Kocha Mwinyi Zahera aachia ngazi Yanga. Mkwasa kuinoa kwa muda

Bwege sana huyo atuachie timu yetu , imekuwa inaboronga kila siku zinavyozidi kwenda , usajili mkubwa lakini poor performance uwanjani
usajili mkubwa upi? alituaminisha mwaka jana kuwa hakupewa fursa ya kusajili wachezaji anaowataka sasa mwaka huu kapewa nafasi hiyo katuletea makarasha yasiyoeleweka kajaza kwenye timu mara, morogoro sijui, mara bausa mbeba mizigo huko kongo malinga na wengine kibao. Timu haina key player hata mmoja wa garama na mwenye kiwango cha ambaye uwepo wake uwanjani unasababisha hamasa kwa wachezaji wengine? oneni wenzenu mikia, mchezaji mmoja tuu MARIA MAGERE ana uwezo wa kuichochea timu nzima ifanye vizuri na akipata akipata nafasi ya kufunga kama anacheza na maboya kila wakati anafumania nyavu, sasa hii ya zahera mashabiki tumehamasika kuichangia timu, tumenunua jezi za gharama na kila tukienda uwanjani tunapigwa au tunafunga kagoli kamoja kwa mbinde? aondoke tuu na machezaji yake , aondoke tu na shishimbi wake anakuwa na harakati kama za pimbi zisizo na mafanikio, zahera amemtelekeza mchezaji wetu pendwa kampa kampa tena kamusoko akawa hampangi mpaka amechukuliwa na zesco na hatimae kuja kutudhalilisha hapa nyumbani? aondoke bwana aende zake
 
Kwa mujibu wa Shafii Dauda kupitia clouds radio huenda ikawa hivyo. Lakini there was a big campaign against him for long time. Japo siyo jambo la ajabu kocha kuondokewa, kwangu amekua mbuzi wa kafara na hasa kutokana na tabia yake ya kusema ukweli. Ki ukweli kulikuwa na ajenda maalum kupitia vyombo vya habari ku mng'oa zahera na kwa mtizamo wangu imefanikiwa.
Tusubirie mpaka ije kuwa hivyo Mkuu.

Japo nitaumia sababu na mie ni sehemu ya wawekezaji kwenye timu ya Wananchi. Teh teh. [emoji2957][emoji2957][emoji85]
 
Duuh!! Baadae kuna press conference huenda tukayasikia yote hayo Mkuu kutoka kwa Uongozi wa Yanga.
 
Ukiaangalia ukweli wachezaji wetu wengi wazuri aliwapiga pin mpaka wakaondoka , tatizo ana porojo nyingi kama yeye ndo msemaji wa timu !! Nilivyosema usajili mkubwa nimemaanisha wachezaji aliowasajili yeye katika timu yetu ni zaidi ya wachezaji 14 kawaleta , huoni ni kama usajili mkubwa sana
 
Kahojiwa Juzi anaulizia umejiaandaaje na gem ya tarehe 8 na Ndanda anasema hio mechi haitambui na unaweza ukashangaa tukapigwa
Na ukiangalia ule Uwanja huwa hatuna bahati nao si ajabu yakawa kama yale ya Ruvu shooting Taifa yaani tunafungwa kamoja ambako kanadumu mpaka dkk ya mwisho
 
Zahera Asitoke Mapema Hadi Afungwe Na Simba Kwanza.
 
Mikia wako busy sana na suala la Zahera.

Ubovu wa Zahera presumably ni faida kwa 5imba na bila shaka wangeomba sana aendelee kuwepo ili wanufaike. Sasa ajabu eti Mikia wanataka Zahera ang'oke. Ili iweje? Arudi Hans Pluijm na kampa tena?
 
Hatimae Mabingwa wa kihistoria wasio na Kombe lolote huenda wakaingia kwenye mgogoro mkubwa wa malipo kwa Kocha wao Mwinyi Zahera endapo watamfukuza bila kumlipa Mafao yake kwa wakati.Yanga kama tujuavyo bado kiuchumi haiko vizuri hivyo ni vema ilajiandaa kimalipo kabla ya kumfukuza Kocha wao Zahera.
 
Sasa ni rasmi zahera out
 

Attachments

  • IMG_20191105_112331_345.JPG
    59.1 KB · Views: 2
Timu apewe kocha mpya
Nawachagulia kocha ni mzuri anaongoza vizuri na mkali Sana
Mkimpata ubingwa nje nje.....





Duuh nilisahau kuwatajia kocha mkuu
Mecco
 
Hii timu hata akipewa babu Wenga bado itaishia Singida united
 
Namtakia safari njema ya Kurudi kwao na asiache kuondoka na mwanae Molinga maana atabaki mpweke sana. Utabili wa Haji Manara umeshatimia ila msimpige vibao kocha Zahera maana mlitoka nae mbali sana.
 
Daah, nimesikitika kutimuliwa angebaki kidogo ashuhudie ubingwa wa tatu mfululizo ukienda Msimbazi ya NguvuMoja
 
Tatizo la sio kocha. Tatizo ni mfumo wa uendeshaji wa klabu. Wazee waka 10 walipiga pesa kwenye usajili. Wakawagaia watu wa magazeti ili kuwapamba wachezaji.

mimi naona yanga kwa kikosi hiki cha magazetini, bora hata kikosi cha mwaka jana kilikua bora kuliko. Yanga wanatakiwa wafanyie mabadiliko katiba waruhusu mfumo wa hisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…