KKKT ni kubwa kuliko Mch. Kimaro, msihuzunike kuna jambo hamlijui, viongozi wake hawajakurupuka

Kila mtu 'aamini kile anachoamini...
Hayo Makanisa ukijiunga wewe inatosha...
 
Huyu mtumishi huwa ninamuelewa sana,wengi wanapiga kelele na kulaumu tu bila kujua kuwa Matamshi ya Mchungaji Kimaro hayaleti picha nzuri Kimaadili ya Kikristo.
 
Moral Theologist tu ndio wanaweza kuelewa kuwa Mchungaji Kimaro ana kosa na kilichofanyika ni sahihi kwaajili ya Ustawi wa roho za waumini.
 
Haya mambo ya Vyeo yanaleta kutukuzwa watu badala ya Mungu. Kiasi kwamba mtu anajiona yeye Yuko juu ya wengine

Bora Mashahidi wa Yehova(JEVOVA's WITNESS) hawana upuuzi huu. Wote mnakuwa wanafunzi wa Biblia.
Lkn Maandiko Matakatifu yenyewe yanatutaka tutii mamlaka,na mamalaka zote zimetoka kwake,kwa hiyo kinyume chake lazima ukutane na mkong'oto tu.
 

Walitaka kumuhamisha lini?
Je, huo ndio utaratibu wa kuhamishwa?
Alikataa kwani akihama si wahumi I wanamfuata au?
Na wa online nimesoma wiki hii ni wengi Sana na ndio wanatoa sadaka kubwa, si watamfata alipo au?
Kariakoo mbona alitoka kwenye wafanya biashara?
 
Umeona eenhh?!!,Angalau wewe ni muelewa.
 
KKK ni taasisi ya kimakabila na wachaga wana nuio la kuamini ni dhehebu lao.
 
Hongera kwa uhandishi mzuri
 
Mleta uzi uko nashukuru kwa uchambuzi wako tena wa bila kuchukua upande, Mch. Kimaro awe myenyekevu na kuwatii viongozi na kuendelea na kazi ya kuhubiri neno la Mungu , asikubali shetani amtie majaribuni, Uongozi wa KKKT nao wasiwe wagumu sana katika hili shauri.
 
Pia ni mkabila yeye anadhani kanisa ni la Wachaga, na wanaotoa mapovu kumtetea wengi wao ni Wachaga wenzake, alishajiona yeye ndie yeye akasahau kuwa kanisa ndilo lililomfanya ajulikane na ndio lililomsomesha hadi akajawa na kibri kwa mwajiri wake, akwende zake akaanzishe kanisa lake na aondoke na hao chawa wake, amelikuta kanisa na ataliacha kanisa.
 
Kweli kabisa mkuu
 
Tatizo kiburi
 
nimecopy vichache tu toka kwenye post yako, hivi hapa

  • Mchungaji kimaro analijua andiko analolihubiri
  • Mchungaji kimaro anawajua waumini anaowahubiri na shida zao
  • Mchungaji kimaro anaijua vyema jamii anayo ihubiri
  • Mchungaji kimaro hayumbishwi hasa pale anapokuwa kapanga jambo lake!
jambo la kwanza kuelewa ni kwamba, kazi ya kuhubiri sio ya mwanadamu, ni ya Mungu mwenyewe kwa njia ya Roto Mtakatifu. mtu asiye na Roho Mtakatifu hana uwezo kuhubiri au kufanya kazi yeyote ya Mungu. why nasema hivi? ni kwasababu hekima ya mwanadamu, elimu au uwezo wake wa kibinadamu hauna nguvu ya kubadilisha roho na kugeuka kuacha dhambi. ila hata tone tu la Roho Mtakatifu likikutana na roho ya mtu kwa kusikia toka kwa watu ambao Mungu anawatumia, linabadilisha. bahati mbaya, huwezi kumpata Roho mtakatifu kama hujaokoka, na kimaro amesoma tu theology ila hajaokoka. hivyo hata Roho Mtakatifu hana, hivyo mahubiri yake yote ni motivation speeches tu.

unasema kimaro anawjaua watu anaowahubiria. kwa kifupi ni kwamba, Mungu ndio anatakiwa awe anatujua, sio sisi. unapohubiri unatakiwa kutumika kama chombo tu, Roho Mtakatifu anakuwa ndani yako, anaongoea toka ndani yako kwa kukutumia wewe kama chombo. hivyo wee hautakiwi kumjua kiundani mtu unayemhubiria, bali Roho wa Mungu ndio anatakiwa kumjua kwasababuu yeye anao uwezo kuchunguza mioyo, na kujua huyu anahitaji Neno lipi. hivyo ukiona mchungaji anahubiri kwasababu anawajua watu anawahubiria jua hata hajui kwasababu uwezo wake kujua watu upo limited, unaishia tu mwilini.

ukisema kimaro hayumbishwi, kama kweli ni hivyo, basi huyo hafai hata kuwa kiongozi. hii ni kwasababu wewe ungekuwa mtu wa Mungu, unawajibika kusikiliza viongozi wako wanasema nini, kama wanasema jambo ambalo sio dhambi, unatakiwa kuwafuata kwasababu ni viongozi wako. huwezi kusema huyumbishwi kwasababu Mungu sio Mungu wa machafuko, ni Mungu wa utaratibu, na anataka watu wawe na taratibu na anakubaliana na jambo ambalo wanadamu wanakubaliana kwa Jina lake. kwahiyo kama mmekublaiana kufuata taratibu fulani za kiuongozi, wewe uliyepo humo kwenye hicho kikundi ukivunja umevunja kitu ambacho hata Mungu aliridhia na ni dhambi. kimaro kuwa mchungaji wa lutheran aliridhia kuwa chini ya taratibu za kilutheri. kuzivunja ni kosa na hawezi kusema hayumbishwi wakati yeye pale ni mwajiriwa tu, kanisa sio mali yake.

mwisho, nawashauri walutherani, mshaurini huyo mwenzenu awanyamazishe wale waumini wake aliowaingiza kwenye usaliti waacha fujo, waendelee na maisha kwasababu, kama kweli wanamwabudu Mungu, hawatakiwi kufuata mwanadamu bali Mungu, na Mungu anaweza kuamua kumtumia yeyote apendaye, hata kama wewe utajiona upo bora kuliko wengine au una umaarufu kuliko wengine.
 
Kiburi ndo shida
 
Yashaisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…