Kodi ya VAT ifumuliwe. It's a complex sales tax iliyojaa ujanja mwingi na upigaji. Itozwe kwenye source pekee as a sales tax na kusiwe na tax returns

Kodi ya VAT ifumuliwe. It's a complex sales tax iliyojaa ujanja mwingi na upigaji. Itozwe kwenye source pekee as a sales tax na kusiwe na tax returns

Yaani:
1: Mzalishaji: VAT 18%
2: Muuzaji jumla: VAT1*18% + VAT18%
3: Rejareja VAT1×18%+VAT2×18%+VAT3
Ukikokotoa kwa namna hiyo, VAT inayolipwa na agent katika kila hatua itatofautiana na na jumla aliyolipa mlaji.

Calculation sahihi,.
1. Mzalishaji : Ametoza vat 18% amelipa 0
2. Muuzaji jumla: ametoza 18% vat - aliyolipa katika manunuzi 18% toka kwa mzalishaji.
3. Rejareja: ametoza vat 18% katika mauzo kwa mlaji - amelipa vat 18% katika manunuzi toka kwa muuzaji jumla.
Mizani inabalance.
 
Dokta vat ililenga kulipwa na mlaji wa mwisho, sio mzalishaji.
Ndo mana kuna ritani zinafanyika kila mwezi kuanzia kwa prodyuza wa bidhaa, wholesaler, retailers wote wanarudishiwa pesa yao waliyoongeza kwenye thamani ya bidhaa. Ili final consumer ndio target yaani yampasa alipe.
Sasa akichajiwa producer wa bidhaa, naona atabebeshwa mzigo mkubwa na pengine hiyo bidhaa ikawa na bei kubwa zaidi.
Maana halisi ya ulichoandika ni kuwa Vat sio kodi sahihi kwa nchi masikimi. Ugumu wote unaopatikana kariakoo kwa watu kutokutoa risiti ni kwa sababu mlengwa wa vat final conu
Mfano;
Hatua ya kwanza; Mzalishaji anauza mfuko wa saruji 10,000 ataongeza VAT (18%)
10,000 + 18% = 11,800
Atamuuzia muuzaji wa jumla kwa shilingi 11,800. Baada ya mauzo atawasilisha TRA 1,800 kama VAT aliyokusanya.

Hatua ya pili; Muuzaji wa jumla, baada ya kujumlisha gharama zake zote, amepanga kuuza kwa shilingi 15,000. Katika bei hiyo atajumlisha 18% ya VAT.
15,000 + 18% = 17,700.
Muuzaji wa jumla atauza mfuko huo kwa shilingi 17,700 kwa muuzaji wa reja reja, na kuwaslilisha TRA kiasi cha shilingi 900 kama VAT.

Hatua ya tatu; Muuzaji wa reja reja baada ya kununua, amepanga kuuza mfuko kwa 20,000. Katika bei yake hiyo ataongeza 18% ya VAT.
20,000 + 18% = 23,600.
Atauza kwa mtumiaji wa mwisho kwa shilingi 23,600 na kiwasilisha TRA 900 kama VAT.

VAT Inayolipwa = VAT muuzaji anayotoza katika mauzo - VAT anayolipa katika manunuzi.

Katika hatua ya kwanza; VAT katika mauzo kwa mzalshaji- VAT katika manunuzi.
Ametoza 1,800 katika mauzo, hakuna alicholipa katika manunuzi. Atawasilisha 1,800.

Katika hatua ya pili; VAT katika mauzo kwa muuzaji reja reja - VAT katika manunuzi toka kwa mzalishaji.
2700 - 1800 = 900
Baada ya ku-recover VAT aliyolipa katika manunuzi, muuzaji wa jumla anawasilisha kiasi kilichozidi toka katika VAT aliyotoza, anawasilisha 900 kama VAT.

Katika hatua ya tatu; VAT aliyotoza muuzaji wa rejareja - VAT aliyolipa katika manunuzi toka kwa muuzaji wa jumla.
3,600 - 2,700 = 900
Muuzaji wa reja reja anawasilisha 900 iliyozidi toka katika kiasi alichochaji katika mauzo kama VAT baada ya ku-recover gharama za VAT aliyolipa katika manunuzi.

