Pablo ni kocha mzuri. Tatizo la Tanzania mara nyingi hatuangalii tulipojikwaa ila tunakimbilia kuangalia tulipoangukia. Pablo kaja Simba kakuta Chama na Luis wameuzwa halafu Mugalu, Boko na Kagere viwango vimeporomoka na huku wana majeraha ya mara kwa mara. Kwa maana hiyo Pablo kaja kakutana na changamoto ya nguvu kwenye safu yake ya ushambuliaji. Na hili la kuporomoka viwango kwa washambuliaji wa Simba lilikuwa dhahiri kabla msimu uliopita kwisha lakini viongozi hawakuliona kwa sababu mafowadi walikuwa wanafunga lakini hakuna mtu alikuwa anajiuliza japo wanafunga magoli lakini katika kila mchezo walikuwa wanapoteza nafasi hata zaidi ya kumi. Pia Chama na Luis walikuwa wanawafichia mafowadi wa Simba madhaifu yao kwa muda mrefu kwani walikuwa wanafunga mara kwa mara pale washambuliaji wa Simba wanaposhindwa kufunga.
Viongozi wa Simba wakatae wakubali kuwa walijikwaa pale walipowauza Chama na Luis halafu wakawaleta Sakho, Duncan Nyoni na Peter Banda kuziba nafasi zao halafu wakategemea wapate ubora ule ule. Pesa waliyopata kwa Luis ndio iliwapa tamaa ya kusajili wachezaji vijana ili wapige pesa ndefu huko mbele ya safari wakasahau kuwa kuna swala la matokeo uwanjani na hilo linaamuliwa na wachezaji wenye uzoefu tu na si vinginevyo. Sakho na Banda kuipa Simba makombe kama wachezaji tegemezi sio chini ya misimu miwili ijayo
Nini kifanyike Simba? Ni maamuzi magumu tu yanahitajika bila kuangalia wachezaji usoni. Kwanza kabisa wapige chini safu yote ya ushambuliaji baada tu ya ligi kwisha.
Na kama kweli wana nia ya kufika nusu fainali au fainali kabisa Afria basi wavunje benki waachane na baadhi ya wachezaji na wasajili wengine wapya. Kwangu mimi nafikiri ni wakati wa Simba kusajili wachezaji ambao pamoja na vipaji vyao lakini wawe wapambanaji kweli kweli uwanjani kwa dakika zote tisini na si vinginevyo. Kuna wakati unaangalia Simba inavyocheza mpaka unawaonea huruma kwa kweli kwani kuna watu wanatoka machozi, jasho na damu kwa dakika zote tisini wakina Kapombe, Zimbwe, Onyango na Inonga halafu kuna wengine wanazurura tu uwanjani wanasubiri mechi iishe wakachukue posho zao kama wakina Bwallya japo huyu ana kipaji kikubwa sana lakini si mpambanaji kabisa. Unakuta mchezaji anapoteza mpira kwa adui halafu anatembea matokeo yake anawafanya wenzake wafanye kazi kubwa uwanjani.
Simba kama kweli wana nia ya kufika nusu fainali/ fainali Afrika basi inahitajika isajili kama ifuatavyo:-
1. Iwaache Mugalu na Kagere badala yao isajili mafowadi wawili wa kimataifa. Angalizo lazima wawe na uwezo kuwazidi hao wanaoachwa.
2. Imuhamishie Boko kwenye benchi la ufundi au kumpeleka kufundisha timu ya vijana nafasi yake achukue Lusajo wa Namungo.
3. Itafute viungo wawili wa kimataifa ambao wote wawe na uwezo wa kucheza kiungo cha chini na cha juu bila wasiwasi. Hapa bila kupepesa
iachane na Bwallya. Nasisitiza iachane na Bwally japo ana kipaji kikubwa sana lakini anakosa kabisa "spirit" ya upambanaji uwanjani.
Ukitaka kujua namaanisha nini basi rudi kaangalie "clip" za Lwanga na Fraga ndio utajua maana ya kujitoa kwa ajili ya timu.
4. Iachane na Muzamiru na Nyoni badala yake wamsajili Cleophas Mukandara kuchukua nafasi yake na pia imrudishe Abdulswamad
aliyetolewa kwa mkopo.
5. Iaachane na Wawa na itafute beki mmmoja wa kimataifa ambaye yupo sawa na Inonga au anayemzidi uwezo Inonga.
6. Itafute beki mmoja mmoja awe wa ndani au wa kimataifa ambaye ana uwezo wa kucheza mbavu zote mbili bila wasi wasi ili kuwasaidia
Kapombe na Zimbwe. Mwenda na Gadiel wameshindwa hili jukumu. Gadiel anakaba vizuri sana ila ana uwezo mdogo wa kupandisha
mashambulizi. Mwenda anaweza kupanda ila krosi zake hazina macho na si mkabaji mzuri. Bahati ni kuwa Kapombe na Zimbwe
hawakupata majeraha ya muda mrefu msimu huu maana ingekuwa aibu kwa Simba.
7. Sakho, Mhilu, Mwanuke na Banda waachwe waendelee kuwepo Simba wazidi kukomaa kwani watakuwa na faida Simba ndani ya misimu
miwili ijayo iwapo watakuwa na mwendelezo walio nao sasa hivi.
8. Morison aendelee kubaki Simba. Atumike tu kuamua matokeo kwenye baadhi ya mechi muhimu kwani amethibitsha hilo analiweza.
Adhibitiwe tu kwenye nidhamu basi. Huyu mtu siku akiamua kucheza mpirra anacheza kwa sababu anauweza sana. Ila siku akiamua
kuaharibu anaharibu kweli sijui huwa ana nini kichwani.
Ni mtizamo tu.