Kofi moja tu akasema watoto sio wangu

Kofi moja tu akasema watoto sio wangu

Zingatia neno la kwanza
Watoto sio wako
 
KUPIGA NI KOSA KISHERIA.
Wengi wameua au wameuwawa kupitia ugomvi,kusababishiana ulemavu wa kudumu,na kadhalika.
Hakuna mtu yeyote mwenye haki ya kumpiga mtu yeyote kwa sababu yoyote ile.
Watu wengine wamejikuta kwwnye kesi na kujikuta wanalipa gharama kubwa kama fidia au faini kutokana na kukosa kushindwa kuzuia hasira zao na kuwashambulia shambuliobla kimwili PHYSICAL VIOLENCE,EMOTIONAL VIOLENCE
Mara nyingi unapompiga mtu unatumia nguvu kumdhuru mwili na pia una muathiri kisaikolojia pia unamdhalilisha na kumnyanyasa.GBV hasa mwanaume ukimshambilia mwanamke ni UNYANYASAJI WA KIJINSIA.
Sasa haya yote ni madhara hasi.
Haishauriwi sana kujichukulia sheria mkononi hata kama ni mke wako.Mimi naamini mtu mzima huwezi kumbadilisha au kumrekebisha tabia,hasa kwa kutumia nguvu mabavu.Ni bora kuachana kwa usalama kama imefikia hatua ya kushindwa kuelewana kwa njia nyingine za amani.
Umeishi ulaya nini? Nusu ya wanawake wa rika la mama zetu wamewahi kupigwa
Wengine bila makofi hawaendi
 
UKATILI dhidi ya wanawake na watoto ni kosa hata ukatili kwa wanayama .
Na wewe mwanaume ukimkosea mtoto au ukimkosea mke wako nani akupige akuadhibu akupige kofi.Kusema wanawake bila kofi hawaendi si sahihi kisheria ni kosa.Hata kimpiga mtu yeyote kupigana au kupiga siyo njia sahihi ya kutafuta suluhisho au kutatua changamoto.
Haina afya kupiga,kupigana,sio sahihi,si busara,ni kuvunja haki za wengine(KOSA KISHERIA).
Na utetezi wa kujitetea kuwa mwanamke bila kofi haendi kwamba ulikuwa unamfundisha adabu au kumkanya kwa kumpiga sio utetezi wenye mashiko.
 
Ugomvi ugomvi piga ngumi piga mateke nikamuotea kofi moja tu
Akapiga kelele hatari na kuropoka ,naondoka na wanangu,nikamwambia haondoki mtoto hapa akajibu,thubutu......naondoka nao, kwanza sio watoto wako,una jeuri ya kuzaa watoto wazuri hivyo,hujioni hilo komwe.

Akaondoka kweli ila wazazi wakasuluhisha yakaisha,
Kwenye kikao cha usuluhishi mke anasema watoto ni wa mumewe ila aliongea tu kwa hasira kumrusha roho jamaa, kupima DNA wazee wamesema aachane nayo.

Sasa amerudi na wale watoto,ndoa ngumu jamani,ikitokea mtoto akadhurika suspect number 1 ni mimi

NB sio mimi ila ni mtu yamemkuta,mimi ningesha wanyonga hao machalii
Haya mambo ni magumu sana. Ukisikiliza na ukasikiliza tena, huwa upande mmoja unajihalalishia kuchepuka na kuzaa huko nje bila shida. Huu upande mwingine hauna mtetezi maana wenye midomo wote wako ule upande wa pili. Siku moja mimi na mke wangu tulikwenda kumjulia kaka mkubwa wa rafiki yangu. Alipata ugonjwa mbaya sana hata sikujua ulikuwa ugonjwa gani, maana alikuwa 'disfigured'. Macho yote mawili yaliharibika, alikuwa tu kama hana macho, na ngozi yake pia. Lakini mkewe alikuwa ndiye akimuuguza hospitali. Then, inaonekana alichokisema na wote tuliokuwepo tulikisikia, ni kumwomba mkewe samahani kwa kumkosea sana. "Mke wangu umeshamisamehe," alisikika akisema. "Nilisema nimeshakusamehe," alisema mkewe. Kwa kifupi, ni kwamba muda wote alioishi na mkewe takribani miaka 40+ hakuwahi amemwambia mkewe kwamba amezaa nje pia besides watoto wake na huyo mkewe. Hivyo, hadi huu ugonjwa ulivyomshika na alipoona hana matumaini ya kupona, ndipo ikabidi tu amwambie mkewe, ambaye muda wote aliamini watoto wake na mumewe ni hao tu waliokuwa nao nyumbani (waliofahamika kwa wote wawili kabla ya ugonjwa huo wa hatari kumshambulia huyo kaka). Baada ya kutoka hapo hospitalini, haikuchukua muda Mungu akawa amemuita. Jaribu kufikiria huyo shemeji alilipokeaje hilo, kwa mtu aliyemwamini miaka 40+, kumbe wapi! Hivyo, haya mambo ni magumu sana. Ukisikia tu ya upande mmoja, unaweza kuwa 'judgemental'. Kuna simulizi lingine, jamaa alikuwa 'anamla' binti yake. Mara nyingi alionekana kama anampa ushauri, kumbe ilikuwa gia ya kumtoa mke wake pale aendelee na kazi zake, then jamaa afanye mambo yake. Siku moja, baba mtu kamkalisha binti, kama kumpa ushauri hivi, mkewe alivyoona hivyo alijifanya anachukua jembe kwenda shambani (na shamba lilikuwa mbali almost kilomita 5 hivi). Mkewe alipoondoka, jamaa kaingia ndani ya nyumba na kumwita Binti ndani (au alivyoingia ndani binti yake alimfuata). Mkewe akajifanya amesahau kitu, akarudi na akakuta pale nje hakuna mtu na mlango umefungwa. Akanyemelea na kusikiliza akadikia sauti ya watu waliolala chini (kwenye mkeka). Akatunza moyoni. Siku nyingine, alikutwa kadi la kliniki limefichwa, na kwenye kadi kuna jina la mumewe...yaani binti alipimwa, akakutwa na ujauzito...sasa kulikuwa kunafanyika mbinu hiyo mimba itolewe...mkewe akalipua bomu! Haya mambo magumu sana! Unaweza ukasikiliza tu sehemu moja, lakini ukisikiliza sehemu zote mbili utagundua kwamba a human being is a mystery! Ngoja nitulie kwanza.
 
