Kocha Syllersaid Mziray amefariki dunia, alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa figo

Jina la bwana liabuduwe,poleni wadau wote hususani ktk issue za michezo
mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi aaamin
 
Duh!!! hii imefuata nini huku kwenye jukwaa la mapenzi? au jamaa alikuwa mtu wa *************?
 
Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi!!!!!
 

wala mkuu usiogope kushambuliwa binafsi najua alikua anamchukua dada mmoja mitaa ya ukonga mzambarauni sasa sijui kama kuna wengine, ili liwe fundisho kwa dada zetu wanaopenda watu maarufu na wenye pesa, wasione vinaelea!
 
Kocha msaidizi wa timu ya Simba, super coach, Syllersaid Mziray amefariki dunia leo asubuhi akiwa katika hospital ya Aga khan alikokuwa amelazwa.kocha huyo maarufu ambaye alikuwa mshauri mkuu wa simba alifikwa na umauti huo baada ya kuugua kwa muda mrefu.
 
Poleni watanzania na wapenda michezo wote
moyo wangu u pamoja na wafiwa kwenye kipindi hiki kizito kwao
 
Ooh GOD! tumepoteza mmoja wa makocha wazalendo na adimu kabisa kwa hivi sasa, poleni wafiwa wote!
 
Duh!!! hii imefuata nini huku kwenye jukwaa la mapenzi? au jamaa alikuwa mtu wa *************?

Mkuu what ever the guy had done, in sports or whatever, anastahili heshima. Mchango wake pamoja na kuwa na utata ulilisaidia taifa.Lakini kweli ni ajabu kwanini imeletwa huku, how come habari ya kusikitisha ikawa kwenye jukwaa kama hili?
 
Finally, "the super coach" mziray is dead:

Tangazo la msiba halianzi na "Finally fulani kafa..." Ulikuwa unasubiri afe? Finally ni kama alikuwa anategemewa, anatakiwa, afe halafu hafi mda unakwenda! Jifunze kuwasiliana.
 
RIP Mwalimu Mziray,you are my hero in ways more than one,ubavu wako wa kutoa hoja nzito katika sekta ya michezo hata kama zinaudhi wakubwa haukuwa na mfano. Mod habari hii ni kubwa na nzito sana sana katika duru la michezo nchini mwetu.Ninakuomba uhihamishie kwenye mada ya michezo au habari mchanganyiko na sio huku kwenye raha,mapenzi na starehe..Natanguliza shukrani.
 
RIP Super Coach Syllersaid Mziray,kumbe wakati ulipoanza kuonekana unapata nafuu ndiyo safari ya kurudi kwa baba ilikuwa imekaribia! Mungu anayehukumu kwa haki atatenda sawa sawa na neno lake! Amen
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…