VAT ilivyolipwa katika mnyororo wa thamani.
Mzalishaji amelipa 1,800 + Muuzaji wa jumla amelipa 900 + Muuzaji wa reja reja amelipa 900 = 3,600

Katika mnyororo mlaji wa mwisho amelipa 3,600 kama Vat ( 20,000*18%). Ni kodi ya mlaji katika dhana ya kuwa, mlaji hayuko katika nafasi ya ku-recover kiasi alicholipa kama agents wengine katika mnyororo wa thamani.

Agents wengine ni wakusanyaji tu wa kodi hii, huwasilisha kilichozidi baada ya kufidia kile walicholipa kama VAT wakati wa manunuzi. Agent hurudishiwa (Refunded) ikiwa tu itathibitika alichotoza katika mauzo kama Vat ni kidogo kuliko alicholipa katika mauzo, tofauti iliyopo atafidiwa.

Nadharia ya VAT kwa ufupi.
Umeielezea vizuri sana vat.
 
Ndivyo inavyo takiwa iwe lkn tra hawapigi hivyo mahesabu yao, hao tra wanapiga from total sales
 
Ukiangalia kwa jicho la ndani zaidi, inazidi kwani. 18% ya mwanzo inaenda kujumuishwa kwenye 18% ya pili pia hizi zote zinaenda kujumuishwa kwenye hesabu ya mwisho kama multiple ya kila moja, ukiacha jumla yake kuu.

Yaani:
1: Mzalishaji: VAT 18%
2: Muuzaji jumla: VAT1*18% + VAT18%
3: Rejareja VAT1×18%+VAT2×18%+VAT3

Suluhisho: A
1: Mzalishaji: VAT 18% ya uzalishaji na faida yake.
2: Muuzaji jumla: VAT Gharama zilizoongezeka kutoka 1 hapo juu na faida yake × 18%
3: Gharama zilizoongezeka kutoka2 na faida yake ×18%

AU
SuluhishoB
Kila bei kwenye stage zote tatu itozwe kila moja itozwe 6%, 6%×3 stages=18%

Athari itapungua japo bado uhalisia upo mbali.
Kwa nini unakwepa kuweka
Suluhisho C:
Itozwe mwenye stage ya kwanza tu kwa kiwango cha 18%? Mbona hii ndiyo best kwani itaiepusha serikali kukimbizana na hao wafanya biashara wa ngazi ya pili na ya tatu. Serikali inakuwa imechukua chake mapema.
 
Dokta vat ililenga kulipwa na mlaji wa mwisho, sio mzalishaji.
Ndo mana kuna ritani zinafanyika kila mwezi kuanzia kwa prodyuza wa bidhaa, wholesaler, retailers wote wanarudishiwa pesa yao waliyoongeza kwenye thamani ya bidhaa. Ili final consumer ndio target yaani yampasa alipe.
Sasa akichajiwa producer wa bidhaa, naona atabebeshwa mzigo mkubwa na pengine hiyo bidhaa ikawa na bei kubwa zaidi.
Hata mfanyabiashara naye ni final mlaji
 
Kwa nini unakwepa kuweka
Suluhisho C:
Itozwe mwenye stage ya kwanza tu kwa kiwango cha 18%? Mbona hii ndiyo best kwani itaiepusha serikali kukimbizana na hao wafanya biashara wa ngazi ya pili na ya tatu. Serikali inakuwa imechukua chake mapema.
Yap, nilisahau hii. Ndo uzuri wa majadiliano.
 
Hata mfanyabiashara naye ni final mlaji
Weee tangu lini mfanya biashara akawa mlaji? By definition mfanya biashara ni mtafutaji faida to the maximum. Ukizubaa hata hiyo VAT anaichukua kama faida yake kwa mbinu zo zote zile hata kama ni kuwahonga kiasi fulani hao maafisa wa TRA watakaoenda kuidai, kutoa risiti fake na kadhalika.

