Kocha wa Taifa Stars afungishwa virago

Kocha wa Taifa Stars afungishwa virago

Niliwaambia hapana haja ya kuwa na timu hiyo. Kaeni hata miaka 5 mtengeneze timu

Hapo ndo napotaka serikali iwe inaingilia soka,ila ndo hivo sheria za FIFA haziruhusu
 
Walichelewa sana mechi zote hizo tumefungwa . Mimi nashauri hata jina la taifa star libadilishwe iitwe wazee wa 3-0. Mbona jezi wamebadilisha?
 
Mimi huu mpira wa taifa stars nimechoka kabisa kushangilia timu ambayo kazi yake ni kufungwa tu.bora watanzania tubaki kumshangilia ali kiba na diamond tu.
 
Mimi huu mpira wa taifa stars nimechoka kabisa kushangilia timu ambayo kazi yake ni kufungwa tu.bora watanzania tubaki kumshangilia ali kiba na diamond tu.

Acha tuwe tunafungwa ili tuzidi kuona makocha wa kigeni wakiletwa na kufukuzwa;maana ndo kazi tunayoweza
 
Sina hakika kama MWENDAWAZIMU anapona, kama anapona basi anahitaji dawa na dozi yakinifu, pia dozi na dawa anaweza akapata ila tatizo wale waliopewa jukumu la kumpa dawa je wanampa kwa utaratibu elekezi?

Kupona kwa MWENDAWAZIMU yahitaji umakini sana.

Ni kweli kabisa Mwendawazimu hajapona.Tumuombe Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi atengue kauli labda tutasalimika. Maana hii sasa inakera kupita kiasi hasa kwetu sisi wapenda soka. Watatuua kwa presha jamani.Wachezaji wenyewe hata hawajali bado wanafanya makosa yale yale ndani 18.
 
Hivi mnaopiga kelele hapa jukwaani ALIYEWAAMBIA MSHABIKIE TIMU YA TAIFA nani?

unayeshabikia timu ya TAIFA STARS unatafuta vidonda vya tumbo bure.

Lazima tuipende Timu yetu ya Taifa si tumezaliwa Tanzania .Kwa nini nipende timu ya nje.Waswahili husema mdharau kwao mtumwa.Vidonda hatupati na tutaendelea kuwapasha hao wanaojifanya viongozi wa soka la bongo.
 
Kujibizana na vijana unajidhalilisha wewe. Ni bora kuonyesha ukomavu. Matusi mitandaoni haijengi maana inawezekana wanakuita mama ingawa ni baba au ni kijana etc. Punguza jazba ili vijana wajifunze kwetu kuvumiliana

Mkuu huyo alijui kaz kujibizana na vijana sasa acha wamwaibishe
 
Usimchekemwenzio.anafamilia inamtegemea ..kesho yako leo yake...mbeleyake.nyuma yako mpwa..kwenye ajora sitoshabikia.mtu akifukuzwa kumbuka familiangap zinamtegemea bahatimbaya akalemalimao na yeye
Wala huna haja ya kimsikitikia kiasi hicho. Tumezoea tu kudanganyana kwa kutumia vichwa vya habari. Bora hata wangesema anastaafishwa kwa manufaa ya umma. Mtu anayeachishwa kazi analipwa mishara yake yote iliyosalia? Si amepewa fursa ya kupata ajira nyengine mapema zaidi bila ya kupoteza mafao ya ajira anayoachana nayo? Wanahabari wawe wakweli, wasijaribu kutufurahisha eti kwa kocha kufukizwa ilhali pesa yetu inateketea. Tulifanya hivyohivyo kwa Paulsen, wakakaa kimya. Sijui huyu Malinzi ana deal nao hawa ili wagawane hicho kivunja mkataba!
 
Mm sioni ubaya wa huyo kocha athari za timu ya taifa kufanya vibaya ni ndogo sana ukilinganisha na athari za serikali ya za majiji ya Dsm.
Kama kweli tuna uchungu na nchi hii na tunahitaji maendeleo ya kweli tungeanza kumuondoa meya wa Dsm Masaburi tukaendelea kuwaondoa mameya wa Ilala Temeke na kinondoni. Na hata viongozi waajiriwa wa majiji hayo.
Uchafu wa kocha wa timu ya taifa ni mdogo sana kuliko watu hao nilio wataja.
Jiji la Dsm limekuwa kama danguro halieleweki halina mpangilio halina usimamizi wala taratibu nahisi sina kauli nzuri yakulielezea zsidi ya kusema viongozi wa majiji yote ya Dsm ni wabovu na hawako kwa ajili ya watu Dsm.
Laiti pangekuwa na vipindi vya radio na tv na kurasa za magazeti zinazo zungumzia utendaji wa majiji ya Dsm kama za michezo basi wengi wetu wangejua kama mpira sio tatizo kama jiji lilivyo.
Lakini kwakuwa mpira una vipindi ktk radio na tv na unakurasa ktk magazeti ndio tunaona tunavyo boronga.
Shida za uchafu shida za foleni za magari shida za kusimamia sheria za majiji shida za kila aina lakini mameya hawazioni mpaka shida za vituo vya dalala nazo hawazioni.
Mm sioni hata kwa nini tunakuwa na mameya.
unaweza kuwa sahihi, lakini kwa ukurasa huu mbona ni sawa an padri anayehubiri ndani ya bar?
 
Malizni nae aondoke ....ukimuondoa chizi sehemu basi ni lazima uondoe na makopo yake
 
Tatizo sio kocha,Maximo alisema kwamba wachezaji wa Tanzania hawafundishiki.

Hapa issue ni mfumo mzima wa kuendeleza vipaji.Na muhim ni kuanzia mashuleni.
Wachezaji wa Taifa wakiwa kwenye line unaona kabisaa kwamba lishe mbovu,ila check Waganda walivyoonekana wameshiba na fizik yao ipo vizuri sana.

Na pia wachezaji nao sifa nyingiiii,yaani kama mie ningeamua kufanya koching basi ningefanya maamuzi magum,ningechomoa wachezaji woote Daraja la Kwanza nikaweka Taifa.

Maana hawa wachezaji tulionao wanajua kwamba Ligi inaanza August,na Team ya taifa haina maslah kwao.Wakishinda kwao haina faida na wakitolewa wanaona ni bora kwao.Sasa huu mfumo ndio umejengeka.

Na mtakumbuka kuna mchezaji aliwahi kuitwa team ya taifa akasema anaumwa halafu siku ya mechi ya team yake siku kama tatu tu akacheza.

Kocha sio tatizo,hapa Micho Ambae ni kocha wa Uganda tulimtimua kuona hana maana,leo ndio amepewa Team ya Taifa ya Uganda na hiii imedhihirisha kwamba Ubabaishaji unaanzia kwenye Vilabu.Na hatimae alifukuzwa na club hapa na kupewa Taifa Uganda na ametudhihirishia kwamba Hapa mpira hakuna zaidi ni ubabaishaji tu kuanzia Club hadi dhamira za wachezaji.

Bado tupo tupo Kwanza na mpira wetu wa Magazeti
 
Kwanza nasikitika na kuona soka letu likiporomoka kwa mwendo kasi uleule tunaouona kwenye maporomoko ya shilingi yetu. Nadhani TFF ilikuwa na wajibu wa kutuambia Watanzania sababu za kiufundi walizozitumia kumuondoa Paulsen na kumwajiri Mart
Noij.
 
Mmemuonea bure mthungu wawatu hapa hata aje nani tutakua wasindikizaji tu
 
Back
Top Bottom