Klabu ya Polisi waingia mkataba wa milioni 50 na kanisa kuiombea timu

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001

Uongozi wa Klabu ya Polisi Tanzania umeingia mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya Sh 50 Milioni na Kanisa la Kingdom Embassy (HPCC) la jijini Dar es Salaam ambao ni maalumu kwa ajili ya kupatiwa maji ya kunywa, fedha na maombi timu inapocheza popote kuhakikisha kwamba wanafanya vizuri zaidi.

Nabii Clear Malisa kutoka Kanisa hilo alisema; “Tutakuwa pia tukijitahidi kuiombea timu yetu kwani maombi ni muhimu ili iweze kufanya vizuri kwenye Ligi.”
 
Heri hawa wanamtegemea Mungu kuliko Simba na yanga zinategemea uchawi
 
Huu ni udini wa waziwazi na inafaa upigwe vita. Michezo na dini wapi na wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…