Stori za Deep pond hizi
 
Stori za kupika hizi
 
Kwahiyo we ukiambiwa hivyo basi unaishiwa nguvu unamrudisha mwanamke ndani 🤣🤣🤣
Kwetu ukizaa na mke wa mtu jamaa anachukua mtoto. Halafu uende kudai kwamba ni mtoto wako, hapo ndipo mtakapoulizana, huyo uliyezaa naye ulimwoa au ulimtolea mahari lini? Ila kwetu mara nyingi naona watu wako 'cool' kwa mambo haya kwamba mtoto anayezaliwa ndani ya familia ni mali ya baba (yaani baba yake ndiye huyo aliye na mama yake). Watu wengine Wana msemo "aliyemwoa mama ndiye baba yangu".
 
Stori za kupika hizi
Yaani hiyo iliyosemwa au hii ya kwangu au zote mbili? Za kwangu ni real in space and time. Tena ninazo nyingi tu ambazo nimezishuhudia: baadhi waliomba usuluhishi, baadhi yalikuwa maneno ya "umemwaga ugali, ngoja na mimi nimwage mboga" na baadhi nilikuwa msikilizaji, nikisikia wahusika wenyewe wakisema: mmoja akisema jambo x, mwingine anasema jambo y na wanatajiana mashahidi (kama huamini kamuulize p na q au hata t na z).
 
Kuwa makini sana maneno anayosema mtu pale tu akiwa na hasira, au emotional state yyte ile. Kuna vitu vinaibuka automatically, lazima tujifunze namna ya kujidhibiti pale tunapokuwa kwenye hisia zisizo za kawaida.
 
Sasa mkuu ukishakuwa kwenye hisia zisizo za kwaida si tayari umeshashindws kujidhibiti?
 
Hapana, hisia huwa mara nyingi ni ngumu kuzikwepa, lakini kudhibiti hisia zisilete mambo mengine zaidi inawezekana kabisa, lazima ujifunze kuwa mtulivu.

Hisia ambazo si za kawaida, namaanisha ni zile ambazo hatukuzizoea au ambazo si za Kila mara mfano hasira, huzuni nk. Unaweza kuwa kwenye Hali ya hasira na ukaweza kudhibiti hasira yako isizue au kuleta makubwa zaidi, waswahili husema Bora nusu shari...wengine hufikia kuua kabisa na wengine huacha yapite, udhibiti Kila mmoja ana kiwango chake.
 
Ugomvi ugomvi piga ngumi piga mateke nikamuotea kofi moja tu
Akapiga kelele hatari na kuropoka ,naondoka na wanangu,nikamwambia haondoki mtoto hapa akajibu,thubutu......naondoka nao, kwanza sio watoto wako,una jeuri ya kuzaa watoto wazuri hivyo,hujioni hilo komwe.

Akaondoka kweli ila wazazi wakasuluhisha yakaisha,
Kwenye kikao cha usuluhishi mke anasema watoto ni wa mumewe ila aliongea tu kwa hasira kumrusha roho jamaa, kupima DNA wazee wamesema aachane nayo.

Sasa amerudi na wale watoto,ndoa ngumu jamani,ikitokea mtoto akadhurika suspect number 1 ni mimi

NB sio mimi ila ni mtu yamemkuta,mimi ningesha wanyonga hao machalii
Mtu akichukia anachowaambia nichakweli
 
Back
Top Bottom