Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) Stand United Vs Simba SC, Dimba la Kambarage

Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) Stand United Vs Simba SC, Dimba la Kambarage

Shadeeeya ...nakuuliza wewe Ni me au ke! πŸ˜ƒ πŸ˜ƒ πŸ˜ƒ πŸ˜ƒ πŸ˜ƒ ✌ ✌
 
Maskiniiii. Hivi manara kafikia huku. πŸ€”πŸ€”πŸ€”
 
Michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports Federation Cup (ASFC), hatua ya 16 bora, kupigwa leo February 25, 2020 ambapo Stand United Chama la Wana, wanawakabili Simba SC, Wekundu wa Msimbazi, kwenye dimba la Kambarage mjini Shinyanga.

Stand United ambao wanaoshiriki michuano ya ligi daraja la kwanza FDL, walitinga hatua ya 16 bora baada ya kuwaondosha Majimaji kwa mikwaju ya penati kwa 5-4 baada ya kumalizika kwa dakika 90 kwa sare ya 1-1 kwenye dimba la Majimaji, Songea.

Simba SC ambayo inashuka dimbani katika mchezo huu wakiwa na morali ya juu kabisa huku wakiwa wametoka kuwasha moto kwenye VPL, imetinga 16 bora baada ya kufanikiwa kuwafurusha Mwadui FC kwa jumla ya mabao 2-1

Kocha wa Stand United, Atuga Manyundo amesema, anawafahamu vilivyo Simba ni timu bora, lakini wamejipanga kupambana kuwaondosha Simba, kwani wachezaji wake amewapa mbinu zote.

Kocha wa Simba, Sven Vanderbroeck amesema, kila mmoja yupo tayari kwa mchezo, lakini kwenya mchezo mmoja hatuwezi kuwatumia wachezaji wote 29 hivyo lazima kuchagua wachezaji wa kuwatumia, na kwa huu mchezo labda kutakuwa na mabadiliko machache.

"Mashabiki wetu wajitokeze kutushangilia, tupo kwenye hali nzuri na tutacheza mchezo mzuri" amesema Vanderbroeck.

Huu ni mtanange wa kukata na soka, nani kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya ASFC? wachezaji kuamua ndani ya dakika 90.

Kumbuka mchezo huu wa Azam Sports Federation kupigwa kuanzia saa 10: 00 jioni..Usikose Ukaambiwa

.......Ghazwat....

Wanaoanza SSC:

Beno Kakolanya, Haruna Shamte, Gadiel Michael, Tairone Santos, Kennedy Juma, Gerson Fraga, Hassan Dilunga, Sharaf Shiboub, Meddie Kagere, Ibrahim Ajibu, Shiza Kichuya.

Akiba:

Salmu, Wawa, Mkude, Chama, Kahata, Kanda, Juma.


View attachment 1368862View attachment 1368863
Niliwaambia hii mechi tunashinda
 
Back
Top Bottom