Lorenzo Samike
JF-Expert Member
- Jun 18, 2021
- 1,187
- 1,914
Huu uharamia wa kodi mpya za miamala ya simu unapaswa kusimama.
Wanasheria wetu mtusaidie hili. Hakuna kitu kinachoitwa sijui "kodi ya uzalendo" — Lazima Mahakama iweke ZUIO la hizi kodi za kitapeli.
Hauwezi ukakata kodi mara tatu kwenye muamala mmoja. Huo ni uhuni na wizi.
Hizi ndizo kodi za dhulma tulizokuwa tunazisema.
Badala ya kudhibiti madini na bandari pamoja na vitega uchumi vingine vikubwa, mmewaachia wazungu wanajichotea tu, halafu mnatengeneza vijikodi vya ajabu ajabu mnamtwika mwananchi mara tatu tatu?
HAPANA, Double taxation ni uhuni na dhuluma ambayo inapaswa kusimama.
Msituletee mambo ya kuupiga mwingi hapa. Kodi za kitapeli ni mwiko.
Wanasheria fanyeni kazi yenu, na tutaipima mahakama kama bado inajitambua kupitia hili.