Klabu ya Yanga imemtaka Ahmed Ally kuomba radhi kwa matamshi wanayodai yameichafua klabu yao (Yanga) na wanadai fidia ya Tsh Bilioni 10

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Klabu ya Yanga imemtaka Meneja habari na mawasiliano wa Simba SC , Ahmed Ally kutoka hadharani na kuomba radhi kwa matanshi wanayodai yameichafua klabu yao (Yanga) mbali na hili wanadai fidia ya Tsh Bilioni 10

Kauli ya Ahmed iliyosababisha haya 👇

“Pacome amemaliza mkataba tukiona anafaa tutahangaika nae , Pacome amemaliza mkataba ndani ya Yanga na hana mpango wa kuongeza ..mtanyoa ndevu mwaka huu hana mpango wa kuongeza amechoka kuchomwa sindano kila siku kama anazuia mimba”

“Tunaangalia kiwango chake kama kitaturidhisha tutahangaika nae lakini kama ataendelea na mwenendo wake anaoendelea nao tutawaachia…kama tulivyowaachia Chama na tunataja majina Live hakuna kutumia code”

Soma Pia: Wanasheria wa Sandaland wadai fidia ya Bilioni 3 dhidi ya Ally Kamwe kwa kukashfu Jezi za Simba

Demand letter ya Yanga imeeleza kuwa kauli hiyo ni ya upotoshaji na imejaa dharau kwa klabu yao , hivyo imeharibu mahusiano yao na wadau wa kibiashara na wadhamini

Yanga wanamtaka Ahmed afanye yafuatayo ndani ya siku tano (5)

1.Kuomba radhi kwa njia sawa na aliyotumia kutoa kauli yake

2.Kufidia malipo ya Tsh Bilioni 10 ( 10,000,000,000)

Yanga wamemaliza kwa kusema kama hayo maagizi hayatafanyiwa kazi watafuata hatua za kisheria zaidi

Credit _ @cloudsfmtz
1000327882.jpg
 
Kweli utopolo ni vilaza na huyo mwanasheria wao nae pia ni kilaza hapo kashfa iko wapi? ndo maana hawajawahi kushinda kesi yoyote, Ahmedy asiombe radhi aache hiyo defamation iende mahakamani ili ikatupiliwe mbali alafu Ahmedy awadai tena fidia Billion 10 za kumsumbua maana huyo mwanasheria wa yanga ni zaidi ya kiazi
 
Klabu ya Yanga imemtaka Meneja habari na mawasiliano wa Simba SC , Ahmed Ally kutoka hadharani na kuomba radhi kwa matanshi wanayodai yameichafua klabu yao (Yanga) mbali na hili wanadai fidia ya Tsh Bilioni 10

Kauli ya Ahmed iliyosababisha haya 👇

“Pacome amemaliza mkataba tukiona anafaa tutahangaika nae , Pacome amemaliza mkataba ndani ya Yanga na hana mpango wa kuongeza ..mtanyoa ndevu mwaka huu hana mpango wa kuongeza amechoka kuchomwa sindano kila siku kama anazuia mimba”

“Tunaangalia kiwango chake kama kitaturidhisha tutahangaika nae lakini kama ataendelea na mwenendo wake anaoendelea nao tutawaachia…kama tulivyowaachia Chama na tunataja majina Live hakuna kutumia code”

Demand letter ya Yanga imeeleza kuwa kauli hiyo ni ya upotoshaji na imejaa dharau kwa klabu yao , hivyo imeharibu mahusiano yao na wadau wa kibiashara na wadhamini

Yanga wanamtaka Ahmed afanye yafuatayo ndani ya siku tano (5)

1.Kuomba radhi kwa njia sawa na aliyotumia kutoa kauli yake

2.Kufidia malipo ya Tsh Bilioni 10 ( 10,000,000,000)

Yanga wamemaliza kwa kusema kama hayo maagizi hayatafanyiwa kazi watafuata hatua za kisheria zaidi

Credit _ @cloudsfmtzView attachment 3167601
Kama mbwai na iwe mbwai
 
Young Africans imemdai msemaji wa Simba Ahmed Ali
Aliyeidhalilisha club ya Yanga alipo sema eti Pacome hana mkataba na Yanga na kwamba amechoka kuchomwa masindano kama anazuia mimba.

Kauli hiyo imesabibisha Young Africans kuathirika kibiashara

Young Africans imemtaka Ahmed Ali atoke Hadharani aombe radhi au alipe billion 10 Kwa kufanya defamation Kwa club ya Young Africans

Tukumbuke Young ndo bingwa mara 30

Na pia anawakirisha nchi katika club bingwa

Yanga bingwa
 
Kwa Ahmed hakuna kesi lakini kwa Kamwe ndo kuna kesi au sio Kolo.
Kamwe alikashifu brand ya Sandaland, Ahmedy hajakashifu hapo ili msinde hiyo kesi itabidi kwanza muwashtaki wachambuzi wote wa mpira wanaoiongelea Yanga kwenye media, inaongelewa manchster united sasa utopolo ni nani asiongelewe?
 
Unaipanga Yanga yupi wa kushitaki na yupi wa kuacha
Yanga tunaanza na Ahmed Ali liwe funzo Kwa wachambuzi na wajinga wengine
 
Unamshtaki kwa kosa lipi? Kila kosa lina ingredients zake hilo kosa mnalotaka kumshitaki nalo linaenda kutupiliwa mbali halina tija hajakashif chochote
 
Sawa mwanachama hai wa Rage
 
Back
Top Bottom