Kodi ya majengo kuanza kukatwa kwenye Luku kuanzia Agosti 20, 2021. Je, Serikali imekosa Dira, mbinu zimewaishia?

Kodi ya majengo kuanza kukatwa kwenye Luku kuanzia Agosti 20, 2021. Je, Serikali imekosa Dira, mbinu zimewaishia?

View attachment 1897744

Naomba kuuliza maswali machache...

Ni sababu ipi hasa ya msingi iliyopelekea kutoka mfumo wa malipo wa zamani kuleta mfumo wa sasa?

Kwa hiyo kwanzia agost 20 kodi ya jengo inalipwa na mpangaji?

Vipi kuhusu nyumba ambazo kila chumba kina mita yake?

Vipi kususu mpangaji mmoja ambaye kapanga nyumba mbili?

vipi nikiwa nikiamua miezi miwili ipite sijanunua luku?

CCM imekosa mbinu za kuendesha hii nchi.
CCM hawana maisha
 
Huu ni ubunifu mzuri ambao utaongeza wingo wa ukusanyaji mapato. ufanyiwe marekebisho tu kwenye hayo mapungufu yaliyo jitokeza. Watanzania wengi wanapolipa kodi angalau mzingo wa kodi kwa mfano wafanyakazi utapungua. Panapo stahili kupongeza sisi wengine tutapongeza.
 
Hivi madelu ana akili timamu kweli? Ni wanunuaji umeme wangpi wenye majengo Yao? Seems watunga Sera na wapanga mipango wetu hawajui wa Tanzania wa kawaida tu naishi vp
 
Ndugu, kujibu swali lako, rudi nyuma ile kodi ya motor vehicle inayolipwa kupitia kununua mafuta.
Ile sasa ndio nzuri maana ina mhusu mwenye gari!

Vipi mimi ambae nimepanga nalipa kodi ya kupanga alafu nikinunua luku namlipia mwenye jengo kodi yake ya jengo?
 
Kodi ya jengo ni elfu 10.

Sasa fikiria una jengo moja lenye vyumba 10 vya wapangaji, ukaamua kila chumba uweke mita yake ili kuepuka usumbufu kwa wapangaji. Na kila mita ikununua umeme inakatwa kodi huoni kama hilo jengo litakuwa linalipa kodi ya sh 100,000 badala ya 10,000?
... nakumbuka kuna kipindi hadi mashine za kusaga zililipia road toll! This is similar.
 
Hii inazidi kuongeza maumivu kwa watu was Hali ya chini Mana ktk Hali hii mpangaji hakuzingatiwa kiukweli.
 
Wakifanya huu ubunifu na kwenye kodi ya VAT itakuwa safi sana. Watafute jinsi ya kuchukua VAT inadvance kwenye source yoyote ya kinacho stahiki kulipiwa kodi hii wamuachie huyo muuzaji kuikusanya kodi yake ambayo ameshailipa inadvance. Tuone kwamba atakwepa kuidai hiyo kodi yake.

Achaneni na utaratibu huu wa sasa wa kuwafanya wafanyabiashara kuwa ni mawakala wa kuikusanyia serikali VAT watawaibia tu.

Nitoe mfano. Kwa mfano bia. Serikali yenye utashi haiwezi kushindwa kujua idadi ya chupa zinazozalishwa na kutoka kwenda sokoni kila siku kiwandani. Haiwezi kushindwa kujua wastani wa bei ya rejareja ya chupa moja ya aina flani ya bia. Hivyo serikali inachukua hii VAT yake ya bei rejareja kiwandani. Kiwanda kinaichukua kwa distributor, ditributor anachukuwa kwa wholesaler. Wholessler anaichukua kwa retailer/ bar na mahoteli, chikeni part nk. Na retailer anaichukuwa kwa mlaji wa mwisho wapiga ulabu wa kwenye bar na masherehe. Simple as that.
 
Rudini kwenye umeme mbadala tuachane na TANESCO yenye Luku
 
Ile sasa ndio nzuri maana ina mhusu mwenye gari!

