Sijaandika kwa presha, sijaona kigeni mpaka sasa kwasababu hayo yote Simba kaishayafanya misimu ya nyuma. Kama kumfunga bingwa mtetezi basi Simba ilishamfunga Al Ahly uwanja huu huu. Kama kushinda nyumbani kwenye robo fainali, Simba imeshinda karibia mechi zote ukiachana na mechi ya Tp Mazembe.
Kinachotakiwa sasa ni kuvuka stage na sio kuridhika na hatua moja hiyo hiyo. Binafsi nitampongeza Robertinho kwa kuwatoa Wydad mashindano kwasababu ni muda mrefu Simba haijacheza nusu fainali.
Tufikie wakati tutamani kubeba makombe na sio kuridhika kuishia njiani.