KMC wanapaswa kupongezwa sana kwa kujenga KIWANJA kizuri Cha mpira

KMC wanapaswa kupongezwa sana kwa kujenga KIWANJA kizuri Cha mpira

uhurumoja

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2014
Posts
9,616
Reaction score
22,521
Ukiangalia uwanja wa kmc unaona kabisa ni KIWANJA kizuri na chenye standard nzuri ukuta na hata majukwaa na vyumba
Hii Inanipa sababu kabisa ya kuwaomba bodi ya ligi na tff mwakani kuwa team za ligi kuu zitumie
1.Uwanja wa Mkapa.
2.uwanja wa uhuru.
3.uwanja wa Azam
4.uwanja wa Mkwakwani(maana naona unaboreshwa sana )
5.kirumba (endapo pitch itaboreshwa ))
6.Kaitaba stadium (endapo itaboreshwa)
7.Majaliwa stadium
Hivi viwanja ni vingi sana na ni vizuri hakuna sababu ya Kutumia viwanja vibovu kama kile Cha Tabora ,Mbeya ,Dodoma,Singida,Morogoro(Simba walifungwa na mbangula hapa) ,Meja Isamwihyo na viwanja vingine vyote vibaya viachwe kabisa hadi pale vitakapofikia level ya kmc stadium na chamazi
 
Tukiwa serious na masuala ya michezo na jamii kiujumla, huo uwanja wa KMC ni hadhi ya viwanja vya taasisi za elimu hasa shule za msingi na sekondari. Hata kwa level za vyuo vikuu huo ni uwanja mdogo sana. Ukishaanza kutumika tu mtaona baada ya muda mfupi utaonekana hapatoshi utasikia wanataka kuuvunja.

Kama waliona eneo finyu wasingelazimisha kuweka uwanja wa mpira pale, wangejenga tu centre ya kisasa ya ndani ya burudani yenye ukumbi wa cinema na ukumbi wa matukio ya sanaa kama live music, comedy, michezo ya jukwaani, nk.

Halafu kwa nini serikali haifikirii kabisa kujenga maktaba? Kila kata ilitakiwa iwe na maktaba. Katika mazungumzo ya masuala ya elimu sijawahi kusikia mtu akiliongelea hili.
 
Ni wazo jipya yes uwanja ni mdogo lakini pia mechi zao huwa hazijazi sana hata wakicheza na team kubwa ni mwanzo mzuri
Sasa wataelekeza nguvu kwenye arena
 
GPdpSORbYAAAi5J.jpg
nadhani bado awajamaliza kufikia atua ya kuwapa maua
 
1.. Zamani hicho cha Tabora (Ally Hassani Mwinyi) kilikuwa kizuri sana ukikiangalia kilivyo leo daah...aibu.
2. Ccm Kirumba tatizo la pitch la muda mrefu tu
 
Ni matumizi mabaya ya ardhi na pesa za umma. Aliyekuja na hilo wazo na walioamua kulitekeleza wote wamefanya makosa.
Wanapaswa kupongezwa shida ni namna ya kuutunza huo uwanja.
Pia ni sawa Sasa wajielekeze kwenye ujenzi wa sport center ya michezo ya ndani kama netball basketball na handball
 
1.. Zamani hicho cha Tabora (Ally Hassani Mwinyi) kilikuwa kizuri sana ukikiangalia kilivyo leo daah...aibu.
2. Ccm Kirumba tatizo la pitch la muda mrefu tu
Tabora ndio uwanja mbaya zaidi kwa msimu ulioisha wa ligi kuu
Yani ule upigwe ban usitumike kabisa
Kirumba ungeboreshwa na kuwekwa nyasi nzuri kama wanavyofanya Mkwakwani ni uwanja mzuri sana sijui Wana fail wapi.
 
Back
Top Bottom