Hata kwenye kodi ya mapato ambayo ndiyo kodi kila mfanya biashara anapaswa kuilipa serikali kuna udanganyifu mwingi mfanya biashara hufanya ili kodi hiyo iwe ya chini sana. Kodi hii ya mapato ni 30% ya faida aliyopata mfanya biashara kwa kila mwezi. Sasa utategemeaje mfanya biashara aiambie TRA ukweli wa kiasi cha faida aliyopata? Si atawaambia alipata hasara au faida kidogo tu. Sasa TRA watajuaje au wataikadiriaje hiyo kodi ya mapato ya mfanya biashara kama siyo kwa maelewano yaliyogubikwa na rushwa kwa maafisa wa TRA? Ndiyo maana maafisa wa TRA wengi ni mabilionea. Na faida ya mfanya biashara si inaanza kupatikana baada ya kurejesha mtaji aliouwekeza kwenye hiyo biashara yake? Hivyo ni mtumishi wa umma tu (toa wabunge na spika wao) ndiye mtu pekee anayelipa 30% ya mapato yake kwani serikali huyakata moja kwa moja kutoka kwenye chanzo cha mshahara wake na posho zake. Waajiriwa kwenye makampuni binafsi nao si rahisi kukwepa makato hayo ya PAYE ingawa makato yao hayo mara nyingi yayapelekwi kwa serikali bali huchukuliwa na waajiri wao kama faida ya biashara zao. Huo ndiyo ukweli wa mifumo yetu ya kodi ulivyo.
 
Ukiangalia kwa jicho la ndani zaidi, inazidi kwani. 18% ya mwanzo inaenda kujumuishwa kwenye 18% ya pili pia hizi zote zinaenda kujumuishwa kwenye hesabu ya mwisho kama multiple ya kila moja, ukiacha jumla yake kuu.

Yaani:
1: Mzalishaji: VAT 18%
2: Muuzaji jumla: VAT1*18% + VAT18%
3: Rejareja VAT1×18%+VAT2×18%+VAT3

Suluhisho: A
1: Mzalishaji: VAT 18% ya uzalishaji na faida yake.
2: Muuzaji jumla: VAT Gharama zilizoongezeka kutoka 1 hapo juu na faida yake × 18%
3: Gharama zilizoongezeka kutoka2 na faida yake ×18%

AU
SuluhishoB
Kila bei kwenye stage zote tatu itozwe kila moja itozwe 6%, 6%×3 stages=18%

Athari itapungua japo bado uhalisia upo mbali.
Suluhisho B haliwezi kuwa sahihi maana kuna baafhi ya bidhaa zinapita kwa suppliers zaidi ya 10, kabla ya kumfikia mlaji, utaigawa vipi hii Vat.
 
Kwa nini unakwepa kuweka
Suluhisho C:
Itozwe mwenye stage ya kwanza tu kwa kiwango cha 18%? Mbona hii ndiyo best kwani itaiepusha serikali kukimbizana na hao wafanya biashara wa ngazi ya pili na ya tatu. Serikali inakuwa imechukua chake mapema.
Ukitoza Vat kwenye stage ya kwanza tayari unakuo umeondoa dhana nzimaa ya Vat.
Kumbuka hii ni kodi ya mlaji, wafanya biashara hata wawe 10 kwenye mnyororo hawapaswi kulipa hii kodi, wao mi wakusanyaji tu.
 
Hata mfanyabiashara naye ni final mlaji
Mfanya biashara hawezI kuwa mlaji, yeye ni mtengeneza faida tu, na tayari kwemye mifumo ya kodi kuna kodi kadhaa analipa ikiwemo mapato,
Mfanya biashara anayeuza mbolea kwa mfano, anakuwaje mlaji wakati mbolea anatumia mkulima namtumbo huko?
 
Sssa wakifunga biashara iyo serikali itachukuwa wapi iyo Kodi?kifupi ni kwamba mifumo yetu ya Kodi ni mibovu na mtu mweusi alivyi na akili mzito na uoga mwingi kufanya maboroshe ya huu mfumo serikali itaendelea kukosa Kodi siku zote.unamuumiza mlaji na kumlinda mzalishaji aisee hii ni changamoto
Wafanyabiashara tulipe kodi kama wanavyolipa watumishi. Yaani endapo Serikali ingesema ikomae wafanyabiashara walipe kodi kama inavyotakiwa nadhani zaidi ya 50% wangefunga biashara. VAT ipo kila nchi. HAIKWEPEK
 
Wafanyabiashara tulipe kodi kama wanavyolipa watumishi. Yaani endapo Serikali ingesema ikomae wafanyabiashara walipe kodi kama inavyotakiwa nadhani zaidi ya 50% wangefunga biashara. VAT ipo kila nchi. HAIKWEPEKI.
Kiranga kasema Marekani waliikataa.
 
