Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Hivi kile kikosi kazi kilienda Urambo kuuwa hawa nyoka sijui waliuwa wangapi maana hawa viumbe ni habari nyingine.

Ila kuna huyu ndege anaitwa Secretary bird ni balaa anapiga karate vibaya yaani round ya kwanza tu Black Mamba anasalimu amri
8a6766a8709523bd407ccd5c07712492.jpg
e03eafefc060bab041432bca397ba30b.jpg
 
Hivi kile kikosi kazi kilienda Urambo kuuwa hawa nyoka sijui waliuwa wangapi maana hawa viumbe ni habari nyingine.

Ila kuna huyu ndege anaitwa Secretary bird ni balaa anapiga karate vibaya yaani round ya kwanza tu Black Mamba anasalimu amri
8a6766a8709523bd407ccd5c07712492.jpg
e03eafefc060bab041432bca397ba30b.jpg


Duh kweli kila mbabe na mbabe wake sikuwahi kumjua huyu ndege
 
Pamoja na kusimulia kwa mtiririko unaofaa, lakini wajua kuwa umeharibu sana!!!
1. Unajua kweli maana ya "KITOWEO"
2. Unaposema "kwa kiingereza anaitwa black mamba" sisi kwa kiswahili tunamwita "koboko" sasa imekuaje umeandika nnsha yako kwa kiswahili na umelionea aibu jina "KOBOKO"?


Mwisho nikuulize huyu ndiye hugonga kichwani pekee? Kama siye basi hujamsimulia aliye hatari kuwazidi wote.

Black mamba anagonga sehemu yoyote ndo nyoka mwenye sumu kuzidi wote alafu wanatofauti na king cobra
 
Nyoka hatari sn huyu, ila naskia mkoa wa Mara watu wanawaua sn kwa kutumia manati.
 
kuna wengine wanasema hawa viumbe hukaa sana pia katika mimea ya bangi,hulipenda sana zao hili sijui kama kuna ukweli wowote
 
Eeh acha kabisa Koboko? Nimekumbuka mbali sana. Tulienda kuchota maji kisimani 1997 huko Ujaluoni kijiji ki1 kinaitwa SUDI kule kuna nyoka aina nyingi sijapataona sehem nyingine. Basi ile kuchuchumaa na kibuyu nianze kuchota kaja kichwa juu. Mmh huyu nyoka gani? anaelea juu ya maji anainuka akinasa tawi lo lote anatokomea anarudi anaibukia kwingine kaja mama 1 tukamwambia ee alivyomuona akasema mtulie hivyo hivyo basi kaja kainuka katuzidi urefu then kaingia tena kwenye maji akatwambia rudini nyumbani. Kufika home kumweleza mama eeh ukawa ugomvi karibu na mboko. Dingi kuja akaambiwa nikasikia huyo ni koboko mbaya sana. Osagha osagha
 
Hakuna nyoka namwogopa kama black mamba ... Niliwahi shuhudia aking'ata daktari mmoja na kumuua chini ya nusu saa... Usiombe kukutana nae
Muongo..... Hukushuhudia ulisikia tuu maana hukuwa eneo la tukio wakati nyoka anafsnya yake
 
Nyoka hatari kuliko wote duniani hukaa saehemu tulivu sana isiyo muingiliano wa makelele ya shughuli za binadam, mara nyingine hukaa kwenye pango lenye nyuki na nyuki hutengeneza masega yao wakiacha njia ya mwamba huyu kupita aingiapo na kutoka.

Simulizi za kibantu zinasema "huyu nyoka anaweza kugonga na kuua kundi la ng'ombe hata sabini kwa dakika chache sana".

Simulizi zinatanabaisha kuwa huyu nyoka akionekana maeneo karibu ilikuwa ni jukumu la akina mama kumkabili huyu nyoka kama ifuatavyo:-

Hupika uji kwenye jungu, uji mzito, ukiwa bado wamoto sana wanaweka ngata kichwani na kujitwika huo uji wa moto na kwenda eneo alipo huyo nyoka.

Kwa tabia yake ya kugonga kichwani, nyoka huyu humuendea kwa kasi na kuruka ili agonge kichwa matokeo yake hujikuta ametumbukiza kichwa chake kwenye uji wa moto na kupofuka on the spot!!!!!!

Huo ndio huwa mwisho wa mchezo.

Nyoka huyu aliripotiwa kuingia gerezani huko singida wilaya ya iramba (ushora) na kuua wafungwa wote akapona mmoja tu aliyejitoa muhanga kumng'ata ng'ata shingoni hadi akamuua naye akiwa hoi almanusura.

Kama nyoka wa character hizi ndio koboko basi ni kiboko kweli, lakini kama koboko hana sifa hizi basi yeye sii zaidi ya wote.
 
Nakumbuka alimgonda mtu mpaka katokwa na mavi huku akiwa kakamaa na kufa!!!!!
 
Back
Top Bottom