Kodi ya majengo kuanza kukatwa kwenye Luku kuanzia Agosti 20, 2021. Je, Serikali imekosa Dira, mbinu zimewaishia?

Kodi ya majengo kuanza kukatwa kwenye Luku kuanzia Agosti 20, 2021. Je, Serikali imekosa Dira, mbinu zimewaishia?

Safi sana Kuna watu tuliwaambia upinzani ni muhimu bungeni yakatuponda sana
 
Bora wangerasimisha nyumba zote tz then kila mmiliki apewe hati, kisha hiyo hati iwe inahuishwa kila mwaka kufosi wamiliki kulipa kodi ya jengo
 
We nawe na huyo dikteta wako jiwe huchoki kupiga porojo.

Kwa wale wanaojua utaratibu wa kuandaa bajeti,wanaelewa kabisa kwamba bajeti hii iliandaliwa wakati wa jiwe. Kwa hiyo,kama angekuwepo,kwa kuwa wewe ulikuwa chawa wake,usingekuja hapa na hizi porojo zako.

Lipeni kodi kwa maendeleo ya nchi. Period.
Watu wanaokaa kwa shemeji zao utawajua tu!

Bajeti hii iliandaliwa kipindi cha jiwe? Inaonekana hata kufuatilia mambo hujui
 
Ndio linalopigiwa kelele, hilo la mpangaji kulipa kodi ya mwenye nyumba.
Alafu walivyokuwa wapuuzi, eti kesho tu imaanza[emoji1787]
Umiliki wa jengo uko wa aina mbili wa muda mfupi na muda mrefu

Mpangaji ninmumiliki was jengo kwa muda mfupi yaani kipindi alichopanga .Hivyo Ni sahihi yeye mpangaji kulipa Kodi ya jengo lake kiwe chumba au Nyumba nzima au fremu

Kwa Kodi hii naunga mkono.Ilikuwa inatusumbua wenye Nyumba kutwa uko Halmashauri kupanga foleni.mara kuchukua control number Mara kwenda kulipia ilikuwa usumbufu.

Fikiria mtu una nyumba tano za kupangisha ziko mikoa tofauti Zina wapangaji .Ilikuwa usumbufu

Mpangaji anawajibika kufanya usafi wa jengo na kulilipia Kodi zote Kodi ya mwenye Nyumba na ya jengo ya serikali. Yeye ndie anatumia Hilo jengo

Kwa hili naiunga mkono serikali
 
Serikali itaanza kukusanya kodi ya majengo kwa kupitia ununuzi wa umeme kuanzia Agosti 20, 2021. Kila mnunuzi atakatwa TZS 1,000 kwa mwezi kwa nyumba ya kawaida na TZS 5,000 kwa mwezi kwa kila sakafu ya ghorofa.

Kwa wanaotumia mita za ankara watalipa katika ankara za mwezi.

View attachment 1897774
Hongera serikali hakika mtapata hela nyingi sana
 

Attachments

Mbaya zaidi wameongeza hiyo Kodi kutoka 10k Hadi 12k
Huyu bibi hakuna anachojua
Alisema yeye ni mtaalamu wa kusoma graph za uchumi sio kama mtangulizi wake aliyekuwa anajua kukagua mifuko ya cement iliyojengea barabara🤣🤣🤣🤣
 
Nyinyi kila kitu ni kupinga tu!
Halafu ukute hulipagi kodi hata kidogo....unachojua ni kupinga tu!
Ndugu hakuna mtu halipi Kodi nchi hii. Labda km hanunui bidhaa au huduma. Na huyo mtu hayupo.
Hapa ndipo mnajisahaulisha
 
Alisema yeye ni mtaalamu wa kusoma graph za uchumi sio kama mtangulizi wake aliyekuwa anajua kukagua mifuko ya cement iliyojengea barabara[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Serikali itaanza kukusanya kodi ya majengo kwa kupitia ununuzi wa umeme kuanzia Agosti 20, 2021. Kila mnunuzi atakatwa TZS 1,000 kwa mwezi kwa nyumba ya kawaida na TZS 5,000 kwa mwezi kwa kila sakafu ya ghorofa.

Kwa wanaotumia mita za ankara watalipa katika ankara za mwezi.

View attachment 1897774
Sasa sisi wapangaji tunaolipia luku za wenye nyumba inakuaje...
 
