Kombora la Urusi latua sehemu ya maduka makubwa Ukraine

Iliteuliwa na Shetani mnywa damu za watu.
Nasubiri bado kusikia Urusi iliteuliwa na nani??? Labda na Bwana wa Majeshi Madhaifu? Maana ina matatizo kidogo kupata maendeleo??
 
aise mm ,najiskia buridani Sana nikiona vitu vizito Kama hivi vinatua pale kwa zele.na hii kwa Russia ni kakombola ka technology ndogo Sana !!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu, samahani mbona unasema vitu vizito vinatua pale lwa Zele? Je unajua mfano ambako ikulu yake imewahi kupigwa? Je unajua sababu picha tunazoonyeshwa ni zaidi mabomu yanayolipuka penye watu raia?
 
Why uanze kukimbiza watu wanaokimbiakimbia eneo la 3km na precision missile system wakati una bomu linapiga eneo la km 6.. Russian style..you can run you can hide but you will die tired..comrade!! make sure these facist have nowhere else to run or hide.

Sent from my LG-M200 using JamiiForums mobile app
 
UKRAINE unataka kuekwa free kutokana na MAGAIDI waliojaa
RUSSIA kama TAIFA TEULE inataka kuikomboa UKRAINE
Achaneni na PROPAGANDA za hao WAMAGHARIBI[emoji35][emoji35][emoji34]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
UKRAINE unataka kuekwa free kutokana na MAGAIDI waliojaa
RUSSIA kama TAIFA TEULE inataka kuikomboa UKRAINE
Achaneni na PROPAGANDA za hao WAMAGHARIBI[emoji35][emoji35][emoji34]

Sent using Jamii Forums mobile app
Unaulizwa kuhusu ushahidi huna! Urusi Taifa Teule ya nani au nini?? Urusi ndiye mkoloni mkubwa duniani (ardhi yote kutoka baada ya Moscow hadi Wladiwostok ni makoloni yake...) - hii husikii kutoka Wamagharibi ambao hawapendi kukumbushwa kuhusu ukoloni ambamo walishindana na Urusi.

Taifa teule linaloua watu wa Afghanistan, Georgia, Chechnya, Syria, Ukraine? (kwa ubaya na uwongo sawa jinsi Marekani iliua watu Iraki, Afghanistan, Vietnam) . . .
Nchi inayojaribu sasa kurudisha ukoloni wake juu ya Ukraine ? Na kufanya makelele ya kurudisha ukoloni Lithuania?
 
Kama kigezo cha kuua watu ndio inafanya isiitwe Russia taifa teule vp kuhusu Israel wanavyofanya mauaji kwa wanawake na watoto huko palestina na bado mnaita taifa teule maana sababu zinazofanya Israel kufanya mauji Palestine ni sawa na Russia wote wanaangalia usalama wa nchi zao
 
Ustadh mimi simwiti yeyote taifa teule isipokuwa ninafuata hapa lugha ya marafiki wa Putin. Katika miezi michache ya vita yake Putin ameshasababisha vifo vingi kushinda mapigano yote ya Israeli kwa miaka mingi.
Ursui ni taifa lililoteuliwa (na nani?) kuonyesha kwamba watoto wa ukombozi hawatambui tena ukoloni wakimshangilia mkoloni mkubwa duniani ambaye ni Urusi.
 
Mkuu heshima kwako, nmekuelewa sana
 
🤝🤝🤝👏👏👏Akijibu cha maana najitoa JF
 
Bucha waliochinjwa hawakukimbia. Ni watu waliobaki mjini. Kumbe facist walibaki kwa hiari, wengine waliwahi kukimbia? Watoto na mababu waliochinjwa Bucha walikuwa wafashisti??
Au watu raia dukani ni fashisti? We Bwana umethibitisha maono ya wengone wanaosema:
Putin anataka kukamata Ukraine bila watu wake . Ambayo ingekuwa ufafanuzi wa "genocide".
Au unaonaje??
 
RUSSIA anapambana na MAGAIDI hivyo Auto anakua MTEULE

Sent using Jamii Forums mobile app
 
BUCHA hakuchinjwa hata mjusi achaneni na PROPAGANDA
Kama kweli walichinjwa NATO kwanini hawajaingilia kusaidia RAIA kama walivyofanya kule LIBYA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
BUCHA hakuchinjwa hata mjusi achaneni na PROPAGANDA
Kama kweli walichinjwa NATO kwanini hawajaingilia kusaidia RAIA kama walivyofanya kule LIBYA

Sent using Jamii Forums mobile app
Acha ndoto zako za uwongo. Kuna mashahidi tele. Walieleza kwa upana na urefu walichoona na jinsi walivyoteswa wakati wa uvamizi wa jeshi la Putin. Na jinsi ndugu, watoto, wazazi wao walivyouawa hovyo.
 
RUSSIA anapambana na MAGAIDI hivyo Auto anakua MTEULE

Sent using Jamii Forums mobile app
Kabisa, Utam!! Anayempinga mungu wako Putin, au anayekutwa kwenye njia ya mashujaa wa Taifa Teule, ndiye gaidi! Ni rahisi kabisa! Kama Chechniya, kama Syria, kama Ukraine, kama mtoto wa miaka 2 au mzee wa miaka 82. Gaidi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…