Wachezaji wa Simba SC ambao Waliitwa kwenye timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars, wameondolewa kwenye kikosi hicho kwa kushindwa kuripoti kambini kwa muda uliotakiwa
Wachezaji hao ni Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Hassan Dilunga, John Bocco na Shiza Kichuya ambao wote walitakiwa kuripoti kambini jana usiku lakini Aishi Manula pekee ndiye aliyeripoti
Kocha Emmanuel Amunike ametoa msimamo huo, kwamba hataki wachezaji wasiojitolea kwa ajili ya timu yao Taifa.
Wachezaji walioitwa kuchukua nafasi ya wachezaji wa Simba kwenye kikosi cha Taifa Stars ni Salum Kimenya, Paul Ngelema, David Mwantika, Salum Kihimbwa, Ali Abdulkadir, Kelvin Sabato, Frank Domayo.
Mbali na wachezaji hao viongozi wa Simba, Hamisi Kisiwa na Meneja Richard Robert watapelekwa katika Kamati ya Maadili ya TFF siku ya Jumamosi ili kuchukuliwa hatua
Timu ya taifa (Taifa stars) inaingia kambini kujiandaa kupepetana dhidi y ya AFCON.
View attachment 850297
Sent using
Jamii Forums mobile app