Kocha wa Simba SC, Pablo Franco ni Kocha mzuri ila anahitaji wachezaji

Sio kocha Yule ni mkandalasi
 
Kwangu bado naona kuna vitu anafosi havina faida, mpaka leo kanoute kashindwa kunishawishi kwa kweli bado anae tu, si aina ya midfielder wa kukamata dimba, akaweza kucommand timu yake na timu pinzani, soka tjnalopenda simba tunahitaji mchezaji wa namna hii, mwenye kuweza kugusa kila nyasi iliyopo uwanjani, kanoute bado katika hili, mugalu kila nikimtizama mimi hanishawishi sio striker wa kuingia uwanjani ukategemea goli toka kwake ama wapinzani wakawa wana mgwaya.
 
Wachezaji wa kigeni mwisho nane tu mkuu...
PB isingewezekana kuwepo.
 
Gadiel ???
 
Mkuu tunatofautiana kwa kanoute....
Kwangu mimi lazima aanze hata jana alipoumia nilikuwa kichwa chini.
Mid mzuri sana ila Mkude ndio Hapana.
 
Wengi wenu naona mnapoint wachezaji wa kuondoka bila kusema timu ijengwe vipi.

Ukiangalia kikosi chetu kwa sasa kuna wachezaji karibia 7 waliotupa mafanikio misimu minne iliyopita wanaweza kuondoka mwisho wa msimu kutokana na kukosa makali au umri wao kuwatupa mkono.
1. Paschal Wawa
2. Erasto Nyoni
3. Meddie Kagere
4. John Bocco
5. Tadeo Lwanga
6. Rally Bwalya
7. Bernad Morisson
8. Hassan Dilunga.
9. Gadiel Michael

Hii ni idadi kubwa sana ya senior players ambao yawezekana zaidi ya nusu yao hatutakuwa nao msimu ujao.

Wapi tuboreshe kwa usajili upi na yupi abaki kwenye hiyo list.?

Kwa upande wangu mimi naona Simba wanahitaji kusajili DM mwingine local mchanga na kwa haraka haraka namuona Aziz Andabwile wa Mbeya City kuwa best pick au Kelvin Nahashon Naftali wa Geita Gold FC.

Kwa upande wa left back Simba wanahitaji back up nzuri zaidi ya Gadiel kwangu mimi namuona Kouassi Attohoula Yao wa Asec Mimosas 25 years of age.

Upande wa kulia iwapo Simba watafanikisha kumsajili Victorien Adebayor waachane na Morisson tayari tuna best wing upande huo ambaye ni Peter Banda, Kibu Denis, Hassan Dilunga. Iwapo Simba wataachana na Dilunga msimu huu warudi pale Azam wakamchukue Tepsie Evans ni fringe player mzuri kwa timu kama Simba.

Upande wa central midfield uwezo wa Bwalya hauongezeki tena tunahitaji a more imposed na creative midfielder zaidi yake Simba wamuone Gilbert Beruti kuwa best like to like replacement ya Bwalya ambaye anaweza kucheza position ya Chama pia anapoflop.

Kuondoka kwa Wawa na Nyoni kutatuachia pengo kubwa sana kikosini kwetu tunatakiwa kupata either local versatile player lakini kuziba pengo hilo ni kuwanyang'anya utopolo yule Yannick Bangala by the way ana mkataba wa mwaka mmoja tu.

Kwenye defensive Midfield akiondoka Tadeo Lwanga na kutokana na injury records zake ni heri tuvunje benki tuende TP Mazembe kumchukua Zemanga Soze au tubaki na tulionao.


Kwenye striking force tunahitaji local striker ambaye atakuwa like to like replacement ya Bocco kwangu mimi namuona Lusajo Reliant amekuwa consistent kwa misimu mingi kwa timu kubwa kama Simba tunaweza kunufaika nae wakati huo tukitafuta mbadala wa Kagere na Mugalu though naona bora kubaki na Mugallu ili tusipoteze wote.
 
Sawa mkuu huenda sikuelewa context ya comment yako
Maoni yako mkuu wapi tufagie? Pablo anatosha?
Kwangu mimi....

Onyango akidai hela nyingi aende, Simba wakiwa wanaimudu hiyo hela wampe.

Morrison aende sawa akibaki sawa....

Kagere aende....

Mugalu aende sawa akibaki sawa......

Wawa dah kama mkataba umeisha astaafu tu kwa heshima, ni ngumu kumkataa moja kwa moja ( Tunatakiwa kuheshimu royalty).

Moses Phiri akija safi.....
Tukiongeza kiungo mkabaji ( mkali wa nje) safi.....
Huu ni Upande wa wachezaji wa Nje.
 
Out.
1. Rally Bwalya
2. Morisson
3. Nyoni
4. Gadiel
5. Kagere
6. Bocco/ Mugallu
7. Lwanga
8. Wawa.

Ins.
1. Aziz Andabwile
2. Zemanga Soze
3. Attohoula Kouassi Yao
4. Moses Phiri
5. Victorien Adebayor
6. Gilbert Beruti
7 Yanic Bangala
8. Tepsie Evan's na Israel Sospeter Bajana.
 
Illmatic
 
Kama ni hivyo basi kusingekuwa na usajili wa dirisha kubwa na ndogo.

Kagere, Bocco, Mugalu ni wachezaji ambao tunawaheshimu kwa kuitumikia Simba kikamilifu..!
Basi msimu ujao tuwapeleke wakacheze timu mojawapo kwa mkopo. Tusajili wengine ili tuwe na Kikosi cha Maangamizi msimu ujao.
 
Ushauri mzuri sana huu ndugu PTER . Sijui kama viongozi wa Simba ushauri huu utawafikia. Naomba uwapelekee kupitia kurasa zao rasmi za mawasiliano za mtandao!
 
zemanga sonze πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯🀝
 
Ushauri mzuri sana huu ndugu PTER . Sijui kama viongozi wa Simba ushauri huu utawafikia. Naomba uwapelekee kupitia kurasa zao rasmi za mawasiliano za mtandao!


Mkuu viongozi wa Simba huwa wanafuatilia kwenye hiyo thread nilisugest Simba wamsajili Tadeo Lwanga baada ya mashindano ya AFCON ambayo na taifa stars tulicheza kwenye dirisha dogo last season wakamleta.

Hata kwenye hiyo orodha yawezekana Aziz, Gilbert, Zemanga Soze, Lusajo wakawa wekundu next season
 
Kwa kanoute nakupinga, yupo vizuri sana, na ameshadhihirisha hilo, sema hanaga mambo ya jukwaani,

Kanoute abaki na awepo sana tu.
 
Hapo kwa Aziz na yanick, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…