Kocha Amunike awaondoa wachezaji wa Simba Taifa Stars kwa kuchelewa kuripoti kambini

Kocha Amunike awaondoa wachezaji wa Simba Taifa Stars kwa kuchelewa kuripoti kambini

Naona Kaingia na LUGOLA STYLE
Ukichelewa unatimuliwa. Je kesho hao hao waliobaki wakitangaza kujiuzulu atacheza yeye,
Lkn pia akumbuke kitendo cha kuengua wachezaji wa klabu mojawapo kubwa tayari ametengeneza Upinzani kwa mashabiki wa Upande huo hawatamuunga mkono kivile kama sio kuzomea. Litazamwe upya hili.
Umeongea point mpaka raha tayari kashagawa mashabiki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dalili za mvua ni Mawingu...huyo kocha kashindwa day one tayari...yeye alivyokuwa timu ya taifa ya Nigeria akichezea vitimu vya "chokochokoroni" wakati akiwahi kambini huku wakina Finidi Geogre na Kanu wakichelewa kambini kutokea Ulaya..walifkuzwa? huyu hatufai tayari

Tulia tuangalie Mchezo Mkuu Huyu Hazijui Fitina Za Bongo! Na akamuulize Masio Maximo yaliyomkuta (Sina uhakika Kama jina lake nimelipatia).

Kwasababu Taifa Stars Hata Kama Hakuwafukuza Zao inajuilikana Kuwa Ni Mbovu itafungwa tu Mbeleni haina Safari. Lakini Sifa ya Wabongo Kwenye Mambo yao Wanakulia Timing tu! Watasubiri Taifa Stars ifungwe Hata Kama Wanajua Kuwa Ni Kawaida Kufungwa! Lakini watakuja na Sababu Kocha Hafai Kwasababu Kawaacha Kina Mkude na wenziwe... Hapo ndiyo balaa itakapomuanzia..
Hill linanikumbusha Kwa Maximo Wabongo Waliposema Tumekosa Kushiriki AFCON Kwasababu Maximo Hamvhezeshi Kaseja.
 
Watanzania ni watu wa ajabu sana...umeshawahi kusikia Ronaldo kaitwa timu ya taifa halaf kachelewa kufika bila taarifa?!..mbona manula kafika kwa wakat hao wenzake kwann wachelewe tena bila taarifa?
Hata kama Manula alifika. Lakini kanuni haikumruhusu yeye kuwahi ni maamuzi tu. Timu inatakiwa kumruhusu mchezaji saa 72 kabla ya mchezo na anatakiwa arudi klabuni kwake saa 24.

Wachezaji hawajavunja kanuni. Tuache mihemko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wachezaji wa Simba SC ambao Waliitwa kwenye timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars, wameondolewa kwenye kikosi hicho kwa kushindwa kuripoti kambini kwa muda uliotakiwa

Wachezaji hao ni Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Hassan Dilunga, John Bocco na Shiza Kichuya ambao wote walitakiwa kuripoti kambini jana usiku lakini Aishi Manula pekee ndiye aliyeripoti

Kocha Emmanuel Amunike ametoa msimamo huo, kwamba hataki wachezaji wasiojitolea kwa ajili ya timu yao Taifa.

Wachezaji walioitwa kuchukua nafasi ya wachezaji wa Simba kwenye kikosi cha Taifa Stars ni Salum Kimenya, Paul Ngelema, David Mwantika, Salum Kihimbwa, Ali Abdulkadir, Kelvin Sabato, Frank Domayo.

Mbali na wachezaji hao viongozi wa Simba, Hamisi Kisiwa na Meneja Richard Robert watapelekwa katika Kamati ya Maadili ya TFF siku ya Jumamosi ili kuchukuliwa hatua

Timu ya taifa (Taifa stars) inaingia kambini kujiandaa kupepetana dhidi y ya AFCON.

View attachment 850297

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama Nidhamu Yeye Mwenyewe Kaikosa! Kama wewe umesahau basi sisi Hatujasahau Kitendo Alichokifanya Yeye na Kina Okocha World Cup 1998 kwa Kudai Pesa za Posho Hadharani Na Kutishia Kugomea Mchezo Wao dhidi Ya Denmark hati Wakaucheza Chini ya Kiwango Wakiwa na Mgomo Baridi.

Sasa Leo Yeye anaona Ajabu Watu Kuchelewa Kambini Wakati Yeye Mwenyewe Ana CV mbovu kabisa Kwa Upande Wa Nidhamu.
Tumempa rungu tukubali matakwa yake. Ndiyo kocha.
 
Hapana za Baba yako... hii sio commedy ni soka huwezi elewa kitu na sio kila kitu lazima uchangie....waache wanaojua mpira wachangie....sijui kama unafahamu hata historia ya Amunike ...pole
Ndio uandish gani?. Hujui kitu na wewe pumba zote ni zako?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata kama Manula alifika. Lakini kanuni haikumruhusu yeye kuwahi ni maamuzi tu. Timu inatakiwa kumruhusu mchezaji saa 72 kabla ya mchezo na anatakiwa arudi klabuni kwake saa 24.

Wachezaji hawajavunja kanuni. Tuache mihemko

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwahiyo manula alikwenda kambini bila ruhusa ya klabu yake?!
 
Hivi kweli huyu kocha mpya anajua mpira wa kibongo kweli

ngoja aje kufungwa hata mechi moja hapo ndo atajua watanzania ni watu wa Aina gani
 
mpira wa kibongo unatawaliwa na SIMBA na YANGA sasa ngoja tushuhudie maneno baada ya kufungwa hata mechi moja wanao msaport kwa sasa ndo hugeuka mwiba kwenye kibarua chake
Kinachotakiwa kocha asingiliwe kwenye maamuzi yake kuendesha timu!
Sema usamba na uyanga ni shida aise hzo timu zinaaribu soko tu la bongo

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mpira wa kibongo unatawaliwa na SIMBA na YANGA sasa ngoja tushuhudie maneno baada ya kufungwa hata mechi moja wanao msaport kwa sasa ndo hugeuka mwiba kwenye kibarua chake
Atajuta kuifahamu bongo
 
tumeshazoea kufungwa hata tukifungwa mara mia mbili siumii tena alichofanya kocha nimekipenda huu umwinyi walionao wachezaji ndio unasababisha tusifanye vizur
 
Kocha kafanya la maana sana, wachezaji wa kibongo wana kua na bichwa sana wakishaanza kusifiwa na kua na kiburi
 
Back
Top Bottom