Mbona ulimbukeni ni neno la kawaida tu labda kama haufahamu tafsiri yake. Kupinga ujenzi wa maktaba tena kwa nchi kama hii ambayo wanafunzi wana uhaba wa vitabu mashuleni, kuna uhaba wa walimu na ukizingatia asilimia ambayo wazazi achilia mbali watoto wana simu janja na ufahamu wa wapi pa kupata hivyo vitabu, mko out of touch kabisa na uhalisia wa maisha ya Watanzania kusema wanafunzi wapakue vitabu online.
Na kama hamjui maktaba ni zaidi ya vitabu, kama ambavyo uwanja ni zaidi ya pitch. Kuna mambo mengi yenye faida yanaweza kufanyika katika mazingira ya maktaba kuanzia mafunzo ya ziada ya ujuzi ambayo wanafunzi hawayapati mashuleni kwa sababu hayapo katika silabasi zao, discussions kati ya wanafunzi wenyewe, mafunzo ya ziada yaani tuition, nk.