Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Sifa nyingine ya koboko anaweza kugonga mara nyingi bila sumu yake kupoteza ukali...
 
Huyu tembea yake huwa kama kinyonga tatizo usije mkanyaga, ila niliwahi ona akitoka mbio kuliko koboko tulipokuwa tunachoma rundo la majani kumbe alikuwemo, alitoka speed kali utadhani msafara wa magu vijijini, halafu kinyonga nae huwa maringo nishakuta kinyonga akienda speed ya mjusi akikimbia moto uliokuwa unachoma msitu,
[emoji23][emoji28][emoji23] habari nyingine chief
 
Sijawahi kuona nyoka mpelelezi kama Koboko huwa anasimama ana angalia ndio ana anza kukukimbiza.
black-mamba_thumb.jpg
 
Hao wanyanyembe huwa nawanyanyulia mikono wana madawa koboko mwenyewe anatuliaga.
Mie nimesomea kilw primary, nilishawahi muona jirani yangu akizindika shamba lake porini la mahindi kama heka 10, alipokuwa anazindika ile dawa alikuwa uchi na ilikuwa mida ya jioni, tulienda tafuta matunda flani hivi huwa yanaitwa mantonga wenyeji wa tabora wanayafahamu, wakati tunarudi ndio tukaona hivyo vitimbi, mwenzangu akasema anazindika shamba lake, hakuna mnyama atakayevamia wala kuibiwa mpaka atakapovuna, na ndio ilivyokuwa, manake kule wanyama wa porini ni wengi tu, na kweli mpaka alivuna, nikasema waafrika tuko mbali, hivyo nakubaliana na wewe, wakonongo ni namba nyingine
 
Mikoa yenye koboko wengi sana hapa nchini ni Tabora,Mbeya,Kayavi,Geita ila Geita wanaanza kuoungua kutokana na shughuli za uchimbaji nadini wengi wanahamia Tabora.
 
True! Wanyamwezi mazindiko wanayajua.
Wana zindiko 1 la nyumba lile kiboko, kama mwanga akisogelea anakita nyumba imezungukwa na ziwa, watu asubuhi wanapita kwenda mashambani, wanakuta mtu anapiga mbizi kwenye majani au matuta, hawa jamaa ni kiboko aisee wana watu wao wanazindika wachawi kwamba akirudi tu anakufa wenyewe wanawaita kamchape
 
NI NYOKA WENYE SUMU KUBWA SANA,MFANO TUU BLACK MAMBA AMBAYE HUKU NDIO TUNAMWITA KOBOKO ANAUWEZO WA KUKUGONGA MARA 120 BILA KUCHOKA WALA KUPUNGUZA KIWANGO CHA SUMU ANAYOTEMA KILA ANAPOKUGONGA,SUMU AMBAYO INAKWENDA KUHARIBU NEVA ZA FAHAMU,PIA CHEMBE ZA KUGANDISHA DAMU ILI USITOKE KWENYE JERAHA YAANI PLATELETS HUWA HAZIWEZI ZUIA DAMU ISIACHE KUTOKA,NA PIA HUATHIRI MFUMO MZIMA WA DAMU,NI NYOKA HATARI SANA,
Kwa mujibu wa watalamu nyoka huyu ndiye mwenye kasi kuliko nyoka yoyote wa nchi kavu, anakimbia 20kmp. Labda Bolt anaweza kujaribu kumuacha. [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
hawa jamaa ni kiboko aisee wana watu wao wanazindika wachawi kwamba akirudi tu anakufa wenyewe wanawaita kamchape
Hahaa umenikumbusha mbali mkuu,uzuri wa wataalam wa Mboka huwa wako vizuri.
 
Back
Top Bottom