Kocha Mkuu Sven Ven Der Broeck aachana na Simba SC

Kocha Mkuu Sven Ven Der Broeck aachana na Simba SC

Alikuwa si mshirika wa mambo ya PAKA simba wameona anawashika miguu
 
Kuwaweka bench akina kahata, kagere, ajibu na nk ni kutokuwa na huruma na club na wachezaji wenyewe, club imeingia gharama kubwa ya kuwapata unaua vipaji vyao.
 
Simba wangefanya km Tp Mazembe kabla hawajaachana na kocha wa Dragan Cvekovic walimpeleka Pamphile kufanya kozi ya miezi mitatu ktk club ya Standard liege ,kisha wakamrudisha na kumpa timu aiongoze tena kuelekea makundi

Huyu matola Simba ingemsomesha zaidi ,sidhani km Mo anashindwa kumsomesha matola kozi
 
Hizi timu zetu hazitokuja kuacha uswahili!!Sikatai kuondoka kwa kocha,ila kwanini zisiwekwe sababu hadharani ili kila mshabiki na wadau wengine wa soka wajue.

Amesimamishwa Mkude mpaka leo hatujui ni nini kimesababisha kusimamishwa,anaondoka Kocha hatujui ni ninini kimefanya aondoke,sasa mimi nashindwa kuelewa usasa wa timu yetu uko wapi.

Mshabiki na wadau wengine wa tasnia hii ya soka wanatakiwa waheshimiwe pia kwa kupata taarifa ya kila kinachoendelea hasa kwa masuala ya aina hii ili kuondoa ile sintofahamu ya mda mrefu ambayo huweza kuzalisha mifarakano mbalimbali.
 
Umesema vyema, lakin sijaona time inayoandika sababu ya kuachana na kocha, Simba ipo very professional. Kocha kaondoka kwa kuwa amepata mazingira Bora ya kazi zaidi ya haya.
 
Hizi timu zetu hazitokuja kuacha uswahili!!Sikatai kuondoka kwa kocha,ila kwanini zisiwekwe sababu hadharani ili kila mshabiki na wadau wengine wa soka wajue...

Unataka ujue nini cha zaidi.

Mkude utovu wa nidhamu.

Kocha anahitajika na familia yake.

Unataka nini wewe shabiki. Haki yako nikushangilia na kuhuzunika tuu sio zaidi.
 
Simba wangefanya km Tp Mazembe kabla hawajaachana na kocha wa Dragan Cvekovic walimpeleka Pamphile kufanya kozi ya miezi mitatu ktk club ya Standard liege ,kisha wakamrudisha na kumpa timu aiongoze tena kuelekea makundi

Huyu matola Simba ingemsomesha zaidi ,sidhani km Mo anashindwa kumsomesha matola kozi
Inawezekana kuelewa mambo ya darasani hayuko vizuri. Wana notes za kutosha huko. Usione watu hawarudi darasani,wamepima upepo.
 
Itakuwa ameamua kukwepa aibu za zaidi, badala ya kupanga kikosi cha kucheza, anapangiwa kikosi ambacho ni nyau watupu.
 
Sikuwahi kumwamini huyu kocha hata chembe. Mbinu zake ni za hovyo kinachomsaidis ni uwezo wa wachezaji mmoja mmoja kama Chama au mikison.

Ni bora ubaki na Matola kushinda huyo jamaa Van da nini sijui.

I never trusted this guy
 
Huyu kocha alikuwa mpole, nyenyekevu na mvumilivu sana

1.Kikosi anapapangiwa na akina Si OOO na MOO

2.Kaipigwa ambakati bin vitasa vya kutosha na mzee magere halafu analazimishwa champagne

3.Yeye a afundisha mbinu za kisayansi lakini uongozi na management wanamvuruga kwa kuleta tiba mbadala ya PAKA
 
SIMBA SC YAACHANA NA KOCHA SVEN

DAR ES SALAAM: JANUARI 07, 2021

#HABARI: KLABU ya SIMBA SC imetangaza kuachana na kocha wake Mkuu Sven Vanderbroeck kwa makubaliano ya pande zote mbili...
Simba idara yake ya mawasiliano kwa Umma ina shida si bure. Juzi mmesababisha taarifa ya kufungiwa Mkude ilete sintofahamu baada ya kukosa 5W+H, Leo mmerudia tena taarifa ya kuachana na Sven kwa kutoa taarifa inayoelea elea tu.

Mnaficha nini kuwaambia wanachama na wapenzi wenu waliojaa nchi nzima sababu ya kueleweka kwa nini mnaachana na kocha aliyewafikisha pazuri?
 
We unaona alikuwa na msaada? hakuwa na plan B timu inapoelemewa. Na lile li-formation lake la striker 1 ilikuwa inaboa sana...
Wacha mambo ya kitapeli bana...Ulozi una msaada gani Dunia hii?? Hebu fanya wewe ulozi uwe Rais basi au Uwe na Utajiri wa Mo.

Kocha huyu ndio alibeba ubingwa na kafikisha timu hapo..tunaona viwango vya wachezaji akina Chama na mickson wako vzr tu...kubadili kocha katika ya michuano mikubwa hii ni hatari sana lakini kibongo bongo ndio soka letu liko hivyo ndio mana hatuna maendeleo mpirani.
 
Back
Top Bottom