Huu ni ubunifu mzuri ambao utaongeza wingo wa ukusanyaji mapato. ufanyiwe marekebisho tu kwenye hayo mapungufu yaliyo jitokeza. Watanzania wengi wanapolipa kodi angalau mzingo wa kodi kwa mfano wafanyakazi utapungua. Panapo stahili kupongeza sisi wengine tutapongeza.
Bado Kuna vyanzo vingi vya kukusanya Kodi isiyoumiza moja kwa moja...
Kubana matumizi ya viongozi Ni chanzo kimojawapo Cha kuongeza mapato,mf wabunge ,mawaziri, DC, RC,DAS etc wangesema wawe wanakatwa angalau elfu 10 kila mwezi ,serikali ingekusanya kiasi gani?

Viongozi wa siasa ,wanapewa magari,nyumba,posho kedekede,wanadhamana inayowawezesha kupata mikopo kirahisi ,familia zao zinaishi vizuri lakini bado wanataka waongezewe posho..

Kama wao wangeanza kujitoa hata sisi wananchi wa kawaida tungepata moyo na hamasa
 
Jamani na kodi ya maji leteni,use na bwawa,dimbwi,bomba,kisima kirefu,tank juu,itaka sawa sana
 
Wakati ulipaji wa kodi ya majengo kupitia manunuzi ya luku ukianza kesho, Ijumaa Agosti 20, 2021 kumekuwa na ongezeko la kodi hiyo kwa viwango tofauti.

Hiyo ikiwa na maana kuwa sasa walio na nyumba za kawaida ndani ya kiwanja kimoja watalipa Sh12, 000 kutoka Sh10, 000 iliyokuwa ikitozwa awali na Sh60, 000 kwa kila sakafu ya ghorofa kutoka Sh50, 000.

Kwa upande wa Halmashauri za Wilaya na Miji Midogo wao pia wataguswa na ongezeko hilo licha ya wao kuwa na ahueni kwani watalipa Sh60, 000 kwa nyumba za ghorofa bila kujali idadi ya sakafu

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Alphayo Kidata leo inaeleza kuwa utekelezaji huo unafanyika chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ukihusisha mita za aina zote za umeme.

“Hili linafanyika kufuatia marekebisho ya Sheria ya Kodi ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa, Sura ya 289 iliyopitishwa na Bunge la Bajeti la mwaka 2021 ambapo viwango vya kodi ya majengo vimebadilishwa,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa njia hii mpya ya ukusanyaji wa kodí, kíla mnunuzi wa umeme atakatwa Sh1,000 kwa mwezi kwa nyumba ya kawaida na Sh5,000 kwa mwezi kwa kila sakafu ya ghorofa.

"Kwa wale wanaotumia mita za Ankara watalipa kodi hii kwa pamoja katika Ankara ya mwezi. Kwa wamiliki ambao majengo yao hayajapata umeme, wataendelea kulipa kodi hiyo kwa kutumia mfumo uliokuwa unatumika hapo awali ambao ni njia ya simu ya mkononi na benki baada ya kupata namba ya kulipia malipo (Control Number) mpaka hapo watakapoingiziwa umeme,"

"Wamiliki wa majengo na wananchi kwa ujumla watakaokatwa kodi hiyo kimakosa na wale watakuwa na malalamiko mbalimbali, watatakiwa kufika katika ofisi za TRA zilizo karibu na maeneo yao kwa ajili ya kushughulikiwa,"

Hapo awali Kodi ya Majengo ilikuwa ikikusanywa na Mamlaka za Serikali za Mitaa ambapo mwaka 2016/17 jukumu hili lilihamishiwa TRA na hadi sasa inaendelea kusimamia jukumu hilo.


Mwananchi
 
Kama Mwanaume nikichangia 12000 Kwa mwaka ili serikali ilete maendelo sioni tatizo ,tuache kulia lia Kama watoto, 12000 ni kitu gani
Kwa hiyo umeitumia nafsi yako na kuwakilisha wanaume wote ? Kwamba kila mwanaume wa nchi hii 12000 si kitu.
 
Kwa nini uweke mita kila chumba wakati kuna sub meters ambazo zenyewe zinasoma kutoka kwenye mita kuu?
Huku kwetu najilinji hizo mita hazipo,mita hizi za kawaida tu inachukua miezi sita kuunganishiwa hizo submeter si ndo itachukua miaka miwili
 
Back
Top Bottom