Kombe la Shirikisho: Yanga yaanza vibaya kwa kukubali kufungwa 2 -1 dhidi ya Pyramids ndani ya CCM Kirumba

Kombe la Shirikisho: Yanga yaanza vibaya kwa kukubali kufungwa 2 -1 dhidi ya Pyramids ndani ya CCM Kirumba

Yanga Bariidii πŸ˜€πŸ˜πŸ˜‚πŸ€£πŸ˜ƒπŸ˜„πŸ˜…
 
HT: Timu bora zinaongoza.
Yanga 0 vs Pyramids 1

Singida 0 vs Simba 1.
 
Yanga watapindua meza tu nina uhakika. Japokuwa mimi naangalia ya Simba sc maana ndiyo yanayo nihusu kwa leo
 
Bora wangechezea taifa wakaongezaa pesa za viingilio kwenye account yao[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Nyie Vyura hamuwezi mpira, nyie mnaweza kuogelea tu pale jangwani. Mpira waachieni simba
 
Kimoja iko mpaka game kwisha
Mabingwa wa kihistoria nchini, Dar es Salaam Young Africa al maarufu kwa jina la Yanga wanaingia uwanjani leo kupambana na timu ya soka ya Pyramids ya kutoka nchini Misri katika mechi ya kwanza ya mtoano kutafuta nafasi ya kuingia kwenye hatua ya mtoano kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho.

Kila la heri wawakilishi wetu wa Tanzania.

Kikosi cha Yanga

Farouk Shikalo
Juma Abdul
Ally Mtoni
Kelvin Yondani
Alli Alli
Feisal Salum
Mrisho Ngasa
Makame Rashidi
Sadney Urikhob
Pappy Tshishimbi
Mapinduzi Balama

UPDATES

Mpira umeanza

5" Yanga 0 - 0 Pyramids

10" Ally Mtoni anapiga shuti kali, golikipa wa Pyramids anaokoa

12" Pyramids wanashambulia lango la Yanga

15" Yanga 0 - 0 Pyramids ---- hawa Pyramids ni warefu na wana miili mikubwa kuliko wachezaji wengi wa Yanga

20" Yanga 0 - 0 Pyramids ---- Yanga wanapata foul baada ya Juma Abdul kufanyiwa rafu; Yanga wanapoteza

22" Yanga wanakosa goli hapa, Ally Ally anapiga kichwa ila namna gani anapiga nje

25" Yanga 0 - 0 Pyramids ---- Mrisho Ngasa anapewa kadi ya njano

35" Yanga 0 - 0 Pyramids ----- Pyramids wanakosa goli hapa

40" Yanga 0 - 0 Pyramids

42" Goal; Pyramids wanapata goli la kwanza kupitia kwa Eric Traore

45" Yanga 0 - 1 Pyramids (Eric Traore)

Mapumziko: Yanga 0 - 1 Pyramids
 
Watu tutamlaumu Zahera bure,

Huko Egypt si ndo alikofichwa yesu ili asiuliweeee.....

Sasa atawaachaje hao jamaa wateseke hapo kirumba, lazima ifanyike namna ambayo si Msolla au Zahera wa kuipindua.
 
Mimi ni Yanga! Nakuthibitishia hilo haliwezekani. Kushinda hii mechi au hata kufuzu tu hatua ya makundi dhidi ya hawa Pyramids ni ndoto ya mchana.

Usajili wa Zahera ni wa kustaajabisha! Jambo la kushangaza, analindwa na viongozi wa timu kana kwamba ameweka hisa zake pale Jangwani. Kiujumla tupambane tu na hali zetu!

Maana kama ni ubingwa, tayari simba watauchukua. Kwenye kombe la Shirikisho la Azam, nako hatuna ubavu wa kupambana kivile!
 
Uongozi wa Yanga eti bado unasubiri miujiza kutoka kwa Zahera. Sjui Zahera kawapa nn wanajagwani? Yanga inaadhilika huku mapro aliowasajili takribani 3 wapo benchi wanapunga upepo tu. Mbaya zaidi timu inacheza ovyo ovyo ovyo kabsa. Ni muda wa uongozi kufanya maamuzi magumu. La sivyo mtaendelea kulokota kunyavu na kuadhilika km msipomtimua huyu Mbuta mbutu wenu. Shauri enu!
 
Yanga nyie ukiangalia sub unashika kichwa.
Kweli Marcelo yule mfupi ndo aje alete mabadiliko ya kuifunga pyramid.
 
Back
Top Bottom