Nuzo Namia Bubelang
Member
- Aug 2, 2024
- 26
- 54
Ukikokotoa kwa namna hiyo, VAT inayolipwa na agent katika kila hatua itatofautiana na na jumla aliyolipa mlaji.Yaani:
1: Mzalishaji: VAT 18%
2: Muuzaji jumla: VAT1*18% + VAT18%
3: Rejareja VAT1×18%+VAT2×18%+VAT3
Maana halisi ya ulichoandika ni kuwa Vat sio kodi sahihi kwa nchi masikimi. Ugumu wote unaopatikana kariakoo kwa watu kutokutoa risiti ni kwa sababu mlengwa wa vat final conuDokta vat ililenga kulipwa na mlaji wa mwisho, sio mzalishaji.
Ndo mana kuna ritani zinafanyika kila mwezi kuanzia kwa prodyuza wa bidhaa, wholesaler, retailers wote wanarudishiwa pesa yao waliyoongeza kwenye thamani ya bidhaa. Ili final consumer ndio target yaani yampasa alipe.
Sasa akichajiwa producer wa bidhaa, naona atabebeshwa mzigo mkubwa na pengine hiyo bidhaa ikawa na bei kubwa zaidi.
Umeielezea vizuri sana vat.Mfano;
Hatua ya kwanza; Mzalishaji anauza mfuko wa saruji 10,000 ataongeza VAT (18%)
10,000 + 18% = 11,800
Atamuuzia muuzaji wa jumla kwa shilingi 11,800. Baada ya mauzo atawasilisha TRA 1,800 kama VAT aliyokusanya.
Hatua ya pili; Muuzaji wa jumla, baada ya kujumlisha gharama zake zote, amepanga kuuza kwa shilingi 15,000. Katika bei hiyo atajumlisha 18% ya VAT.
15,000 + 18% = 17,700.
Muuzaji wa jumla atauza mfuko huo kwa shilingi 17,700 kwa muuzaji wa reja reja, na kuwaslilisha TRA kiasi cha shilingi 900 kama VAT.
Hatua ya tatu; Muuzaji wa reja reja baada ya kununua, amepanga kuuza mfuko kwa 20,000. Katika bei yake hiyo ataongeza 18% ya VAT.
20,000 + 18% = 23,600.
Atauza kwa mtumiaji wa mwisho kwa shilingi 23,600 na kiwasilisha TRA 900 kama VAT.
VAT Inayolipwa = VAT muuzaji anayotoza katika mauzo - VAT anayolipa katika manunuzi.
Katika hatua ya kwanza; VAT katika mauzo kwa mzalshaji- VAT katika manunuzi.
Ametoza 1,800 katika mauzo, hakuna alicholipa katika manunuzi. Atawasilisha 1,800.
Katika hatua ya pili; VAT katika mauzo kwa muuzaji reja reja - VAT katika manunuzi toka kwa mzalishaji.
2700 - 1800 = 900
Baada ya ku-recover VAT aliyolipa katika manunuzi, muuzaji wa jumla anawasilisha kiasi kilichozidi toka katika VAT aliyotoza, anawasilisha 900 kama VAT.
Katika hatua ya tatu; VAT aliyotoza muuzaji wa rejareja - VAT aliyolipa katika manunuzi toka kwa muuzaji wa jumla.
3,600 - 2,700 = 900
Muuzaji wa reja reja anawasilisha 900 iliyozidi toka katika kiasi alichochaji katika mauzo kama VAT baada ya ku-recover gharama za VAT aliyolipa katika manunuzi.
VAT ilivyolipwa katika mnyororo wa thamani.
Mzalishaji amelipa 1,800 + Muuzaji wa jumla amelipa 900 + Muuzaji wa reja reja amelipa 900 = 3,600
Katika mnyororo mlaji wa mwisho amelipa 3,600 kama Vat ( 20,000*18%). Ni kodi ya mlaji katika dhana ya kuwa, mlaji hayuko katika nafasi ya ku-recover kiasi alicholipa kama agents wengine katika mnyororo wa thamani.
Agents wengine ni wakusanyaji tu wa kodi hii, huwasilisha kilichozidi baada ya kufidia kile walicholipa kama VAT wakati wa manunuzi. Agent hurudishiwa (Refunded) ikiwa tu itathibitika alichotoza katika mauzo kama Vat ni kidogo kuliko alicholipa katika mauzo, tofauti iliyopo atafidiwa.
Nadharia ya VAT kwa ufupi.
Ndivyo inavyo takiwa iwe lkn tra hawapigi hivyo mahesabu yao, hao tra wanapiga from total salesMfano;

Kwa nini unakwepa kuwekaUkiangalia kwa jicho la ndani zaidi, inazidi kwani. 18% ya mwanzo inaenda kujumuishwa kwenye 18% ya pili pia hizi zote zinaenda kujumuishwa kwenye hesabu ya mwisho kama multiple ya kila moja, ukiacha jumla yake kuu.
Yaani:
1: Mzalishaji: VAT 18%
2: Muuzaji jumla: VAT1*18% + VAT18%
3: Rejareja VAT1×18%+VAT2×18%+VAT3
Suluhisho: A
1: Mzalishaji: VAT 18% ya uzalishaji na faida yake.
2: Muuzaji jumla: VAT Gharama zilizoongezeka kutoka 1 hapo juu na faida yake × 18%
3: Gharama zilizoongezeka kutoka2 na faida yake ×18%
AU
SuluhishoB
Kila bei kwenye stage zote tatu itozwe kila moja itozwe 6%, 6%×3 stages=18%
Athari itapungua japo bado uhalisia upo mbali.
Hata mfanyabiashara naye ni final mlajiDokta vat ililenga kulipwa na mlaji wa mwisho, sio mzalishaji.
Ndo mana kuna ritani zinafanyika kila mwezi kuanzia kwa prodyuza wa bidhaa, wholesaler, retailers wote wanarudishiwa pesa yao waliyoongeza kwenye thamani ya bidhaa. Ili final consumer ndio target yaani yampasa alipe.
Sasa akichajiwa producer wa bidhaa, naona atabebeshwa mzigo mkubwa na pengine hiyo bidhaa ikawa na bei kubwa zaidi.
Tuko nae kwenye boti moja. Shida ni anaepokea VAT je anapokea 18% tu toka kwa mlaji?Hata mfanyabiashara naye ni final mlaji
Yap, nilisahau hii. Ndo uzuri wa majadiliano.Kwa nini unakwepa kuweka
Suluhisho C:
Itozwe mwenye stage ya kwanza tu kwa kiwango cha 18%? Mbona hii ndiyo best kwani itaiepusha serikali kukimbizana na hao wafanya biashara wa ngazi ya pili na ya tatu. Serikali inakuwa imechukua chake mapema.
Weee tangu lini mfanya biashara akawa mlaji? By definition mfanya biashara ni mtafutaji faida to the maximum. Ukizubaa hata hiyo VAT anaichukua kama faida yake kwa mbinu zo zote zile hata kama ni kuwahonga kiasi fulani hao maafisa wa TRA watakaoenda kuidai, kutoa risiti fake na kadhalika.Hata mfanyabiashara naye ni final mlaji
Suluhisho B haliwezi kuwa sahihi maana kuna baafhi ya bidhaa zinapita kwa suppliers zaidi ya 10, kabla ya kumfikia mlaji, utaigawa vipi hii Vat.Ukiangalia kwa jicho la ndani zaidi, inazidi kwani. 18% ya mwanzo inaenda kujumuishwa kwenye 18% ya pili pia hizi zote zinaenda kujumuishwa kwenye hesabu ya mwisho kama multiple ya kila moja, ukiacha jumla yake kuu.
