Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Taarifa za uhakika zinasema kocha Nasreddine Mohamed Nabi, naye anasubiri ruhusa (Approval) ya CAF kumuwezesha kukaa kwenye benchi hapo kesho kwenye mchezo wa Champions League.
Nabi ambaye msimu uliopita alikaa benchi kwenye mechi 2 dhidi ya Rivers United ana vyeti vya UEFA 'A' na UEFA-Pro alizosomea Belgium, lakini taarifa zake zilichelewa kupelekwa CAF.
Habari zaidi zinasema taarifa zake (vyeti) zimewasilishwa CAF na wanasubiri Shirikisho hilo la Soka Barani Afrika, kuidhinisha tu ili akae kwenye benchi kesho.
Hali hii ni kama ambayo imemkuta Kocha Mkuu wa Simba SC Juma Mgunda, ambaye naye anasubiri idhini ya CAF ili naye akae kwenye benchi kesho Jijini Lilongwe kwenye mchezo dhidi ya Nyasa Big Bullets.
Mgunda yeye alichelewa kuidhinishwa kwa kuwa yeye vyeti vyake vimechelewa kuwasilishwa kwa kuwa yeye ni kocha mpya.
============
Updates;
Kocha Mkuu Juma Mgunda amekuwa Approved na CAF hivyo atakuwa kwenye benchi la Simba SC kama Kocha Mkuu katika mchezo dhidi ya Nyasa Big Bullets.
Naye Kocha wa Yanga SC Nasreddine Mohamed Nabi amezuliwa na CAF kukaa kwenye benchi la Yanga kwa kukosa vigezo hivyo Cedric Kaze ataongoza benchi la Yanga kwa mchezo dhidi ya Zalan FC.