Kodi mpya ya Majengo kupitia LUKU inatakiwa kulipwa na Mmiliki wa Jengo na sio Wapangaji wa Jengo

Na kuna nyumba nyngne wananunua umeme mara moja kwa miez miwili mpaka mitatu,,,je hapo itakuaje?
Ile miezi yote ambayo mtu hajanunua, atakutana nayo kwenye ule mwezi atakaonunua. Kwa mfano sasahivi kodi hii imeanza kukatwa mwezi huu wa 8, lakini wanakata hata kodi ya mwezi wa 7. Mtu akinunua sasahivi anakatwa 2,000/=, kama hata huu mwezi wa 8 hatanunua kwa sababu alinunua umeme wa kutosha say mwezi wa 7, akaja kununua mwezi wa 9 huko, atakatwa miezi mitatu, 7, 8 na 9.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu kuna mahali nina ofisi naona wanakata 5000 kila mwezi na sio nyumba ya ghorofa...hii ikoje.
 
Huu ni upigaji kama upigaji mwingine tu, haiwezekan property tax ifyonzeshwe kwenye bili ya umeme,huko vijijini wanaumia zaidi,au rea ilipelekwe Ili hata nyumba za udongo zilipe Kodi kupitia bili? Eti waende Tra, vijijini Kuna matawi ya Tra?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…