Yaani:
1: Mzalishaji: VAT 18%
2: Muuzaji jumla: VAT1*18% + VAT18%
3: Rejareja VAT1×18%+VAT2×18%+VAT3
Suluhisho: A
1: Mzalishaji: VAT 18% ya uzalishaji na faida yake.
2: Muuzaji jumla: VAT Gharama zilizoongezeka kutoka 1 hapo juu na faida yake × 18%
3: Gharama zilizoongezeka kutoka2 na faida yake ×18%
AU
SuluhishoB
Kila bei kwenye stage zote tatu itozwe kila moja itozwe 6%, 6%×3 stages=18%
Athari itapungua japo bado uhalisia upo mbali.
Ukitoza Vat kwenye stage ya kwanza tayari unakuo umeondoa dhana nzimaa ya Vat.Kwa nini unakwepa kuweka
Suluhisho C:
Itozwe mwenye stage ya kwanza tu kwa kiwango cha 18%? Mbona hii ndiyo best kwani itaiepusha serikali kukimbizana na hao wafanya biashara wa ngazi ya pili na ya tatu. Serikali inakuwa imechukua chake mapema.
Mfanya biashara hawezI kuwa mlaji, yeye ni mtengeneza faida tu, na tayari kwemye mifumo ya kodi kuna kodi kadhaa analipa ikiwemo mapato,Hata mfanyabiashara naye ni final mlaji
Wafanyabiashara tulipe kodi kama wanavyolipa watumishi. Yaani endapo Serikali ingesema ikomae wafanyabiashara walipe kodi kama inavyotakiwa nadhani zaidi ya 50% wangefunga biashara. VAT ipo kila nchi. HAIKWEPEK
kusiTatizo ni ugumu na gharama kubwa wa kumpata na kumfuatilia huyo muuzaji wa mwisho aka wa reja reja. Hawa ni wengi. Ni wengi sana na wako kwenye kila kichochoro cha nchi yetu hii kubwa.
Wazalishaji ni wachache. Wanajulikana sehemu waliko. TRA ni rahisi kuwafikia, wakaona kilichozalishwa na kukiwekea lable ya TRA. Watajua kiasi kilichouzwa na vat yake kwa usahihi bila udanganyifu wo wote. Vivyo hivyo kwa bidhaa zinazoingia kwenye mipaka yetu rasmu kutoka nje.
Ifananishe VAT na chumvi ya iodine inayozuia uvimbe wa tezi ya shingo (goiter). Ni rahisi sana kuifikisha chumvi hii kwa kila mwananchi kama utaiweka kwenye vyanzo vyao vya maji ya kunywa ie kwenye uzalishaji. Utapata taabu sana kuifikisha kwa kila mwananchi kama utatumia njia ya kumfikia kila mwananchi nyumbani kwake na kumwekea chumvi hiyo kwenye mtungi wake wa maji ya kunywa ie retailers. Kwanza utakuwa una mkera na unaweza kusambabisha ugomvi na yeye. Hivyo njia rahisi ni hiyo kwenye chanzo bila hata yeye kujua kwamba kawekewa chumvi ya vat! Atainywa tu. Hata huyo retailer na wholesaler wala hatajua kabeba na chumvi ya vat kwenye bidhaa anazouza. Very simple lakini TRA njia hiyo hawaitaki kwani itawanyima masilahi yao binafsi. Inabidi Mama asimame kidete.
Viwanda na wazalishaji wana corporate Tax ambayo ni 30% ya mapato ghafi, hii kodi inalipwa kila wanapopata faida.Lazima tujue hizo Kodi za Viwanda kwanza ndio tujadili mantiki ya VAT hapo kiwandani maana Serikali isingeiweka hapo Kwa mzalishaji kama ana Kodi zake zingine ,ingeweza kuweka tuu Kwa wholeseller na Retailers.
