Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Hao jamaa ni hatari sana, lakini kuna watu wanawakamata kama kuku, hata akiingia ndani ya shimo wanachimba na kumtoa
Kina mfipa 1 tabora anawaua sana na ni bwana mdogo tu, tulipokuwa wadogo niliwahi sikia story kuwa kama ukitaka muua nyoka mwanamke ashike matiti na mwanaume ashike magoti mwingine awe anampiga nyoka anakuwa hakimbii, anabiringita hapo hapo, niliwahi iona hii ukerewe nikiwa nalima na bibi na kweli nilimuua kifutu huku bibi akiwa ameshika matiti, huwa mpaka leo najiuliza wanaposhika hivyo kuna logic yoyote na inafanya kazi
 
Tutakupoteza siku nyingine mkuu cheza na wengine sio koboko.
Tatizo wengi humu ni wanaume wa Dar wanaogopa hata mende

Labda niwafundishe tu kitu kimoja,
Nyoka ukitaka kumuua mpige sehemu yoyote ile hata mkiani, yaani ukishampiga tu ataanza kujibiringisha sababu ya maumivu,

Na hapo ndo unapopaswa kuendeleza mashambulizi,

Huyu KOBOKO kwetu Tunamwita KISANGA na hata Wamasai wakisikia tu hilo jina basi wataanzisha harakati za kumuwinda, wasipomuua ndani ya siku mbili au tatu basi lazima wahame,

Na hao mnaowaita KIFUTU si kwetu tunawaita MOMA hawa bwana kuwakuta ndani ya Nyumba yako ni kitu cha kawaida haswa majira ya Kiangazi, utakuta ukifungua mlango tu ili uingie ndani kama ni usiku au mchana lazima akukaribishe ndani, utasia FOOOOOO, Hapo unajua ndani kuna ugeni, ili kujua eneo alipo wee utaendelea kufuata hiyo sauti maana akihisi unamkaribia na yeye anazidi kufoka, hivyo hapo kuna mawili,

Umtimue atoke nje (kwa kuchoma Chumvi ya mawe kwenye moto) au umuue

Ila ukweli hawa KOBOKO ni hatari sana maana siku hiyo nakumbuka nilikuwa napita tuu njiani nikakutana nae na yeye alikuwa anavuka kuniona badala ya kuendelea na safari yake akasimama yaani kaziba njia kabisa hakuna kupita, nikaagiza ikabidi nimwambie dogo lete Fimbo

Kuna mwingine alikuwa anakuja kuuza dawa za nyoka ye alikuwa anakuja na KOBOKO

Katika NYOKA wote aliokuwa nao huyo ndo alikuwa hamtoi ovyo maana nakumbuka kuna siku ile kumtoa tu akaanza kutoka nduki kilichosaidia aliwahi kumdaka,huyu jamaa watu tulimnyooshea mikono, maana hatujui yule mdudu kamkamata vipi na kamtoaje sumu maana mziki wake sio wa kitoto
 
Kina mfipa 1 tabora anawaua sana na ni bwana mdogo tu, tulipokuwa wadogo niliwahi sikia story kuwa kama ukitaka muua nyoka mwanamke ashike matiti na mwanaume ashike magoti mwingine awe anampiga nyoka anakuwa hakimbii, anabiringita hapo hapo, niliwahi iona hii ukerewe nikiwa nalima na bibi na kweli nilimuua kifutu huku bibi akiwa ameshika matiti, huwa mpaka leo najiuliza wanaposhika hivyo kuna logic yoyote na inafanya kazi
Kunamti ukiweka ndani Huyo jamaa hakai, pia kunadhana iliyojengeka ndani kwa baadhi ya makabila kuwa mwanamke akiingia maziwa nyoka hakimbii lakini hainaukwel nisawa na kuambiwa wakati wa kupiga penati akitokea mchezaji wa tim pizani akashika pumbu zake, mpira hautaenda gorin
 
Wanaosemaga kuwa koboko akikuona huwa anakimbia angalia hii video anavyo wapigia hesabu hawa mapark rangers,huyo aliyekuwa na kamera imebidi aache kurekodi baada Kiboko kuwachenjia kibao.
 
Unamkosea heshima.

Puff ader ametoka kuzaliwa sasa hivi na sasa hivi akikung'ata ujue ndiyo safari hiyo.

Ana camouflage nzuri sana inayomsaidia mawindoni, huko kutulia unakokusema ni sehemu ya mbinu za akiwa mawindoni.

Force anayotoka nayo ili kushambulia windo inatosha kuua windo hata bila kutumia sumu.
Hahahhahaa, ila kuna mwaka flan morogoro tukiwa tunalima na baba yangu mdogo mume wa mama yangu mdogo, sasa wakat analima ghafla kifutu kakimbia, da! Baba mdogo alisikitika sana huku akisema""HUU NI MKOSI, LAZIMA NITAPATA TAARIFA ZA MSIBA KUTOKA MAHALI" "unafikir ilichukua hata masaaa matatu katumwa mshenga kutoka mbali kwelkweli kwamba ndugu yao muhimu kafariki
 
Muwinda huwindwa, hapa tai alimchanganya koboko na nyoka mwingine akagongwa, koboko hakuachia mpaka chui alipotia timu chi nae akapiga kwenzi.

