Kodi ya majengo kuanza kukatwa kwenye Luku kuanzia Agosti 20, 2021. Je, Serikali imekosa Dira, mbinu zimewaishia?

Kodi ya majengo kuanza kukatwa kwenye Luku kuanzia Agosti 20, 2021. Je, Serikali imekosa Dira, mbinu zimewaishia?

Naomba kujibu

1. Serikali imeondoa mfumo wa zamani sababu ulikuwa rahisi watu kukwepa kulipa na ngumu kukamatwa. Hivyo serikali ilikuwa inapoteza sana mapato.
Umejibu upumbavu sana, hivi unazijua nyumba za kupanga wewe?
 

Naomba kuuliza maswali machache.

Ni sababu ipi hasa ya msingi iliyopelekea kutoka mfumo wa malipo wa zamani kuleta mfumo wa sasa?

Kwa hiyo kwanzia agost 20 kodi ya jengo inalipwa na mpangaji?

Vipi kuhusu nyumba ambazo kila chumba kina mita yake?

Vipi kususu mpangaji mmoja ambaye kapanga nyumba mbili?

vipi nikiwa nikiamua miezi miwili ipite sijanunua luku?

CCM imekosa mbinu za kuendesha hii nchi.
Ungeuliza Mwigulu na viongozi wanaolipiwa umeme wao na serikali watalipiaje maghorofa yao wanayopangisha kwa dola?
 
Wakati ulipaji wa kodi ya majengo kupitia manunuzi ya luku ukianza kesho, Ijumaa Agosti 20, 2021 kumekuwa na ongezeko la kodi hiyo kwa viwango tofauti.

Hiyo ikiwa na maana kuwa sasa walio na nyumba za kawaida ndani ya kiwanja kimoja watalipa Sh12, 000 kutoka Sh10, 000 iliyokuwa ikitozwa awali na Sh60, 000 kwa kila sakafu ya ghorofa kutoka Sh50, 000.

Kwa upande wa Halmashauri za Wilaya na Miji Midogo wao pia wataguswa na ongezeko hilo licha ya wao kuwa na ahueni kwani watalipa Sh60, 000 kwa nyumba za ghorofa bila kujali idadi ya sakafu

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Alphayo Kidata leo inaeleza kuwa utekelezaji huo unafanyika chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ukihusisha mita za aina zote za umeme.

“Hili linafanyika kufuatia marekebisho ya Sheria ya Kodi ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa, Sura ya 289 iliyopitishwa na Bunge la Bajeti la mwaka 2021 ambapo viwango vya kodi ya majengo vimebadilishwa,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa njia hii mpya ya ukusanyaji wa kodí, kíla mnunuzi wa umeme atakatwa Sh1,000 kwa mwezi kwa nyumba ya kawaida na Sh5,000 kwa mwezi kwa kila sakafu ya ghorofa.

"Kwa wale wanaotumia mita za Ankara watalipa kodi hii kwa pamoja katika Ankara ya mwezi. Kwa wamiliki ambao majengo yao hayajapata umeme, wataendelea kulipa kodi hiyo kwa kutumia mfumo uliokuwa unatumika hapo awali ambao ni njia ya simu ya mkononi na benki baada ya kupata namba ya kulipia malipo (Control Number) mpaka hapo watakapoingiziwa umeme,"

"Wamiliki wa majengo na wananchi kwa ujumla watakaokatwa kodi hiyo kimakosa na wale watakuwa na malalamiko mbalimbali, watatakiwa kufika katika ofisi za TRA zilizo karibu na maeneo yao kwa ajili ya kushughulikiwa,"

Hapo awali Kodi ya Majengo ilikuwa ikikusanywa na Mamlaka za Serikali za Mitaa ambapo mwaka 2016/17 jukumu hili lilihamishiwa TRA na hadi sasa inaendelea kusimamia jukumu hilo.


Mwananchi
Ndio inaitwa for more dreams and financial stability
 
Naomba kuuliza maswali machache.
Jibu ni NDIYO! Atalipia kwa kila mita

Na hapa watu tunataka kujiaminisha kuwa ni Kodi ya umeme, hapana. Ni Kodi ya jengo na imewekewa sheria (wameirejea kwenye tangazo) so kusema ni Kodi ya umeme kwa mlango wa jengo ni kupotosha

Kimsingi tatizo linabaki palepale, kwamba serikali hii imekosa watu wabunifu kwenye masuala ya utengenezaji mapato ndio maana wanazidi kumnyonya huyu anayeitwa mnyonge

Ni ajabu tena ya kushangaza kupitisha sheria hii huku ukisahaulisha kuwa kundi kubwa la watu wanaishi kwenye nyumba za kupanga...Sasa mpangaji ndio alipe Kodi ya jengo la mmiliki?

Mjinga anaweza kujibu "Jenga Yako"! Atakuwa amejibu, lkn ni jibu la kijinga

Ila napenda tu vile tunakamuliwa sote, yani ule utamu wa kuisoma namba upo kotekote


Ni sababu ipi hasa ya msingi iliyopelekea kutoka mfumo wa malipo wa zamani kuleta mfumo wa sasa?

Kwa hiyo kwanzia agost 20 kodi ya jengo inalipwa na mpangaji?

Vipi kuhusu nyumba ambazo kila chumba kina mita yake?