Producer halipi Vat, yeye ni mkusanyaji tu wa kodi hiyo. Kuna wakati procucer huyu anafanya manunuzi pia, hapo sasa scenario inabadilika yeye anakuwa mlaji.Unadhani Kwa nini Serikali iweke VAT Kwa producer ambae mwisho wa siku atakuja kurudishiwa Kwa njia ya returns? What is the logic behind?
Asante sana kwa huu uchambuzi, nchi hii wananchi wanabebeshwa mzigo mzito na kinachopatikana kinaishia mifukoni mwa wachache.Ukweli ni kwamba kila mtanzania kuanzia akiwa tumboni mwa mama yake analipa kodi ya serikali bila yeye kujua kodi hiyo iko kwenye mfumo wa indirect taxation.
Mfumo huu ni very friendly na hakuna mtu wa kuukwepa hata kama ni mtoto mchanga. Kodi hii iko kwenye kila bidhaa au huduma anayonunua. Mama mjamzito hugawana chakula na mtoto wake aliye tumboni ambacho kalipia kodi.
Tatizo letu ni huu mfumo wa VAT wa kukusanya hiyo indirect taxes za bidhaa na huduma ambazo kila mtanzania hununua. Yaani mfumo uko complex uliojaa ujanja mwingi unaotoa mianya mingi kwa pesa hizo nyingi kuishia kwenye matumbo ya wajanja.
Mfumo wenyewe uko hivi: Chukua mfano kiwanda kinachozalisha bidhaa fulani hususani sementi. Baada ya uzalishaji kiwanda kinapanga kuuza hiyo sementi TZS 10,000 kila mfuko kikiwa kimezingatia gharama na faida ya uzalishaji huo na ushindani wa soko uliopo. Serikali haingilii bei hiyo ya mwenye kiwanda (which is very good).
Badala yake inamwambia serikali inamwambia huyo mwenye kiwanda aongeze TZS 2,000 kwenye kila mfuko ambayo itakuwa ni kodi ya serikali atakapoiuza (sales tax). Hadi hatua hiyo bado ni very good.
Tatizo na ujanja unaanzia baada ya hatua hiyo. Serikali inamwambia huyo mwenye kiwanda kwamba hiyo TZS 2,000 kwa kila mfuko serikali itamrudishia mwenye kiwanda baada ya serikali (TRA) kupata (VAT) tax returns kutoka muuzaji wa mwisho wa rejareja (retail) aka mmachinga huko Sumbawanga.
Mwenye kiwanda huuza bidhaa zake kwa wholesalers. Hivyo mfuko mmoja wa sementi mwenye kiwanda atamuuzia wholesaler kwa TZS 12,000. Huyu wholesaler naye atapanga bei atakayoiuza hiyo sementi huko Sumbawanga akizingatia gharama ya usafirishaji, faida yake na ushindani wa soko. Bei yake inaweza ikawa TZS 15,000 kwa kila mfuko. TRA itamwambia aongeze TZS 2,000 kama kodi ya serikali (VAT) ambayo atarudishiwa baada huyo atakayemuuzia (retailer) kurejesha tax returns. Hivyo wholesaler atamuuzia retailer mfuko mmoja wa sementi kwa TZS 17,000.
Huyo retailer naye atapanga faida yake na kuona aiuze kwa TZS 20,000. Naye TRA itamwambia aongeze TZS 2,000 kwenye bei hiyo kama VAT na atoe risiti na tax returns. Hivyo bei ya mfuko mmoja wa sementi anaiuza kwa mlaji kwa TZS 22,000.
Katika mfumo huo wa VAT huyo retailer anatakiwa kuandaa na kuwakilisha VAT returns za bidhaa aina zote alizouza kila mwezi ili kuwezesha hao wholesalers na wenye viwanda (source) warejeshewe hizo TZs 2,000 zao. Yeye harudishiwi cho chote.
