Kocha wa Yanga: Wachezaji wangu hawana fitness ya kucheza dakika 90

Kocha wa Yanga: Wachezaji wangu hawana fitness ya kucheza dakika 90

Kocha mzuri ni kukubali tu hatukucheza vizuri na ukweli Al Hilal walicheza vizuri kwa malengo kabisa unaona wanataka nini mambo ya fitness ni yenu kambini league iko round sijui ya 8 unaongelea fitness. Mpira wetu unakuzwa kwenye mitandao kuliko uhalisia ilifika wakasema Job na Baca wangekuwa real Madrid wasingeruhusu ma goal mechi na Barca. Kidogo wakaanza kuamini ubingwa wa Africa wanachukuwa. Leo tumejuwa uwezo wetu. Kwenda Afcon ni kwa sababu team 24 siku hizi enzi za 12 hatugusi.
 
Ndio maana nawaambieni Mpira amuujui bali naongea na mashabiki wa Mpira sio wanaoufahamu Mpira kiufundi,,kikawaida timu yoyote Ile inapokosa game time kwa muda mrefu lazima ipate tatizo la kiufundi kwenye Kasi, fitness, na miili kuwa mizito kufanya jambo,, vitu hivi ndivyo vilivyowacost yanga jana kwa kiwango kikubwa,,unaposema tulifungwa na Tabora kwa kucheza mfululizo ilikuwa pia ni sababu kiufundi kwa kuwa unacheza mechi 4 mfululizo ndani ya siku 10 unategemea nini kwa afya ya wachezaji? Kiufundi ni risk maana utazalisha majeraha mengi sana kwa wachezaji!
Simba pia mechi yao na Pamba iliahirishwa lakini wakaomba wacheze, kama hiyo ndiyo sababu mmefungwa basi viongozi wenu hawana akili.
 
Mimi kama shabiki namba moja wa uto nasemaje... fukuza huyu kocha na tulete kitu kipya hivi karibuni
 
Kabisa mkuu,ametuona hatujui mpira.
Wewe muda wote uko na mpira wanzako wamepata shot 2 tu on targets wamefunga zote,wewe shot 5 umekosa zote unazungumzia fitness .wonder shall never end.
Unaeza uka posess mpira kwakuwa mpinzani wako mbinu yake ni kukabia chini lakini swali la kuuliza unashambulia kwa intensity ipi?

Kama kwa low intensity inakuwa kazi bure ,hata kwenye ukabaji unakaba kwa kasi ipi?
 
Wasitafute visingizio,tunataka magoli,na si kumiliki mpira na chenga nyingi
 
Huyu kocha kuanzia aje hajaongeza chochote kwenye kikosi cha Yanga. Ni kama wachezaji walijichezea tu kama walivyoona inafaa.
Unaweza kuongeza kitu kwa mchezaji kwa muda mfupi kama ule? Acheni kufuatilia mipira ya Simba vs yanga fuatilieni na duniani huko?
 

Attachments

  • VID-20241109-WA0006.mp4
    3.6 MB
  • FB_IMG_1732642883392.jpg
    FB_IMG_1732642883392.jpg
    99.6 KB · Views: 4
Yanga imebadilika sana na si kwa uzuri. Si Aziz Ki wana Pacome wote kwishnehi. Timu inabebwa na Maxi tu.

Kutocheza mechi za mashindano pia ni tatizo. Tabia waliyozoea ya kukimbia mechi inawacost. Juzi kina Fernandez, Ahoua na Ngoma walikuwa off kwa kutocheza kwa muda mechi ya mashindano, hawa wenzetu wakabaki wamejifungia wakitegemea maajabu. Nina uhakika wangecheza mechi ya ligi siku 3/4 zilizopita, leo wangekuwa bora zaidi.
 
Back
Top Bottom