ukomandoo ni mafunzo ya medani za kivita, asikari jeshi anaweza kuwa komando ilihali hana cheo chochote yaani private, lakini pia katika mission za kijeshi anayeongoza platoon yoyote ya makomandoo lazima awe amewazidi cheo cha uafisa wale makomandoo anaowaongoza kwenye mission,
Pia ifahamike kuwa asikarijeshi kuwa komando hakumuweki kuwa juu ya maafisa wengine walio juu yake hata kama sio komando, komando ni kikosi ndani ya jeshi hivyo wako chini ya wakuu wa vikosi na kamandi husika.
kazi ya kikosi cha komandoo ni kufanya missions ngumu, kwenye mazingira magumu na hatari ( ambapo asikarijeshi wa kawaida hawezi kutekeleza jukumu hilo) na haraka zaidi ( commando is a time keeper personnel).
kuna madaraja ya ukomandoo, hapa Tanzania vijana kutoka RTS yaani shule za mafunzo za jwtz huchukuliwa na maafisa wa jwtz kutoka kikosi cha komando kwa kuzingatia uimara, mwonekano, nidhamu, saikolojia n.k, vijana hawa hupelekwa kwenye mafunzo ya komando daraja la tatu (commando level 3) pale Ngerengere- sangasanga 92kj- Morogoro kwa miezi 18, baada ya hapo hupelekwa course za kiutendaji vitani. Ila hapa komando anakuwa na nusu mbawa.
by Lt.saguda (a mythical name)