KKKT, Walokole je, ni sawa kwa mwanamke alie kwenye hedhi kuendesha ibada?

KKKT, Walokole je, ni sawa kwa mwanamke alie kwenye hedhi kuendesha ibada?

Kwa nature ya ile kitu ni vyema wasiikaribie madhabahu, maudhi ni mengi, mood swings, chango kali, damu nyingi mwili kuchoka nk
 
sheria za torati zilikuwa za mwilini zaidi, agano jipya lilikazia kutoka mwilini kwenda rohoni. Mambo ya rohoni hujulikana kwa jinsi ya rohoni, fahamu pia kuna tohara ya rohoni
Ni kinyume hata kwa agano jipya kitabu cha 1Timotheo 2 inayohusu maagizo ya utaratibu wa ibada,

1 Timotheo 2:12 >> Simruhusu mwanamke ye yote kufundisha au kuwa na mamlaka juu ya wanaume. Mwanamke anapaswa kukaa kimya
 
Hakuna neno,wote wameumbwa Kwa utukufu wa Mungu,hata mwanamume anazaliwa na mwanamke pia,spiritually we are equal before God,hakuna roho yensi jinsia me Wala ke
 
Hapa suala sio mwanamke yupo mwezini au hayupo, hapa tuelezane tu, huu utaratibu wa mwanamke kuendesha ibada wameupata wapi? kwenye biblia ipi?

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Hakuna neno,wote wameumbwa Kwa utukufu wa Mungu,hata mwanamume anazaliwa na mwanamke pia,spiritually we are equal before God,hakuna roho yensi jinsia me Wala ke
WE ARE NOT EQUAL UNDER OUR CREATOR,

Mwanaume ndie aliumbwa kwanza, Mungu alimuumba mwanamke kama msaidizi wa Mwanaume tena ni kutoka kwenye ubavu wa mwanume...Hio haiji badilika ila ni ruksa kuota
 
Ni kinyume hata kwa agano jipya kitabu cha 1Timotheo 2 inayohusu maagizo ya utaratibu wa ibada,

1 Timotheo 2:12 >> Simruhusu mwanamke ye yote kufundisha au kuwa na mamlaka juu ya wanaume. Mwanamke anapaswa kukaa kimya
sawa, hili fundisho kuna madhebu wanalizingatia sana na hawampi mwanamke nafasi ya kuendesha ibada na kusimama mbele ya wanaume ila madhehebu mengine wanakuambia pazia la hekalu lilipopasuka, patakatifu pa patakatifu pakawa panafikiwa na watu wote, hakuna kizuizi
 
Hata mvua, jua, upepo vinafikia watu wote ila suala la kuwa muwakilishi wa wa shughuli za kitakatifu ni lazima awe mwanaume
 
Hata mvua, jua, upepo vinafikia watu wote ila suala la kuwa muwakilishi wa wa shughuli za kitakatifu ni lazima awe mwanaume
kwa hoja hii huoni kuwa ukikutana na wanaharakati wa masuala ya wanawake utaonekana unashadidia mfumo dume na kuwakandamiza wanawake?
 
Kwamba Mungu anaogopa hedhi [emoji23] kwahiyo huyo Mungu mwanamke akiwa hedhini yeye anakimbia anarudi shetani na hedhi zikiisha Mungu anarudi

Au mimi sijaelewa sababu za kuruhusiwa kutoa mahubiri wakati hana hedhi na kumfukuza kama hana hedhi kwani ina athiri nini!?
 
Hapo zamani KKKT hawakuruhusu ila nadhani walianza kuiga kwa Walokole. Je, kwa mwanamke alie kwenye mzunguko, ni sawa kuendesha ibada takatifu?

Ni kinyume hata kwa agano jipya kitabu cha 1Timotheo 2 inayohusu maagizo ya utaratibu wa ibada.

1 Timotheo 2:12 >> "Simruhusu mwanamke yeyote kufundisha au kuwa na mamlaka juu ya wanaume. Mwanamke anapaswa kukaa kimya."
Halafu kuna watu wanasema uislamu unawanyanyapaa wanawake 🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom