Kodi ya majengo kuanza kukatwa kwenye Luku kuanzia Agosti 20, 2021. Je, Serikali imekosa Dira, mbinu zimewaishia?

Kodi ya majengo kuanza kukatwa kwenye Luku kuanzia Agosti 20, 2021. Je, Serikali imekosa Dira, mbinu zimewaishia?

Sio sifa Mkuu,kodi ya 12000 kwa mwaka Kwa raia anayejitambua ni kitu gani?Tulipe Kodi ili tupate haki ya kulalamika tunapoona hakuna maendelo
Lini tulikuwa hatulipi kodi? Kodi tunalipa miaka nenda miaka rudi, hawatupi mpango wa kuzuia ufisadi, wanatujazia makodi tu ambayo hatujui kama pesa zitafika kwenye miradi lengwa ama lah!
 
Naomba kuuliza maswali machache.

Ni sababu ipi hasa ya msingi iliyopelekea kutoka mfumo wa malipo wa zamani kuleta mfumo wa sasa?

Kwa hiyo kwanzia agost 20 kodi ya jengo inalipwa na mpangaji?

Vipi kuhusu nyumba ambazo kila chumba kina mita yake?

Vipi kususu mpangaji mmoja ambaye kapanga nyumba mbili?

Vipi nikiwa nikiamua miezi miwili ipite sijanunua luku?

CCM imekosa mbinu za kuendesha hii nchi.
Hapo kuna kikundi cha wahuni wanaendesha nchi kihuni. Hivi mtu mwenye akili timamu unampaje gaidi mwigulu asimamie uchumi wa nchi?
 
Kama Mwanaume nikichangia 12000 Kwa mwaka ili serikali ilete maendelo sioni tatizo ,tuache kulia lia Kama watoto, 12000 ni kitu gani
Nisaidie 5000 tu boss. Sisi masikini sh mia ikipotea tu lazima tulalamike sanaaa, sasa elf kumi alafu uongeze na mbili useme ni kitu gan!!!! Anyway money talks [emoji817]
 
Najiuliza taasisi zisizolipaga bill zozote, huenda ndiyo serikali imetumia na hizo taasisi katika takwimu imefikiria ina wateja wengi, au mie sijui kufikiria??

Everyday is Saturday................................😎
 
Hapa kama nawaona wale wanyonge wa awamu tano wanavyomkumbuka Mzee baba,Badala ya kuwa na amani na mama aliyetuachia sasa watoto wanamkumbuka baba
 
Hii kodi ya wizi waliiweka wakijua fika wapangaji ni wengi zaidi ya wenye nyumba.
 
Kama Mwanaume nikichangia 12000 Kwa mwaka ili serikali ilete maendelo sioni tatizo ,tuache kulia lia Kama watoto, 12000 ni kitu gani
Issue sio hela, we ndio huna akili, ama labda na ni mnufaika. Issue ni matumizi ya izo fedha. Tembea inchi nyingi utakuja kuona Tanzania ndio inchi kama sio 10 bora basi ni ya kwanza inayotumia fedha za umma ama za walipa kodi vibaya kupita mfano
 
Hapa kama nawaona wale wanyonge wa awamu tano wanavyomkumbuka Mzee baba,Badala ya kuwa na amani na mama aliyetuachia sasa watoto wanamkumbuka baba..........halafu jamani katika ili swala la kodi ya jengo wazee wamesamehewa katika ili ama ndio panga la watu wote
 
Naomba kuuliza maswali machache.

Ni sababu ipi hasa ya msingi iliyopelekea kutoka mfumo wa malipo wa zamani kuleta mfumo wa sasa?

Kwa hiyo kwanzia agost 20 kodi ya jengo inalipwa na mpangaji?

Vipi kuhusu nyumba ambazo kila chumba kina mita yake?

Vipi kususu mpangaji mmoja ambaye kapanga nyumba mbili?

Vipi nikiwa nikiamua miezi miwili ipite sijanunua luku?

CCM imekosa mbinu za kuendesha hii nchi.
Ujinga huu utasababisha watu wengi wachezee mita za luku
 
Naunga mkono, ni kiwango kidogo sana na itasaidia serikali sana kukusanya kodi ya majengo, maana kodi hii ya majengo tulipiga kelele sana serikali itafute namna watu tulipe iwe chanzo kipya cha mapato. Asante sana serikali kwa ku implement hii kodi, maana kodi ya majengo ni lazima dunia nzima. Sasa limepata ufumbuzi. Tulipeni ni kwa faida yetu, na serikali itaongeza mapato.
 
Mimi swali langu linakuja ni baada ya hayo malipo kwa kutumia Tanesco je, risiti za malipo ya majengo tutazipata vipi?
Umuhimu wa kununua luku kwa wakala, tunza receipt weka file maalum la receipt za luku
 
Kama Mwanaume nikichangia 12000 Kwa mwaka ili serikali ilete maendelo sioni tatizo ,tuache kulia lia Kama watoto, 12000 ni kitu gani
Tatizo linaanzia pale pesa yako inapotafunwa bila habari na walafi wachache kutoka serikaliNI😔😔INAKERAAAAA
 
Fungua kesi udai refund bosi.

Nyumba zisizo na umeme umeambiwa wataendelea na utaratibu wa zamani.

Wengine tuassume tu ni kama kodi ya uzalendo.

Haya maujenzi ili yaishe lazima tukamuliwe wote, hatutaki tena kukopa kwa mabeberu na kudaiwa riba...sasa tukamuane tu wote za matajiri zimeisha na wengine wamefirisika.
Miradi isiyokuwa na tija kama kuhamia Dodoma ndiyo inatubebesha mizigo isiyokuwa na mantiki kama hii
 
Back
Top Bottom