Kombe la Shirikisho: Medeama yaifunga Yanga 3-1 hatua ya makundi

Kombe la Shirikisho: Medeama yaifunga Yanga 3-1 hatua ya makundi

Yanga Makopo Yanga Makopo Simba Imara Simba Imara
 
Hatimaye Mabingwa wa Soka Tanzania Yanga ya Tanzania imekipata cha mtema kuni baada ya kubamizwa bao 3-1 Na miamba ya Ghana.

Visingizio vimeanza Mara uwanja wakati timu zote zimecheza uwanja huo , mbona Ule uwanja hauna tofauti Na uwanja wa Kaunda ambao Yanga ndio wameuzoea?

Yanga acheni visingizio mkifungwa mbona mlishindwa kuwafunga kwenye Uwanja wa Taifa?Hakuna wa kimataifa wote wa matopeni.
 
Kufuatia kipigo cha aibu ilichokipata leo kutoka kwa timu ya Ghana inayoshika nafasi za chini katika msimamo wa ligi ya nchi hiyo, wapenzi na mashabiki wamesema wazi kuwa kunahitajika kusajiliwa kwa walinzi makini.

Yanga imetandikwa bao 3-1 na timu changa ya Medeama ambayo ni ngeni katika ulimwengu wa soka.

Unajua beki namba 3, 4, 5 wamechoka kabisa na ni wazee. Tunataka Manji atupatie walinzi mbadala. Leo tungeweza kufungwa hata bao saba kama wangekuwa makini.

Sura zetu tutazificha wapi, alilalama shabiki mmoja baada ya mpira kwisha. Tutakuwa wapuuzi kama lengo letu ni kuwadhihaki Simba wakati sisi timu yetu mbovu.

Ninashaka na uwezo wa kocha, yaani timu ikizidiwa ndio basi, anawatoa wachezaji tegemeo na kuingiza potelea mbali.
 
Dah! Wana bahati sana hawa ndala, zilikuwa 8 kabisa zile. Yale majamaa yamekosa magoli ya wazi kabisaa!

Halafu nimekumbuka yale matobo waliyopigwa leo ... Hoi kabisa. Mpira hauchezewi kwenye vijiwe vya kahawa jamani!
 
Waache visingizio hao YEBO YEBO, ule uwanja wataulinganisha na uwanja wa MajiMaji Songea? SHAME...
 
Tuliwambia , ngoma ya kitoto haikoshi mikono ya MTU mzma ,mkabisha kikowapi ,mbendembe.....
 
....mpira wa Tanzania bado sana, nasema tena BADO SANA...tuendelee kudanganyana tu, km kawaida yetu!
 
Mtotoo akililia wembe mwache .....atapopata kidonda. Mmnghh titiii
 
Mkuu, Taifa Stars na klabu zake bado hazijafikia level hata ya kufuzu Afcon (and its corresponding competitions). Na kama zikiqualify mara nyingi zimekuwa zikitia aibu. Mfano mzuri ni mechi ya leo (timu ya Yanga). Yaani hadi mtu unashindwa kujipa moyo kwamba wamejitahidi..as ilikuwa ni full aibu kama vile Yanga ni timu kutoka Ndondo Cup. WaTZ lazima tubadilike, otherwise tutaendelea kushangilia timu mbovu mpaka mwisho wa dahari. Yatupasa kuemploy BRN kwenye michezo pia, muda wa maneno bila vitendo umeisha. We must say no to politics katika michezo.
Kushangalia timu sio dhambi haijalishi ikoje km VP hama nchi pia sbb Tz mbovu shabikia Ureno
 
Back
Top Bottom