Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 2,818
- 7,940
Mpira sio uadui; mpira ni furaha, burudani na umoja. Kitendo kinachodaiwa kufanywa na kiongozi wa Yanga cha kumpiga ngumi kocha wa Gaborone United kinaharibu taswira ya mpira wa miguu nchini Tanzania.
Matukio ya aina hii yanaweza kugeuza mpira kuwa uhasama, jambo ambalo ni hatari zaidi katika mechi za kimataifa ambazo zinapaswa kutuunganisha, kutangaza nchi yetu na kujenga heshima ya Tanzania kimataifa.
Tumetumia miaka mingi kujenga taswira nzuri ya Tanzania katika soka. Hatuwezi kuruhusu taswira hiyo iharibiwe na vitendo vya watu wachache vinavyokiuka misingi ya nidhamu na ustaarabu wa michezo.
TFF, suala hili lisipuuzwe. Wale wote watakaothibitika kuhusika wachukuliwe hatua na kupewa adhabu stahiki kwa mujibu wa kanuni za soka. Tusubiri hatua kabla mambo hayajawa makubwa zaidi.
Tuilinde heshima ya Tanzania. Mpira ubaki kuwa mchezo, sio uwanja wa visasi na uhasama.