Kocha Syllersaid Mziray amefariki dunia, alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa figo

Kocha Syllersaid Mziray amefariki dunia, alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa figo

Mbona kuna post imewekwa kua Mzirai kafariki hebu tupeni habari vizur
 
Nitamkumbuka kwa mbwembwe zake tuu za maneno ya apa na pale.
RIP
 
habari zimeingia asubuhi hii zinasema super coach syllesaid mziray amefariki dunia alfajiri ya leo katika hospitali ya aga khan jijini dar alikokuwa amelazwa akisumbuliwa n malaria. Habari za mipango ya mazishi zitafuata mara tu baada ya kupatikana.



coach mziray , aliyekuwa mwajiriwa wa chuo kikuuu huria kama mhadhiri, atakumbukwa kwa umahiri katika ufundishaji soka katika vilabu mbalimbali hadi timu ya taifa iliyoshinda ubingwa wa nchi za afrika mashariki. Alifundisha pia pilsner, simba, yanga, pan african na kabla ya mauti kumkuta alikuwa mwalimu wa viungo na saikolojia wa klabu ya simba.

globu ya jamii inaungana na watanzania wote kuomboleza msiba huu mzito ambao ni pigo kwa tasnia ya michezo nchini ukizingatia tuna makocha wachache waliosomea fani hiyo na kubobea.

mola aiweke roho ya marehemu
mahala pema peponi
- amin
 
Back
Top Bottom