Nakumbuka mwaka 2012 nlikuwa na jamaangu tunabishana kuhusu Messi na Ronaldo, jamaa alikuwa mbishi sana jamaa mshabiki wa Man United, ilivyofika 2015 kuna siku tulikuwa tunaangalia game ya barcelona alinifuata kisiri siri akaniambia kichini chini jamaa zake wasisikie “Ujue me nlikuwa timu Ronaldo ila kwa mabalaa anayofanya huyu mtoto Messi me nimehama ila usiwaambie wana” nlicheka vibaya mno, Messi sio mchezo anaesema Messi ni kawaida we muulize tu nan kaupiga mwingi kuliko messi alafu mwende kwenye data sasa, manake mpira sio maneno mdomoni mpira ni numbers
Huyo rafiki yako ni mfano wa watanzania wengi wajinga, ambao wanaishia kupata msongo wa mawazo kwa sababu wanaamini katika utimu tu kwa kila jambo.
Timu diamond, kiba, harmonize
Timu nandy vs zuchu vs ruby
Timu samia vs magu vs lowassa vs lissu
Timu ccm vs chadema
Timu wasafi vs konde gang
Timu simba vs yanga (hapa ndo headquarters ya mazombie)
Timu Israel vs Palestina,
Timu Russia vs Ukraine
Timu USA & co vs Russia
Timu USA vs China, North Korea, Iran, etc
Timu Messi vs CR7
Uislam vs ukristo (hasa humu jf)
Arusha vs Mwanza, Dar vs Nairobi, kahama sijui na njombe
Na kuendelea
Watz wengi hawana neutrality. Kila jambo ni kulichagulia utimu, matokeo yake ni kuteseka kama huyo mwamba alivyoteseka hadi kuamua kukuvunjia ukimya.
Neutrality ni chanzo cha amani na furaha ya kweli, unaenjoy to the maximum bila mipaka wala unafiki
Sent using
Jamii Forums mobile app