Dr Restart
JF-Expert Member
- Jul 15, 2021
- 4,949
- 24,046
Shirikisho la Soka barani Africa (CAF) limetoa orodha ya makocha ambao hawatoruhusiwa kuwa sehemu ya benchi la ufundi katika timu zao kwa kukosa vigezo vya leseni ya CAF A na UEFA PRO.
Didier ambaye ana diploma ya UEFA A, hajakidhi vigezo vilivyowekwa kwa kocha Mkuu kuwa na leseni ya CAF A ama UEFA PRO.
Katika maelezo yaliyotolewa na CAF, kocha Mkuu anapaswa kuwa na leseni tajwa hapo juu huku kocha Msaidizi akipaswa kuwa na CAF B.
Kocha ambaye hatokidhi vigezo tajwa hatoruhusiwa kuwa sehemu ya benchi la ufundi wakati wa mechi za Ligi ya Mabingwa na kombe la Shirikisho.
Hatua hii imefikiwa na CAF ili kuleta thamani na ubora katika michuano hiyo. Hii ni ili kuleta maendeleo katika soka la Africa kwa kuhakikisha kuwa vilabu vinafunzwa na makocha wenye viwango toshelezi katika madaraja ya juu.
Pamoja na kocha Didier, makocha wa klabu za APR, KMKM, El Mereikh na wengine hawatoruhusiwa kuwa sehemu ya benchi la ufundi katika mechi tajwa.
Simba huenda ikawakosa kocha Mkuu na kocha Msaidizi kwa kuwa kocha msaidizi Ndg Selemani Matola ana lesenu ya CAF C ambayo haikidhi vigezo vya kuwa kocha msaidizi.
Simba wana kazi ya ziada ya kufanya.
Naipenda Simba Mshabiki wa Damu.
Pia, soma=> Simba: Kocha Gomez anasoma online course, tuna imani hadi mchezo wetu unachezwa atakuwa ameshamaliza masomo