Kodi ya majengo kuanza kukatwa kwenye Luku kuanzia Agosti 20, 2021. Je, Serikali imekosa Dira, mbinu zimewaishia?

Kodi ya majengo kuanza kukatwa kwenye Luku kuanzia Agosti 20, 2021. Je, Serikali imekosa Dira, mbinu zimewaishia?

Kodi ya jengo ni elfu 10.

Sasa fikiria una jengo moja lenye vyumba 10 vya wapangaji, ukaamua kila chumba uweke mita yake ili kuepuka usumbufu kwa wapangaji. Na kila mita ikununua umeme inakatwa kodi huoni kama hilo jengo litakuwa linalipa kodi ya sh 100,000 badala ya 10,000?
Tangazo linasema Kodi ya jengo, na sheria imetajwa hapo. Sio Kodi ya umeme. NO! Ni ya JENGO under sheria.

Usijifikirishe tofauti ukataka kupotosha ukweli.
 
Tangazo linasema Kodi ya jengo, na sheria imetajwa hapo. Sio Kodi ya umeme. NO! Ni ya JENGO under sheria.

Usijifikirishe tofauti ukataka kupotosha ukweli.
Kodi ya hilo jengo unailipa vipi wakati unaaambiwa inalipwa kwa kununua Luku?
 
Hiyo nyumba yenye wapangaji kumi ni ya biashara,unastahili kulipa.

Lipa mkuu,Kuna reli ya umeme anatakiwa akamilishe Dar-Morogoro, Morogoro-Dodoma. Alafu aanzishe na akamilishe Dodoma-Singida-Tabora-Shinyanga mpaka Mwanza. Mzigo aloachiwa Ni mkubwa. Na akifeli mtasema! Ameshindwa!

Kuna mradi wa kufua umeme,zahanati na Sasa Barabara vijijini. Hivi mama lazima amalizie kwani ameachiwa mzigo.

Kodi ya jengo ni elfu 10.

Sasa fikiria una jengo moja lenye vyumba 10 vya wapangaji, ukaamua kila chumba uweke mita yake ili kuepuka usumbufu kwa wapangaji. Na kila mita ikununua umeme inakatwa kodi huoni kama hilo jengo litakuwa linalipa kodi ya sh 100,000 badala ya 10,000?
 
Kama Mwanaume nikichangia 12000 Kwa mwaka ili serikali ilete maendelo sioni tatizo ,tuache kulia lia Kama watoto, 12000 ni kitu gani
Hakuna anayekataa wawe wanatoa feedback kila mwezi wamekusanya kiasi gani na mgawanyiko wa fedha zimekwenda wapi na zimetumikaje ... Wakifanya hivyo hata elfu hamsini tutachangia tu ..
 
Hakuna anayekataa wawe wanatoa feedback kila mwezi wamekusanya kiasi gani na mgawanyiko wa fedha zimekwenda wapi na zimetumikaje ... Wakifanya hivyo hata elfu hamsini tutachangia tu ..
Uwafikirie na bibi zako kule kijijini ambao hata 500 ya chumvi wanakosa, hiyo elfu 12 unaona ndogo?
 
Serikali itaanza kukusanya kodi ya majengo kwa kupitia ununuzi wa umeme kuanzia Agosti 20, 2021. Kila mnunuzi atakatwa TZS 1,000 kwa mwezi kwa nyumba ya kawaida na TZS 5,000 kwa mwezi kwa kila sakafu ya ghorofa.

Kwa wanaotumia mita za ankara watalipa katika ankara za mwezi.

IMG_2619.jpg

---
Wakati ulipaji wa kodi ya majengo kupitia manunuzi ya luku ukianza kesho, Ijumaa Agosti 20, 2021 kumekuwa na ongezeko la kodi hiyo kwa viwango tofauti.

Hiyo ikiwa na maana kuwa sasa walio na nyumba za kawaida ndani ya kiwanja kimoja watalipa Sh12, 000 kutoka Sh10, 000 iliyokuwa ikitozwa awali na Sh60, 000 kwa kila sakafu ya ghorofa kutoka Sh50, 000.

Kwa upande wa Halmashauri za Wilaya na Miji Midogo wao pia wataguswa na ongezeko hilo licha ya wao kuwa na ahueni kwani watalipa Sh60, 000 kwa nyumba za ghorofa bila kujali idadi ya sakafu

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Alphayo Kidata leo inaeleza kuwa utekelezaji huo unafanyika chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ukihusisha mita za aina zote za umeme.

“Hili linafanyika kufuatia marekebisho ya Sheria ya Kodi ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa, Sura ya 289 iliyopitishwa na Bunge la Bajeti la mwaka 2021 ambapo viwango vya kodi ya majengo vimebadilishwa,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa njia hii mpya ya ukusanyaji wa kodí, kíla mnunuzi wa umeme atakatwa Sh1,000 kwa mwezi kwa nyumba ya kawaida na Sh5,000 kwa mwezi kwa kila sakafu ya ghorofa.

"Kwa wale wanaotumia mita za Ankara watalipa kodi hii kwa pamoja katika Ankara ya mwezi. Kwa wamiliki ambao majengo yao hayajapata umeme, wataendelea kulipa kodi hiyo kwa kutumia mfumo uliokuwa unatumika hapo awali ambao ni njia ya simu ya mkononi na benki baada ya kupata namba ya kulipia malipo (Control Number) mpaka hapo watakapoingiziwa umeme,"

"Wamiliki wa majengo na wananchi kwa ujumla watakaokatwa kodi hiyo kimakosa na wale watakuwa na malalamiko mbalimbali, watatakiwa kufika katika ofisi za TRA zilizo karibu na maeneo yao kwa ajili ya kushughulikiwa,"

Hapo awali Kodi ya Majengo ilikuwa ikikusanywa na Mamlaka za Serikali za Mitaa ambapo mwaka 2016/17 jukumu hili lilihamishiwa TRA na hadi sasa inaendelea kusimamia jukumu hilo.

Mwananchi
 
Kama Mwanaume nikichangia 12000 Kwa mwaka ili serikali ilete maendelo sioni tatizo ,tuache kulia lia Kama watoto, 12000 ni kitu gani
Ungekuwa unaletewa bure hapo sawa. Lakini hayo unayoita maendeleo licha ya kuletwa kwa Kodi yako 18% VAT, bado unalipa na hizi tozo kubwa... Kisha unalipia tena hizo huduma ulizoletewa.
Sijui km unalijua hili
 
Hii ina maana kuanzia kesho, na itakuwa ni kwa wale wenye majengo tu au hata ukiwa na kiwanja chenye hati unachangia?
 
Back
Top Bottom