Klabu ya Yanga imetangaza kumsajili mshambuliaji hatari Lazarus Kambole

kwa hiyo mmemsajili kwa ajili ya mechi za derby?
 
Mngekuwa hampendi maneno ya kike kike msinge msajili manara dirisha dogo

Mi nacho jiuliza kwanini mmemsainisha mkataba wa pango kama expectation yenu ni vitu vikubwa?

Hao unaowataja kuwa walifeli hawajawahi kuwa na record mbovu ya goli 2 kwa miaka miwili

Na hayo magoli ya kambale hatujatafiti tu kiundani huwenda aliyapata kwenye mechi na timu kama Ken Gold
 
Bora Wawa kuliko huyu galasa, yaani msimu mzima striker ana goli 1 ahahahhaha
 
Bahati na sibu sio kipaumbele na ndio maana tunaangalia statistics

Ingekuwa ndio hivyo basi hata wachezaji wabovu wangepewa nafasi kwa hoja ya kwamba ni bahati nasibu.

Huyu jamaa tuache utani ebu tuongee ukweli tuache mapenzi, inawezekanaje mshambuliaji miaka miwili ukawa na goli 2 kwenye kikosi chenye wachezaji bora?
 
Mmesajili mkaa benchi mwenye goli 2 misimu miwili acha mboyoyo
 
Tumempenda wenyewe,so kama ni galasa nyie Mikia nini kinawauma na si mchezaji wenu?
Hii striker tishio ndio hatutaki huu uongo, haiwezekani striker tishio msimu mzima goli 1, labda mseme tishio wa sura
 
Chico Ushindi kwa mbaaaali nimeanza kumuelewa, itakuwa alikuwa majeruhi wa muda mrefu. Ana ball balance nzuri sana, mwili anao apunguze papara ambazo kwa mbaali nimeanza kuona akizinguza
Chico ni mzuri kuliko Moloko
 
Kwa kambale hapana mzee hii ni record moja mbovu sana

Miquioson alitia kamba mbili kwenye mechi moja tena mechi ambayo ilikuwa ngumu lakini kambale alihitaji miaka miwili kufikisha idadi hiyo
 
Hii striker tishio ndio hatutaki huu uongo, haiwezekani striker tishio msimu mzima goli 1, labda mseme tishio wa sura
Nikama Chama tu,Tz anaabudiwa ila alipokuwa RS Berkane alikuwa anabeba jezi za wenzake, level ya ligi nayo inasadifu, mchezaji anaye kaa benchi Ligi ya Africa Kusini, hawezi kuwa sawa na mchezaji anayeanza kikosi cha Mbeya city
 
Sema hivi wanaosajili ni gsm na wanaolipa mshahara ni gsm
Uto hamna pesa za kusajili chupli chupli sana
 
Morrison alifukuzwa kwa mambo binafsi ya nje ya uwanja, sio huyo mkaa benchi mwenye goli 1 la dawa msimu mzima
Kwahiyo mtu kukaa bench maana yake si mchezaji mzuri Kwa uelewa wako? Unadhani hapo Kaizer alipelekwa tu na mjomba yake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…