunge.

Hivyo Kwa uzoefu wangu na elimu yangu ndogo ya kuchunguza matukio kama haya ikiwemo migogoro ya kiimani, kijamii, mauaji, siasa na uchumi n.k

Naweza kusema mchungaji ELIONA KIMARO Ana sifa zifuatazo
  • Mchungaji kimaro analijua andiko analolihubiri
  • Mchungaji kimaro anawajua waumini anaowahubiri na shida zao
  • Mchungaji kimaro anaijua vyema jamii anayo ihubiri
  • Mchungaji kimaro hayumbishwi hasa pale anapokuwa kapanga jambo lake!
  • Mchungaji kimaro siyo msimamizi mzuri wa rasilimali na fedha za kanisa ( fedha ni rahisi kupotea mikononi mwake)
  • Mchungaji kimaro kwa kutambua karama yake anaitumia kuficha madhaifu mengine hasa kwenye matumizi ya fedha!
  • Kuna uwezekano mkubwa wa wa kuonywa lakini kwa kiburi cha kupendwa na waumini aliamini hagusiki!
  • Kwa karama yake ya kichungaji alipogundua viongozi wakuu wake wana jambo naye! Alianzisha semina nyingi za mafunzo ili atakapoitwa WAUMINI Waone kama kuna shida!
ELIONA KIMARO ni mchungaji mzuri sana! Na hili ndilo lengo la makanisa mengi ikiwemo kanisa hili la KKKT!

Lakini kwasababu kanisa lina hitaji uponyaji wa kiroho, kimwili na kiuchumi! Ni lazima VIONGOZI wake wafanye hivyo walivyofanya! Kumuhamisha kwasababu za ndani za kiuchumi! HAWAJAKURUPUKA

Hata viongozi wanaweza kuwa wanampenda sana ELIONA KIMARO Lakini haina budi kupisha eneo hilo linalohitaji usimamizi bora wa kiroho, kimwili na kiuchumi kwa mstakabali wa kanisa zima!

Ikiwapendeza viongozi wanaweza kumrudisha lakini awe chini ya usimamizi wa mchungaji mwingine!
Lakini kwa kutambua nguvu aliyonayo kimaro kuwa chini ya mtu palepale Kijitonyama ni changamoto!

Huenda viongozi wameona ni bora sasa akatumike na kwingine.

Kama lengo lingekuwa moja tu kuinjilisha huenda wangemuacha.

Lakini kwasababu linahitaji kukua zaidi kiroho na kiuchumi, ndiyo maana VIONGOZI WAMEFIKIA UAMUZI HUU.

Endeeleeni kusubiri taarifa ya KKKT lakini nauhakika haiwezi kuwa mbali na maoni yangu.

Wewe unampenda kimaro, Viongozi wanampenda kimaro lakini tusisaha Kanisa la KKKT ni kubwa kuliko Kimaro.

Tuliokaribu naye tumsihi asiwaone wabaya viongozi, alipokee hili kwa wema na akatumike popote atakapopangiwa.

Asikuruouke KUHAMA au KIANZISHA KANISA ATAPOTEA, Atambue kwamba mbio zake ni kama samaki baharini,

Kimaro anaonekana kupiga mbizi za kuvutia akiwa ndani ya KKKT, akitoka inje ATAPOTEA!
KKKT ni bahari inayomfanya a-shine!
Asithubutu kutoka Bali atii mamlaka yake ilivyoamua!

Mapadri wa kikatoliki huhamishwa, wachungaji KKKT huhamishwa, Kimaro asione ajabu kuhamishwa.

Yesu alihubiri Galilaya, Yerusalem, Kapenaumu hata kirindini kwa wavuvi kanisa!

Kwanini KIMARO ang'ang'ane pale pale kijitonyama na sio kwingine? HAMJIULIZI HILO?

JF ukweli na uwazi.

 
Haya mambo yanayotokea makanisani ni kama ya familia, huwa naona yakiibuka wengi hukimbilia kuhukumu kwa kutoa sababu za pesa, au nyinginezo lakini ukweli hawaujui..

Naona wenye familia [waumini] hasa wale wanaohudhuria ibada kwenye makanisa husika, wanaopata nafasi ya kusikiliza mahubiri ya wachungaji husika, hivyo kuzijua tabia zao, ndio waachwe watoe maoni yao, wengine tuwe watazamaji tu.

Kama umeshasema kwa mtazamo wako unamuona anajiamini, hayumbishwi, sasa iweje tena utake mtu wa aina hiyo awekwe chini ya usimamizi wa kiongozi mwingine? unadhani kwa hiyo tabia yake ya kujiamini atakubali kufuata ushauri wa kiongozi wake?
 
Mimi ni Muumini wake mzuri sana pale Kitonyama Mkesha wa Mwaka Mpya nilikuwa hapo na Mch.Kimaro ana Mafundisho mazuri sana hasa ya Ki Imani.

Ila kwenye hili...

Mch.Kimaro anapaswa kuwa na hekima ya ki Mungu sana kwenye hili lililotokea...

Ingewezekana hata ile kuaga angeaga kawaida tu kama Wachungaji wengine wanavyoaga kwenye Sharika zao wakipata Uhamisho ila ile kuaga ameonesha kuna uonevu kafanyiwa.(Ni Mtazamo wangu)

But yote kwa yote sijui nini kimetokea hadi kupelekea hayo..Nimuombee tu yamalizike salama na arejee kwenye kulisha Kondoo wake.
 
Back
Top Bottom