Kuna mtu wa kusimama kidete? serikali yetu ni ya watu wasiofikiria kwa upana na siioni km Wana malengo ya kumsaidia mtanzania, watanzania wako na Hali mbaya sana kiuchumi na ndio wanabeba zigo ILO la kodi.alafu Huwa nashangaa Hawa jamaa Huwa wanadai tunasimamia Sheria tulizojitungia sisi wenyewe Huwa nacheka sana.
Tatizo ni ugumu na gharama kubwa wa kumpata na kumfuatilia huyo muuzaji wa mwisho aka wa reja reja. Hawa ni wengi. Ni wengi sana na wako kwenye kila kichochoro cha nchi yetu hii kubwa.

Wazalishaji ni wachache. Wanajulikana sehemu waliko. TRA ni rahisi kuwafikia, wakaona kilichozalishwa na kukiwekea lable ya TRA. Watajua kiasi kilichouzwa na vat yake kwa usahihi bila udanganyifu wo wote. Vivyo hivyo kwa bidhaa zinazoingia kwenye mipaka yetu rasmu kutoka nje.

Ifananishe VAT na chumvi ya iodine inayozuia uvimbe wa tezi ya shingo (goiter). Ni rahisi sana kuifikisha chumvi hii kwa kila mwananchi kama utaiweka kwenye vyanzo vyao vya maji ya kunywa ie kwenye uzalishaji. Utapata taabu sana kuifikisha kwa kila mwananchi kama utatumia njia ya kumfikia kila mwananchi nyumbani kwake na kumwekea chumvi hiyo kwenye mtungi wake wa maji ya kunywa ie retailers. Kwanza utakuwa una mkera na unaweza kusambabisha ugomvi na yeye. Hivyo njia rahisi ni hiyo kwenye chanzo bila hata yeye kujua kwamba kawekewa chumvi ya vat! Atainywa tu. Hata huyo retailer na wholesaler wala hatajua kabeba na chumvi ya vat kwenye bidhaa anazouza. Very simple lakini TRA njia hiyo hawaitaki kwani itawanyima masilahi yao binafsi. Inabidi Mama asimame kidete.
kusi
 
Lazima tujue hizo Kodi za Viwanda kwanza ndio tujadili mantiki ya VAT hapo kiwandani maana Serikali isingeiweka hapo Kwa mzalishaji kama ana Kodi zake zingine ,ingeweza kuweka tuu Kwa wholeseller na Retailers.
Viwanda na wazalishaji wana corporate Tax ambayo ni 30% ya mapato ghafi, hii kodi inalipwa kila wanapopata faida.
Yeyote anayevuka was threshold ya 100 milions kwenye turnover kwa mwaka anatakiwa ajisajili kuwa wakala wa kukusanya Vat. Viwanda vingi kwa mantiki hii ni mawakala wa kukusanya Vat, kwa kila wanachouzza wataongeza kodi hiyo na wataiwakilisha serikalini kabla ya kila tarehe 20 ya kila mwezi.
Lengo la serikali ni kukusanya kodi hii kila bidhaa inapopanda bei kwenye myororo wake, kama bidhaa hii inapita kwenye wafanyabiashara 10, basi serikali inachukua kodi hii mara 10. Kwa sababu kila mfanya biashara huongeza bei ya bidhaa ili apate faida.
 
