Tutakupoteza siku nyingine mkuu cheza na wengine sio koboko.
Tatizo wengi humu ni wanaume wa Dar wanaogopa hata mende
Labda niwafundishe tu kitu kimoja,
Nyoka ukitaka kumuua mpige sehemu yoyote ile hata mkiani, yaani ukishampiga tu ataanza kujibiringisha sababu ya maumivu,
Na hapo ndo unapopaswa kuendeleza mashambulizi,
Huyu KOBOKO kwetu Tunamwita KISANGA na hata Wamasai wakisikia tu hilo jina basi wataanzisha harakati za kumuwinda, wasipomuua ndani ya siku mbili au tatu basi lazima wahame,
Na hao mnaowaita KIFUTU si kwetu tunawaita MOMA hawa bwana kuwakuta ndani ya Nyumba yako ni kitu cha kawaida haswa majira ya Kiangazi, utakuta ukifungua mlango tu ili uingie ndani kama ni usiku au mchana lazima akukaribishe ndani, utasia FOOOOOO, Hapo unajua ndani kuna ugeni, ili kujua eneo alipo wee utaendelea kufuata hiyo sauti maana akihisi unamkaribia na yeye anazidi kufoka, hivyo hapo kuna mawili,
Umtimue atoke nje (kwa kuchoma Chumvi ya mawe kwenye moto) au umuue
Ila ukweli hawa KOBOKO ni hatari sana maana siku hiyo nakumbuka nilikuwa napita tuu njiani nikakutana nae na yeye alikuwa anavuka kuniona badala ya kuendelea na safari yake akasimama yaani kaziba njia kabisa hakuna kupita, nikaagiza ikabidi nimwambie dogo lete Fimbo
Kuna mwingine alikuwa anakuja kuuza dawa za nyoka ye alikuwa anakuja na KOBOKO
Katika NYOKA wote aliokuwa nao huyo ndo alikuwa hamtoi ovyo maana nakumbuka kuna siku ile kumtoa tu akaanza kutoka nduki kilichosaidia aliwahi kumdaka,huyu jamaa watu tulimnyooshea mikono, maana hatujui yule mdudu kamkamata vipi na kamtoaje sumu maana mziki wake sio wa kitoto