Mfano;
Hatua ya kwanza; Mzalishaji anauza mfuko wa saruji 10,000 ataongeza VAT (18%)
10,000 + 18% = 11,800
Atamuuzia muuzaji wa jumla kwa shilingi 11,800. Baada ya mauzo atawasilisha TRA 1,800 kama VAT aliyokusanya.
Hatua ya pili; Muuzaji wa jumla, baada ya kujumlisha gharama zake zote, amepanga kuuza kwa shilingi 15,000. Katika bei hiyo atajumlisha 18% ya VAT.
15,000 + 18% = 17,700.
Muuzaji wa jumla atauza mfuko huo kwa shilingi 17,700 kwa muuzaji wa reja reja, na kuwaslilisha TRA kiasi cha shilingi 900 kama VAT.
Hatua ya tatu; Muuzaji wa reja reja baada ya kununua, amepanga kuuza mfuko kwa 20,000. Katika bei yake hiyo ataongeza 18% ya VAT.
20,000 + 18% = 23,600.
Atauza kwa mtumiaji wa mwisho kwa shilingi 23,600 na kiwasilisha TRA 900 kama VAT.
VAT Inayolipwa = VAT muuzaji anayotoza katika mauzo - VAT anayolipa katika manunuzi.
Katika hatua ya kwanza; VAT katika mauzo kwa mzalshaji- VAT katika manunuzi.
Ametoza 1,800 katika mauzo, hakuna alicholipa katika manunuzi. Atawasilisha 1,800.
Katika hatua ya pili; VAT katika mauzo kwa muuzaji reja reja - VAT katika manunuzi toka kwa mzalishaji.
2700 - 1800 = 900
Baada ya ku-recover VAT aliyolipa katika manunuzi, muuzaji wa jumla anawasilisha kiasi kilichozidi toka katika VAT aliyotoza, anawasilisha 900 kama VAT.
Katika hatua ya tatu; VAT aliyotoza muuzaji wa rejareja - VAT aliyolipa katika manunuzi toka kwa muuzaji wa jumla.
3,600 - 2,700 = 900
Muuzaji wa reja reja anawasilisha 900 iliyozidi toka katika kiasi alichochaji katika mauzo kama VAT baada ya ku-recover gharama za VAT aliyolipa katika manunuzi.
VAT ilivyolipwa katika mnyororo wa thamani.
Mzalishaji amelipa 1,800 + Muuzaji wa jumla amelipa 900 + Muuzaji wa reja reja amelipa 900 = 3,600
Katika mnyororo mlaji wa mwisho amelipa 3,600 kama Vat ( 20,000*18%). Ni kodi ya mlaji katika dhana ya kuwa, mlaji hayuko katika nafasi ya ku-recover kiasi alicholipa kama agents wengine katika mnyororo wa thamani.
Agents wengine ni wakusanyaji tu wa kodi hii, huwasilisha kilichozidi baada ya kufidia kile walicholipa kama VAT wakati wa manunuzi. Agent hurudishiwa (Refunded) ikiwa tu itathibitika alichotoza katika mauzo kama Vat ni kidogo kuliko alicholipa katika mauzo, tofauti iliyopo atafidiwa.
Nadharia ya VAT kwa ufupi.