Asante kwa video yako
kiboko ya black mamba na cobra Ni kamnyama kadogo kanaitwa mongoose sijui kiswahili anaitwaje.
wakikutana porini mongoose lazima amuuwe cobra/black mamba au nyoka yoyote mwenye sumu kali nyoka haponi kabisa.
kama Una ranch yako ukifuga hawa wanyama hutaona nyoka akisogea kwako.
Ni kamnyama kana kasi Sana damu yake inavumilia sumu za nyoka halafu anamchokesha kwanza nyoka kama Mohamed Ali anavyokwepa ngumi za mpinzani kabla ya kurusha yake ya KO.
moongose akishamchokesha nyoka kwa kukwepa kila nyoka akiruka kugonga anamrukia nyoka kwa kasi ya ajabu na kumng'ata eneo la Shingo kwa meno yake makali Sana na kuvunja uti WA mgongo WA nyoka hapo tena nyoka Hana ujanja anakuwa chakula ya mongoose
lakini mwisho WA yote sisi binadamu tumepewa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge na nguvu za yule mwovu hazitatudhuru kamwe, Luka 10:19
 
Asante kwa video yako
kiboko ya black mamba na cobra Ni kamnyama kadogo kanaitwa mongoose sijui kiswahili anaitwaje.
wakikutana porini mongoose lazima amuuwe cobra/black mamba au nyoka yoyote mwenye sumu kali nyoka haponi kabisa.
kama Una ranch yako ukifuga hawa wanyama hutaona nyoka akisogea kwako.
Ni kamnyama kana kasi Sana damu yake inavumilia sumu za nyoka halafu anamchokesha kwanza nyoka kama Mohamed Ali anavyokwepa ngumi za mpinzani kabla ya kurusha yake ya KO.
moongose akishamchokesha nyoka kwa kukwepa kila nyoka akiruka kugonga anamrukia nyoka kwa kasi ya ajabu na kumng'ata eneo la Shingo kwa meno yake makali Sana na kuvunja uti WA mgongo WA nyoka hapo tena nyoka Hana ujanja anakuwa chakula ya mongoose
Ni Nguchiro huyo kwa kiswahili
Hii habari nyingine yaani ana tactics nzuri sana za kumkabili adui
Yaani akimuona nyoka tu anacheeeka
 
Wanaosemaga kuwa koboko akikuona huwa anakimbia angalia hii video anavyo wapigia hesabu hawa mapark rangers,huyo aliyekuwa na kamera imebidi aache kurekodi baada Kiboko kuwachenjia kibao.
Duu nimeiona
Halafu nimeiona inayofuatia jinsi mamba alivyomvamia koboko na kumkatakata
 
Nakumbuka siku moja tuko shambani tunavuna mahindi kwa mtindo wa mstari mmoja hatuna hili wala lile, ghafla niliposimama nataka kupeleka mguu mbele nikaona mwili unasisimka, nikasita kwenda kuangukia chini vizuri nikaona huyu jamaa (kule kwetu tunamwita LIMOMA ) katulia zake kimya huko kamkia kanatingishika.

Nikaitisha mundu yenye mpini mrefu na wengine wameshika fimbo, ile kupiga mara moja kwa mundu nikaona imejaa damu.

Tukamtoa na kumwangalia vizuri Ee bwana ehh ni bonge la dude halafu fupi, kuangalia vizuri tumboni ana mayai mengi halafu lina mafuta meeengi.

Mwisho, tukamchoma kwa moto huku tukichukua tahadhari ya uwepo wa dume Karibu yetu.
 
Puff adder ni kifutu ambae ni mfupi na wanauwa sana kuliko hata koboko
Koboko ndio huyu wanaogopa hata kumtaja jina na ndio huyu black mambas
Huyu hapa anaezungumziwa
Hebu msome kidogo View attachment 766058
Khaa!! Yaani ndo Koboko mwenyewe huyu?! Mi nilidhani ni lijijoka flani hivi linatisha ile mbaya!

Oh Lord!! Yaani hivi alivyo alivyo kama ndo ningekutana nae hivi am sure ningemchukulia poa sana... wallah kama ndo angenitisha hivi halafu akaamua kusepa zake, huenda ningemtafutia bakora ili nikamtandike nayo kichwani... manake nasikia ukitaka kumuua nyoka kirahisi; basi mtandike kichwani!!

Kwahiyo wadau mnasema ningejifanya kumdindia ingekuwa ni sawa na kudandia mabasi ya BRT yanayoelekea kuzimu?!

Halafu hiyo kutomtaja jina ndo kwamba ukimtaja tu, Mwana anaweza kuwaibukia; au?!
 
Hizo ni figure of speech tu !una asilimia 99 ya kushinda vita dhidi ya nyoka wakati una less than 10% au no chance at all kushinda vita dhidi ya simba na chui
Ahsante!! Unafanya masihara na Simba nini!! Kuna mdau hapo kadai aliua Koboko kwa mundu; sasa mbele ya mzee simba sidhani hata kama huo mundu wenyewe mdau angeweza kuuinua!

Haya mambo ya simba bora tuwaachie wenyewe Wamasai... tena Wamasai original na sio hawa tunaopiga nao viepe downtown!
 
Back
Top Bottom