Vipi kususu mpangaji mmoja ambaye kapanga nyumba mbili?

vipi nikiwa nikiamua miezi miwili ipite sijanunua luku?

CCM imekosa mbinu za kuendesha hii nchi.
Daah ifike mahali watuhurumie mbona hivi lakini
 
Ukinunua Umeme sasa hivi unalipa Kodi nne:

1. VAT asilimia 18

2. Ewura Asimilia 3

3. REA asilima 1

4. Kodi ya Jengo (Tsh 1000- Tsh 5000)
 
nadhani wanataka kufanya mabadiliko katika kodi za jengo kwa kuongeza malipo ya umeme hii inawezekanaje? inamaanisha bili itakuwa kubwa kufidia kodi ya jengo?
... inashangaza hao TRA wanarudi mbio mbio wakati walishajitoa kwenye masuala ya kodi za majengo na kuwaachia halmashauri kwa kisingizo "ukusanyaji wake ni gharama kuliko kiasi kinachopatikana". Baada ya kutozwa kupitia bili za umeme wamerudi mbio kwa sababu watazichota kirahisi kutoka Tanesco (kwa "kushirikiana na Tanesco"); sina hakika kama WATAVUKA MALENGO kama enzi zile. Hii inaonesha ubunifu nchi hii ni SIFURI.
 
bro kila mita inanamba ya jengo ko aiwezi kuwa tabu
Kodi ya jengo ni elfu 10.

Sasa fikiria una jengo moja lenye vyumba 10 vya wapangaji, ukaamua kila chumba uweke mita yake ili kuepuka usumbufu kwa wapangaji. Na kila mita ikununua umeme inakatwa kodi huoni kama hilo jengo litakuwa linalipa kodi ya sh 100,000 badala ya 10,000?
 
Serikali inapiga ndege wawili kwa jiwe moja. Kwanza, kupunguza kusukumana na watu katika kulipa kodi ya majengo. Pia ukusanyaji wake hautakuwa na gharama kubwa. Asante tekinolojia ya mawasiliano.

Pili, kupanua wigo wa walipa kodi kwa vile kila mwenye luku lazima atalipa hiyo kodi. Zimekuwepo hoja kwamba hapa bongo watu wachache wanatwishwa mzigo wa kulipa kodi. Serikali nimejaribu kupata ufumbuzi wa hoja hiyo. Kama kodi ni kubwa (kama inavyosemekana kwenye miamala) au ni ndogo hilo ni suala lingine na linazungumzika.

Kimsingi, serikali (iwe ya CCM, Chadema, act-wazalendo, chauma n.k.) haiwezi kuchochos maendeleo bila kukusanya kodi. Vyanzo gani vya kodi, Wabunge wetu wanatuwakilisha katika kufikia maamuzi hayo (wamepatikanaje hiyo ni hoja tofauti ambayo haihusiani na vyanzo na viwango vya kodi).

Kuhusu mpangaji kulipishwa kodi badala la mwenye nyumba ni suala la maelewano kati ya hao wawili. Kiwango cha kodi kinaeleweka. Hivyo mwenye nyumba anawajibika kumrejeshea mpangaji wake kwa utaratibu watakaokubaliana. Hili siyo jukumu la serikali.
Umesomeka
 
Serikali yenyewe inatudharau wananchi kwa sababu hatuwezi kupinga chochote wale Wezi wa bungeni watakachoamua.
"Nyie viongozi wekeni Kodi mnazojisikia maana mnaongoza kondoo"
 
Sio sifa Mkuu,kodi ya 12000 kwa mwaka Kwa raia anayejitambua ni kitu gani?Tulipe Kodi ili tupate haki ya kulalamika tunapoona hakuna maendelo
Basi warudishe na Kodi ya kichwa kwani sh 4000 kwa mwaka Ni kitu gani kwa raia anayejitambua.
 
Naomba kujibu

1. Serikali imeondoa mfumo wa zamani sababu ulikuwa rahisi watu kukwepa kulipa na ngumu kukamatwa. Hivyo serikali ilikuwa inapoteza sana mapato. Mfumo mpya ni ngumu kukwepa.

2. Mpangaji halipi Kodi ya nyumba. Hapo ni makubaliano na mwenye nyumba akisema utalupa mwenyewe hama nyumba usikae kulalamika kitu kipo ndani ya uwezo wako

3. Kila chumba kuwa na Mita hayo ni maamuzi binafsi ya mwenye nyumba anaweza kuondoa au akaacha au akanunua sub meters ambazo bill yake haitoki direct TANESCO bali inatokana na mgao unaotoka kwenye main meter.

4. Mpangaji aliyepanga nyumba mbili hapo narudi kwenye jibu langu la pili kuwa mpangaji atabaki kulipa kodi ya pango akilipa kodi ya TRA ni makubaliano yake na mwenye nyumba.

5. Unauliza usiponunua Umeme. Hapo weka vizuri swali lako maana usiponunua Umeme si unalala giza? Au unamaanisha unanunua Umeme labda wa 200k wanakukata 1,000 yao alafu unautumia huo mwaka Mzima? Kama ndivyo utakuwa umewakomoa.
Ujinga mtupu ulioujibu hapa,!
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Namba ya jengo?

Unachekesha wewe!
 
Back
Top Bottom