OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Uongozi wa Klabu ya Polisi Tanzania umeingia mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya Sh 50 Milioni na Kanisa la Kingdom Embassy (HPCC) la jijini Dar es Salaam ambao ni maalumu kwa ajili ya kupatiwa maji ya kunywa, fedha na maombi timu inapocheza popote kuhakikisha kwamba wanafanya vizuri zaidi.
Nabii Clear Malisa kutoka Kanisa hilo alisema; “Tutakuwa pia tukijitahidi kuiombea timu yetu kwani maombi ni muhimu ili iweze kufanya vizuri kwenye Ligi.”