Unadhani Kwa nini Serikali iweke VAT Kwa producer ambae mwisho wa siku atakuja kurudishiwa Kwa njia ya returns? What is the logic behind?
Producer halipi Vat, yeye ni mkusanyaji tu wa kodi hiyo. Kuna wakati procucer huyu anafanya manunuzi pia, hapo sasa scenario inabadilika yeye anakuwa mlaji.
Kimachoitwa Returns ni mahesabu ya mauzo na manunuzi ya vat. Mfano kiwanda x kimefanya mauzo ya mil 10 vat lakini hapo hapo kikanunua matairi kwa ajili ya magari yake, hapo kiwanda kitalpa Vat. Labda mil2
Returns zitakuwa 10 - 2 = 8 mil, mwenye kiwanda kauza 10 mil ila atawakilisha serikalini 8 milions kwa sababu alifanya matumizi ya 2 mil. Unaweza kudhani serikali imesamehe hii 2 mil, hii 2 mil itaenda kulipwa na huyo aliyeiuzia kiwanda matairi, maana na yeye ni wakala pia.
 
Ukweli ni kwamba kila mtanzania kuanzia akiwa tumboni mwa mama yake analipa kodi ya serikali bila yeye kujua kodi hiyo iko kwenye mfumo wa indirect taxation.

Mfumo huu ni very friendly na hakuna mtu wa kuukwepa hata kama ni mtoto mchanga. Kodi hii iko kwenye kila bidhaa au huduma anayonunua. Mama mjamzito hugawana chakula na mtoto wake aliye tumboni ambacho kalipia kodi.

Tatizo letu ni huu mfumo wa VAT wa kukusanya hiyo indirect taxes za bidhaa na huduma ambazo kila mtanzania hununua. Yaani mfumo uko complex uliojaa ujanja mwingi unaotoa mianya mingi kwa pesa hizo nyingi kuishia kwenye matumbo ya wajanja.

Mfumo wenyewe uko hivi: Chukua mfano kiwanda kinachozalisha bidhaa fulani hususani sementi. Baada ya uzalishaji kiwanda kinapanga kuuza hiyo sementi TZS 10,000 kila mfuko kikiwa kimezingatia gharama na faida ya uzalishaji huo na ushindani wa soko uliopo. Serikali haingilii bei hiyo ya mwenye kiwanda (which is very good).

Badala yake inamwambia serikali inamwambia huyo mwenye kiwanda aongeze TZS 2,000 kwenye kila mfuko ambayo itakuwa ni kodi ya serikali atakapoiuza (sales tax). Hadi hatua hiyo bado ni very good.

Tatizo na ujanja unaanzia baada ya hatua hiyo. Serikali inamwambia huyo mwenye kiwanda kwamba hiyo TZS 2,000 kwa kila mfuko serikali itamrudishia mwenye kiwanda baada ya serikali (TRA) kupata (VAT) tax returns kutoka muuzaji wa mwisho wa rejareja (retail) aka mmachinga huko Sumbawanga.

Mwenye kiwanda huuza bidhaa zake kwa wholesalers. Hivyo mfuko mmoja wa sementi mwenye kiwanda atamuuzia wholesaler kwa TZS 12,000. Huyu wholesaler naye atapanga bei atakayoiuza hiyo sementi huko Sumbawanga akizingatia gharama ya usafirishaji, faida yake na ushindani wa soko. Bei yake inaweza ikawa TZS 15,000 kwa kila mfuko. TRA itamwambia aongeze TZS 2,000 kama kodi ya serikali (VAT) ambayo atarudishiwa baada huyo atakayemuuzia (retailer) kurejesha tax returns. Hivyo wholesaler atamuuzia retailer mfuko mmoja wa sementi kwa TZS 17,000.

Huyo retailer naye atapanga faida yake na kuona aiuze kwa TZS 20,000. Naye TRA itamwambia aongeze TZS 2,000 kwenye bei hiyo kama VAT na atoe risiti na tax returns. Hivyo bei ya mfuko mmoja wa sementi anaiuza kwa mlaji kwa TZS 22,000.

Katika mfumo huo wa VAT huyo retailer anatakiwa kuandaa na kuwakilisha VAT returns za bidhaa aina zote alizouza kila mwezi ili kuwezesha hao wholesalers na wenye viwanda (source) warejeshewe hizo TZs 2,000 zao. Yeye harudishiwi cho chote.

