Kuna siku nilikuwa nafatilia interviews za matukio baada ya mechi.
Kuna mwana yanga mmoja alitoa ushauri ambao binafsi nakubaliana naye kwa % kubwa.
Alisema tanzania tunaweza tukajijenga vizuri kisoka na tukafanya mambo makubwa ya kuwashangaza mataifa mengine endapo tutakubali kuwa wachoyo
Kwamba leo tukicheza na timu kubwa pinzani, wachezaji wetu wataoonesha ubora zaidi na kuwafanya timu hizo pinzani zisifunge basi management ya timu hizo zitataka kuwanunua hao.
Tatizo linapokuja ni baada ya sisi kuwauza hao wachezaji wazuri na kubakisha hawa wenye average ya kati.
Sasa badala ya hizo Pesa tulizopata baada ya kuuza wachezaji wetu kwa Pesa kubwa tuzitumie kununua wachezaji wengine wakubwa wa aina hiyo au zaidi ya hapo ikiwezekana hata katika hiyo Pesa tuongeze na nyingine ili kupata mchezaji mwenye uwezo wa juu kufikia malengo, tunaanza kuhangaika na sajili za laki mbili mbili eti tuwakuze.
Hapa katikati tutatumia muda mwingi mpaka kunijenga wakati wenzetu wahafika mbaliz na kukishajijenga watakuja tena na madau yao kununua wachezaji ambao wao wanawaona ni tishio kwao.
Kwanini tusiwe wachoyo tusikubali kuwauza, au tuwauze kwa bei kubwa afu tununue wa aina hiyo au zaidi ya hao?
Na ndio maana tunaishia kufukuza makocha, lakini sio kweli kuwa kila matokeo mabaya yanayopatikana basi Sababu ni kocha.
Simba inabidi ifahamu kuwa saizi ni muda wa kufanya makubwa zaidi ya kuishia robo, Wafanye sajili kubwa tano za maana.
Mugalu asepe, bocco tunamheshimu lakini hatuna namna, kagere plus na umri hata yeye mwenyewe analijua, wawa hatufai ana vi cross vya hovyo sana, sakho akishindwa kujirekebisha na tabia yake ya kucheza na jukwaa afungashiwa vilago...
Wengi wenu naona mnapoint wachezaji wa kuondoka bila kusema timu ijengwe vipi.
Ukiangalia kikosi chetu kwa sasa kuna wachezaji karibia 7 waliotupa mafanikio misimu minne iliyopita wanaweza kuondoka mwisho wa msimu kutokana na kukosa makali au umri wao kuwatupa mkono.
1. Paschal Wawa
2. Erasto Nyoni
3. Meddie Kagere
4. John Bocco
5. Tadeo Lwanga
6. Rally Bwalya
7. Bernad Morisson
8. Hassan Dilunga.
9. Gadiel Michael
Hii ni idadi kubwa sana ya senior players ambao yawezekana zaidi ya nusu yao hatutakuwa nao msimu ujao.
Wapi tuboreshe kwa usajili upi na yupi abaki kwenye hiyo list.?
Kwa upande wangu mimi naona Simba wanahitaji kusajili DM mwingine local mchanga na kwa haraka haraka namuona Aziz Andabwile wa Mbeya City kuwa best pick au Kelvin Nahashon Naftali wa Geita Gold FC.
Kwa upande wa left back Simba wanahitaji back up nzuri zaidi ya Gadiel kwangu mimi namuona Kouassi Attohoula Yao wa Asec Mimosas 25 years of age.
Upande wa kulia iwapo Simba watafanikisha kumsajili Victorien Adebayor waachane na Morisson tayari tuna best wing upande huo ambaye ni Peter Banda, Kibu Denis, Hassan Dilunga. Iwapo Simba wataachana na Dilunga msimu huu warudi pale Azam wakamchukue Tepsie Evans ni fringe player mzuri kwa timu kama Simba.
Upande wa central midfield uwezo wa Bwalya hauongezeki tena tunahitaji a more imposed na creative midfielder zaidi yake Simba wamuone Gilbert Beruti kuwa best like to like replacement ya Bwalya ambaye anaweza kucheza position ya Chama pia anapoflop.
Kuondoka kwa Wawa na Nyoni kutatuachia pengo kubwa sana kikosini kwetu tunatakiwa kupata either local versatile player lakini kuziba pengo hilo ni kuwanyang'anya utopolo yule Yannick Bangala by the way ana mkataba wa mwaka mmoja tu.
Kwenye defensive Midfield akiondoka Tadeo Lwanga na kutokana na injury records zake ni heri tuvunje benki tuende TP Mazembe kumchukua Zemanga Soze au tubaki na tulionao.
Kwenye striking force tunahitaji local striker ambaye atakuwa like to like replacement ya Bocco kwangu mimi namuona Lusajo Reliant amekuwa consistent kwa misimu mingi kwa timu kubwa kama Simba tunaweza kunufaika nae wakati huo tukitafuta mbadala wa Kagere na Mugalu though naona bora kubaki na Mugallu ili tusipoteze wote.