Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza ratiba ya hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB kwa msimu wa 2025/2026, ambapo vigogo wa soka nchini wamepangiwa vibarua vizito mwezi Mei.
Katika ratiba hiyo, klabu ya Simba SC itakuwa mwenyeji wa TRA United ya Chobwedo kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, jijini Dar es Salaam, mchezo unaotarajiwa kuwa wa vuta nikuvute huku TRA wakijaribu kuushangaza ulimwengu mbele ya "Mnyama".
Kwa upande mwingine, mabingwa watetezi Young Africans (Yanga) wamepangiwa safari ya "kijeshi" ambapo watavaana na JKT Tanzania. Mchezo huo pia utapigwa katika dimba la Meja Jenerali Isamuhyo.
Mbali na mechi hizo za Dar es Salaam, ratiba hiyo itazishuhudia timu nyingine zikiumana kutafuta nafasi ya nusu fainali kati ya tarehe 16 na 17 Mei, 2026. Coastal Union "Wagosi wa Kaya" watawakaribisha Singida BS katika dimba la Mkwakwani mkoani Tanga, huku Mashujaa FC wakipepetana na matajiri wa Jiji la Dar es Salaam, Azam FC, katika uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.