Mlaji wa mwisho anakuwa ameongezewa TZS 2,000 mara tatu kwenye hiyo thamani ya bidhaa lakini serikali sana sana inaambulia TZS 2,000 tu! Hapo utaona kuna myanya ya wenye viwanda na wholesalers kurejeshewa hizo TZS 2,000 kwa maelewano tu na maafisa wa TRA.
Hapo utaona mapambano ya maafisa wa TRA na retailers kuhusu risiti na tax returns ambao huishia mara nyingi kwa retailers kutoa rushwa kwa maafisa hawa.
Hivyo ndivyo ulivyo mfumo huu wa VAT kwa bidhaa zingine zinazotoka nje ya nchi na ndani ya nchi. Inashangaza zaidi kuwa hata bidhaa zinazozalishwa na taasisi zinazomilikiwa kwa asilimia 100% na serikali nazo zinawekewa kodi ya serikali, yaani serikali inajitoza kodi?
Shirika kama la TANESCO miradi yake imejengwa kwa pesa yetu (kodi zetu). Hata kama baadhi ya pesa iliyotumika tulikopa nje bado kodi zetu zitalipa hilo deni letu. Ni shirika letu, sasa linawezaje kututoza kodi? Sisi ndiyo wenye mamlaka ya kupanga umeme tulipe kwa bei gani ili kuwezesha kulipa mishahara na other charges (OC) za shirika letu zilizopitishwa na bunge letu la bajeti. Ziada ikipatikana inaweza kugharimia mambo mengine hususani madawa na vifaa tiba.
Hitimisho: VAT is nothing but a sales tax. Itozwe mara moja tu kwenye chanzo ya hiyo bidhaa. Kama bidhaa inazalishwa hapa nchini basi huyo mwenye kiwanda pekee ndiye atozwe/ akusanye hiyo kodi na kuiwakilisha serikalini baada ya kuuza bidhaa hiyo.
Hao wholesalers na retail sellers na machinga haiwahusu maana serikali itakuwa ilishachukua kilicho stahili yake. Kama bidhaa inatoka nje ya nchi, serikali ichukue kodi yake pale pale mipakani inapoingilia.
Kwenye zingine kama zile za kilimo na mifugo kodi hii ilipwe kwenye minada mikubwa kutoka kwa wafanya biashara wakubwa wanaonunua bidhaa hizo. Mambo ya kurudishana kodi yawe mwisho.
Kazi ya watumishi wa TRA iwe kwenye maeneo haya tu na kushirikiana na polisi kunasa bidhaa zinazoingia kwa magendo kupitia panya routes. Serikali ni moja. Mambo ya kodi za serikali za mitaa na kodi za serikali kuu (TRA) hayana maana kwa mwananchi.
Zote kwake ni za serikali, wao watajua wanagawana vipi. Mambo ya direct taxations tuachane nayo au yapunguzwe kabisa. Yana maudhi sana na kuwafanya wananchi waichukie serikali yao. Imagine kama kodi ya kichwa ikarejeshwa hata kama ni buku moja tu kwa kila kichwa kwa mwaka, unadhani itakuwaje?
Hata nchi za ulaya wanafanya hivi.Wataalamu wa kodi wafuatilie mfumo wa kodi wa nchi ya Canada ambao kinacho rudishwa kwa jamii kinaoneka dhahiri na hurudishwa pia kwa mlipa kodi ,(as an individual), yaani kwako mwenyewe mlipa kodi, mfano endapo mlipa kodi atasimamishwa kazi ama akipata changamoto ,mfumo umtambue huwezesha kumlipia kodi ya nyumba na posho ya chakula kwakifupi uwe ni mfumo ambao kila mmja apate faida nao usipo utumia inakula kwako
Hawa wataalamu wetu tena wanaoitwa wabobezi wamebobea kwenye nini, labda wamebobea kwenye mifumo ambayo inawanufaisha wao, kwakifupi mfumo wetu wa kodi hauko wazi, (not even competitive)Hata nchi za ulaya wanafanya hivi.