Vipi mimi ambae nimepanga nalipa kodi ya kupanga alafu nikinunua luku namlipia mwenye jengo kodi yake ya jengo?
Ndio linalopigiwa kelele, hilo la mpangaji kulipa kodi ya mwenye nyumba.
Alafu walivyokuwa wapuuzi, eti kesho tu imaanza[emoji1787]
 
Kama Mwanaume nikichangia 12000 Kwa mwaka ili serikali ilete maendelo sioni tatizo ,tuache kulia lia Kama watoto, 12000 ni kitu gani
Tatizo siyo watu kuchangia, tatizo kwenye matumizi ya serikali. Kama nchi tungeshiriki pamoja sisi wananchi na viongozi wetu kufunga mikanda tulete maendeleo ya nchi yetu.

Kinachoshangaza kila mwaka reports za CAG huwa zinaonyesha mapungufu (ubadhilifu) katika matumizi ya pesa za serikali (pesa zetu). Ununuzi wa magari ya kifahari kwa viongozi wetu wa serikali kwa nchi ambayo bado kuna sehemu maji hayajafika, madarasa na madawati hayapo, nk.

Sijui report ya CAG kuhusu harufu ya BOT kati ya January hadi March 2021 iliishia wapi??

Kuna matumizi mabaya ya pesa zetu serikalini, hayo ndiyo yanafanya watu wahoji maswali mengi namna hii.
 
Kodi ya jengo ni elfu 10.

Sasa fikiria una jengo moja lenye vyumba 10 vya wapangaji, ukaamua kila chumba uweke mita yake ili kuepuka usumbufu kwa wapangaji. Na kila mita ikununua umeme inakatwa kodi huoni kama hilo jengo litakuwa linalipa kodi ya sh 100,000 badala ya 10,000?
Kwa nini uweke mita kila chumba wakati kuna sub meters ambazo zenyewe zinasoma kutoka kwenye mita kuu?
 
Bora waanze nilikuwa nasikitika kila siku mbona wanachelewa, kodi ni muhimu jamani
 
View attachment 1897744

Naomba kuuliza maswali machache...

Ni sababu ipi hasa ya msingi iliyopelekea kutoka mfumo wa malipo wa zamani kuleta mfumo wa sasa?

Kwa hiyo kwanzia agost 20 kodi ya jengo inalipwa na mpangaji?

Vipi kuhusu nyumba ambazo kila chumba kina mita yake?

Vipi kususu mpangaji mmoja ambaye kapanga nyumba mbili?

vipi nikiwa nikiamua miezi miwili ipite sijanunua luku?

CCM imekosa mbinu za kuendesha hii nchi.
Nyinyi kila kitu ni kupinga tu!
Halafu ukute hulipagi kodi hata kidogo....unachojua ni kupinga tu!
 
Ungekuwa unaletewa bure hapo sawa. Lakini hayo unayoita maendeleo licha ya kuletwa kwa Kodi yako 18% VAT, bado unalipa na hizi tozo kubwa... Kisha unalipia tena hizo huduma ulizoletewa.
Sijui km unalijua hili
Hawezi kujua,labda amsubirie shemeji yake akitoka kazini amuulize

Sent from my Nokia 2.1 using JamiiForums mobile app
 
Upumbavu tu!

Ndio mtajua kwamba nchi hii Rais wake alifariki toka tarehe 17/03/2021

Hivi inakuwaje?

Yani ile elfu 7 tuliyokuwa tunatozwa kipindi kile kabla ya Magufuli kuiondoa ndio wameirudisha kwa njia hii?

Hivi anaetakiwa kulipa kodi ya jengo ni mpangaji au mwenye jengo?

Unapokata kodi ya jengo kwenye luku maana yake mpangaji ndio atakuwa mlipaji wa kodi ya hilo jengo maana mwenye jengo yeye anachojali ni nyumba yake alishaingiza umeme na anakusanya kodi yake ya pango basi! Habari ya kwamba umenunua luku au laa yeye haimuhusu.

Tuliambiwa mafuta yanapanda sababu kwenye soko la dunia yanepanda,! Haya huko kwenye soko la dunia saa hii mafuta ni dola 64 kwa pipa, vipi wameshusha bei hapa nchini.?
We nawe na huyo dikteta wako jiwe huchoki kupiga porojo.

Kwa wale wanaojua utaratibu wa kuandaa bajeti,wanaelewa kabisa kwamba bajeti hii iliandaliwa wakati wa jiwe. Kwa hiyo,kama angekuwepo,kwa kuwa wewe ulikuwa chawa wake,usingekuja hapa na hizi porojo zako.

Lipeni kodi kwa maendeleo ya nchi. Period.
 
Back
Top Bottom