Mlaji wa mwisho anakuwa ameongezewa TZS 2,000 mara tatu kwenye hiyo thamani ya bidhaa lakini serikali sana sana inaambulia TZS 2,000 tu! Hapo utaona kuna myanya ya wenye viwanda na wholesalers kurejeshewa hizo TZS 2,000 kwa maelewano tu na maafisa wa TRA.

Hapo utaona mapambano ya maafisa wa TRA na retailers kuhusu risiti na tax returns ambao huishia mara nyingi kwa retailers kutoa rushwa kwa maafisa hawa.

Hivyo ndivyo ulivyo mfumo huu wa VAT kwa bidhaa zingine zinazotoka nje ya nchi na ndani ya nchi. Inashangaza zaidi kuwa hata bidhaa zinazozalishwa na taasisi zinazomilikiwa kwa asilimia 100% na serikali nazo zinawekewa kodi ya serikali, yaani serikali inajitoza kodi?

Shirika kama la TANESCO miradi yake imejengwa kwa pesa yetu (kodi zetu). Hata kama baadhi ya pesa iliyotumika tulikopa nje bado kodi zetu zitalipa hilo deni letu. Ni shirika letu, sasa linawezaje kututoza kodi? Sisi ndiyo wenye mamlaka ya kupanga umeme tulipe kwa bei gani ili kuwezesha kulipa mishahara na other charges (OC) za shirika letu zilizopitishwa na bunge letu la bajeti. Ziada ikipatikana inaweza kugharimia mambo mengine hususani madawa na vifaa tiba.

Hitimisho: VAT is nothing but a sales tax. Itozwe mara moja tu kwenye chanzo ya hiyo bidhaa. Kama bidhaa inazalishwa hapa nchini basi huyo mwenye kiwanda pekee ndiye atozwe/ akusanye hiyo kodi na kuiwakilisha serikalini baada ya kuuza bidhaa hiyo.

Hao wholesalers na retail sellers na machinga haiwahusu maana serikali itakuwa ilishachukua kilicho stahili yake. Kama bidhaa inatoka nje ya nchi, serikali ichukue kodi yake pale pale mipakani inapoingilia.

Kwenye zingine kama zile za kilimo na mifugo kodi hii ilipwe kwenye minada mikubwa kutoka kwa wafanya biashara wakubwa wanaonunua bidhaa hizo. Mambo ya kurudishana kodi yawe mwisho.

Kazi ya watumishi wa TRA iwe kwenye maeneo haya tu na kushirikiana na polisi kunasa bidhaa zinazoingia kwa magendo kupitia panya routes. Serikali ni moja. Mambo ya kodi za serikali za mitaa na kodi za serikali kuu (TRA) hayana maana kwa mwananchi.

Zote kwake ni za serikali, wao watajua wanagawana vipi. Mambo ya direct taxations tuachane nayo au yapunguzwe kabisa. Yana maudhi sana na kuwafanya wananchi waichukie serikali yao. Imagine kama kodi ya kichwa ikarejeshwa hata kama ni buku moja tu kwa kila kichwa kwa mwaka, unadhani itakuwaje?
Asante sana kwa huu uchambuzi, nchi hii wananchi wanabebeshwa mzigo mzito na kinachopatikana kinaishia mifukoni mwa wachache.
 
Wataalamu wa kodi wafuatilie mfumo wa kodi wa nchi ya Canada ambao kinacho rudishwa kwa jamii kinaoneka dhahiri na hurudishwa pia kwa mlipa kodi ,(as an individual), yaani kwako mwenyewe mlipa kodi, mfano endapo mlipa kodi atasimamishwa kazi ama akipata changamoto ,mfumo umtambue huwezesha kumlipia kodi ya nyumba na posho ya chakula kwakifupi uwe ni mfumo ambao kila mmja apate faida nao usipo utumia inakula kwako
Hata nchi za ulaya wanafanya hivi.
 
Hata nchi za ulaya wanafanya hivi.
Hawa wataalamu wetu tena wanaoitwa wabobezi wamebobea kwenye nini, labda wamebobea kwenye mifumo ambayo inawanufaisha wao, kwakifupi mfumo wetu wa kodi hauko wazi, (not even competitive)
 
Back
Top Bottom